Kutafakari kuhusu Mt 13,
44-52
Sura kumi na tatu
ya injili ya Mathayo inajulisha mifano mingi ya Yesu ili kuonyesha kwamba hali
ya Ufalme wa Mungu siyo mbali na hali zetu bali inatokea miongoni mwetu na
ndani yetu. Baada ya mtaguso wa Vaticano wa pili, baba mtakatifu Paulo wa VI
aliandika waraka mmoja unaoitwa Evangelii Nuntiandi akiwaimarisha Wakristo kwa
kazi ya kueneza injili kwa njia mpya. Kati ya mambo ya waraka, yeye alitaja
jambo la ufalme wa Mungu/mbinguni, akisema, “Ufalme ambao injili inatangaza
huchukuliwa na watu walio wa utamaduni halisi kwa njia ya ndani. Haiwezekani
kujenga ufalme huu kwa kuacha thamani za ustaarabu na tamaduni za kibinadamu” (EN 20). Kwa maneno mengine, hali
ya ufalme inachanganyika na hali yetu. Thamani za ufalme zinapaswa kuwa rejeo
la maisha yetu. Kwa hivyo Yesu anatujulisha siku ya leo mifano mitatu.
Katika mfano wa
kwanza ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichika na kukutwa shambani;
wa pili, unafanana na lulu nzuri kuliko nyingine zote; na tatu, na wavu
uliotupwa baharini, ukanasa samaki wa kila aina. Mifano miwili ya kwanza
inadhihirisha kwamba Ufalme wa mbinguni ni hali inayopatikana, lakini ni muhimu
pia kuitafuta hali hii. Kulingana na utabiri wa nabii Isaya, ndiye Mungu
mwenyewe anayepatikana na kwa hivyo tunaalikwa kumtafuta. Anasema Carlo Dellari
kwamba, “Sio sisi tuliomfikia Mungu ili kumjua bali ndiye yeye aliyetutangulia
katika mkutano na kutuimarisha kutembea ili kukutana naye. Mtakatifu Agustino
alikwisha sema uthibitisho huu wakati ulipomfanya Bwana kusema maneno haya,
yaani ‘wewe haungenitafuta ikiwa haungalikwisha nikuta mimi’”.
Basi ufalme sio muundo wa nguvu kama falme za
nchi bali ni tendo la Mungu mwenyewe ambaye anapatikana kwa wote. Lakini sio
wote ambao wanapatikana kukutana nawe. Ufalme huu una thamani sana na
husababisha furaha kubwa katika maisha ya mtu ambaye aliugundua ama aliukuta.
lakini kwa ajili ya furaha hii mwanafunzi anaalikwa kujinyima kila kitu, yaani
kuacha mahali, mali na “usalama” wa uwongo kwa sababu “bila juhudi za kutafuta
na kujinyima, furaha ya mkutano haiwezekani." Uzoefu wa kugundua ufalme
kama hazina ni uzoefu wa kukuta maana ya kweli ya maisha. Hali nyingine haina
maana tena. Furaha tunayoiona ndiyo matokeo ya chaguo letu.
Katika mfano wa
tatu Yesu alifananisha ufalme na wavu uliotupwa baharini ambao unanasa samaki
ya kila aina. Mfano huu unadhihirisha kwamba Mungu ana mpango wa wokovu kwa
wote kwa sababu anataka kuwakaribisha wote katika ufalme wake. Lakini ni lazima
hukumu iwe kwa sababu makaribisho ya pendekezo lake si sawa kwa wote. Kulingana
na maana ya mfano huu, katika mwisho wa nyakati wabaya hawatakuwa na nafasi
sawa na wema. Kila mmoja atakuwa na nafasi ambayo alichagua kulingana na maisha
aliyoishi. Lakini hakuna sababu ya kukata tamaa kwa maana Mungu anataka
kuwaokoa wote na kutuimarisha kutafuta kwanza ufalme wake kama chaguo
kamili.
Basi, Huu ndio
mwendo wa kumfuata Yesu. Yeye ndiye hazina yetu ya kweli. Anatuvutia kwake kwa
sababu ya wema, ukweli, uvumilivu na unyenyekevu wake. Yule ambaye
anakutana na Kristo habaki alivyo kwa
sababu alikuta lile ambalo linatoa maana kwa kila kitu. Kweli mkutano unaweza
kubadilisha maisha yetu kabisa kwa sababu unaleta njia tofauti ya kuona na
kutenda. Furaha ndio matokeo ya mkutano naye na kumchagua kama rejeo la pekee
la maisha yetu. Yesu alitushirikisha Ufalme wake nasi tunaalikwa kujikabidhi
mikononi mwake kwa ajili ya kuchagua vizuri katika kila kitu. Yule ambaye
alimchagua Kristo yeye alichagua ufalme ulio hali ya ahadi ya kindugu, ya amani
na ya upatanisho. Ndicho kipimo cha furaha kubwa na kamili.
Fr Ndega
Mapitio ya Kiswahili: Christine Githui
Nenhum comentário:
Postar um comentário