Kutafakari kuhusu Hek 12, 13.16-19; War 8,26-27; Mt 13,
24-43
Kulingana na tafakari yetu katika wiki
iliyopita, kati ya mbegu zilizoanguka kwenye ardhi, moja peke yake ilipatikana
kuwa hali nzuri ili kupokea mbegu njema na kuzaa matunda. Mbegu njema ni neno
la Mungu ambalo lina nguvu ndani yake ili kuzaa maisha mapya katika mahali
linapokaribishwa. Kulingana na andiko la siku ya leo, hata ikiwa ardhi ni sawa,
inaweza kupatikana magugu pia. Magugu ni mfano wa ishara za mauti ambazo
tunaweza kukuta mahali ambapo ishara za maisha zipo. Hali hii inamaanisha
kwamba hata ikiwa moyo fulani ni mwema unaweza kubeba mbegu ya uovu, yaani
unaweza kuwa na mwelekeo mbaya. Adui ya Mungu atatenda daima kuwazuia watoto
wake waishi kulingana na mapenzi yake.
Andiko la Hekima ni wimbo unaoongelea wema na
uvumilivu wa Mungu kwa watoto wake wote. Enzi na nguvu yake haimzuii kutenda
kwa upole na upendo, akiwatunza wote, hasa wale wasio na nguvu. Akitenda hivyo,
aliwaelimisha watu wake akiwapa nafasi ya toba na mabadiliko ya maisha ili yawe
kulingana na matarajio yake. Mungu ndiye mwenye huruma na mvumilivu kwa sababu
anapenda kwa upendo wa milele, yaani
upendo unaotoa tumaini zuri kwa kufungua milango ambayo tumefunga kwa sababu ya
makosa yetu. Tunahitaji upendo huu na tunataka sana kupenda kama Mungu alivyo.
Hilo ndilo tendo la Roho wake anayekaa ndani yetu ili tujifunze kuomba kwa
imani ya watoto, kwa kutamani moyoni mwetu Mungu anayetamani ndani yetu.
Mfano ambao Yesu anatujulisha unaongelea
mwendo wa Ufalme ulio kama mtu mmoja aliyepanda mbegu njema katika konde lake,
lakini wakati wa usiku adui yake alikuja na kupanda pia magugu kati ya ngano.
Tunataka kutafakari kidogo juu ya tabia mbili, yaani: tabia ya kosa la
uvumilivu kwa upande wa watumishi na uvumilivu wa mwenye konde (mbele ya tendo
la adui na ya kutokomaa kwa watumishi). Nia ya Yesu ni kuongelea Mungu kama
Yule anayepanda mbegu njema katika konde kubwa la ulimwengu wala hawezi kufanya
tofauti maana yeye ndiye mwema. Adui yake alipanda magugu, yaani mbegu mbaya.
Je, inawezekana kufanya nini kwa magugu haya? Mwenye konde ana mpango mmoja,
lakini anapendelea kusubiri na kutenda katika wakati mwafaka, yaani katika
wakati wake mwenyewe. Adui aliyepanda magugu alitenda katika usiku, yaani
amefichwa. Matendo dhidi ya mapenzi ya Mungu yaonyesha hali za giza maishani
mwetu.
Ni wazi katika andiko hili kwamba uovu hautoki
kwa Mungu; yeye hataki uovu. Yeye mwenyewe anawaimarisha wanafunzi wa Mwanawe
waangalie njia yake ya kutenda kwa kuondoa uovu wa ulimwengu na wa maisha yao.
Kwa bahati mbaya, binadamu anabeba pia uovu ndani yake pamoja na wema unaotoka
kwa Mungu. Haikuwa hivyo tangu mwanzo. Mungu alifanya binadamu kama mtu mwema
na mwenye uhuru ili aweze kuchagua, yaani “Mungu alimwambia binadamu, ikiwa
unachagua wema na uhai wewe utaishi milele; ikiwa unachagua uovu na mauti wewe
utakufa.” Wakati uhuru wa binadamu ‘haufanywi upya na injili’ unaweza kutenda
kama adui. Basi, kama matokeo ya uamuzi wa kibinadamu, wema na uovu umekua
pamoja ulimwenguni. Mara nyingi uovu unaonekana wenye nguvu kuliko wema kwa
sababu tunaulisha zaidi. Tena mara nyingi tumeshangaa tunapoona kwamba mtu
fulani anayeonekana mwema ndiye mbaya na yule anayeonekana mbaya ndiye mwema. Kwa
matarajio siyo mazuri na kwa haraka tuko na mazoea ya kuwahukumu wengine. Tendo
hili siyo kazi yetu.
Kulingana na mwendo wa mfano huu, ni lazima
kuwa na uvumilivu na utambuzi ili kuondoa uovu katika wakati mwafaka na kwa
matendo kamili ili yaweze kuimarisha wema pia na sio kupunguza nguvu zake.
Ndiyo katika hali hii ya wema na uovu ambayo thamani za Ufalme zilipandwa. Kama
Mungu ndiye wa kwanza kwa nia ya kuondoa uovu wa ulimwengu, yeye mwenyewe
anatualika kusubiri kwa uvumilivu kwa kujifunza kutoka kwake ambaye
anawanyeshea mvua watu wa haki na wasio na haki ama watu wema na wabaya. Kwa
uvumilivu wake Mungu ametupa nafasi nyingi za toba na mabadiliko ya maisha.
Basi, kuwa na uvumilivu sio kukubali uovu bali kuifuata njia ya Mungu ambaye
ana milele mbele yake na kujua jinsi ya kubadilisha uovu kuwa wema kwa sababu
anajua jinsi ya kupenda. Kweli huu ndio mwaliko tubadilishe mtazamo wetu kwa
kutenda kulingana na moyo wa huruma ya Mungu.
Fr Ndega
Mapitio ya Kiswahili: Christine Githui
Nenhum comentário:
Postar um comentário