Kutafakari
kuhusu Mwanzo 2, 7-9; 3,1-7; Waroma 5, 12-19; Mathayo 4, 1-11
Binadamu
alifanyika kwa mavumbi ya ardhi ili kupokea uhai wa Mungu ndani yake. Pamoja na
mahali pazuri pa kuishi, binadamu alipewa pia zawadi zote alizohitaji aishe kwa
ushirika na Mungu na kwa maelewano na ardhi iliyo sehemu ya maisha yake. Lakini
majaribio ya kutumia zawadi zake kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe yalimwongoza
binadamu kuacha ushirika na Mungu na kupanga maisha yake tofauti kabisa na
mpango wa Mungu kwake. Binadamu wa kwanza alipendelea kumtii “nyoka”, aliye
mfano wa “yule mwovu,” kuliko kumtii Mungu. Hali hii ilisababisha mauti kwa
watu wote. Ndiye Yesu “Adamu wa kweli” aliyegundua tena mpango Mungu na
kushinda uovu akimtii Baba yake. Chagua yake ilifanya tofauti kwa sababu ikawaletea
wote uzima.
Mambo yote
ambayo Yesu aliweza kufanya alipata mafanikio kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Ndiye huyo Roho ambaye alimwongoza nyikani na huko pia alijaribiwa na shetani. Kweli
Yesu alionyesha ahadi na hali yetu ya kibinadamu. Mfano, yeye alienda jangwani
baada ya ubatizo. Ingawa hakuhitaji kubatizwa alikubali uzoefu huu kwa ajili ya
mshikamano nasi tulio wenye dhambi na ya kuiheshimu kazi ya Yohane. Vivyo
hivyo, alikubali kushawishiwa jangwani. Anataka kutuonyesha kwamba “baada ya
ubatizo majaribio mengi yanatujia.” Kwa upande wake, ingawa alijaribiwa
jangwani, “alichagua kubaki mwaminifu kwa Mungu.” Yesu alijua wazi sana kwamba yeye
ni Mwana wa Mungu na kwamba alikuja kwa ajili ya kufanya mapenzi ya Baba yake. Kwa
kifupi, ndiye Roho Mtakatifu aliyemsaidia Yesu kuwa mwaminifu kwa mpango wa
Mungu.
Katika
uzoefu wake wa jangwa, Yesu alifunga kwa siku arobaini na akaona njaa. Arobaini[1] ni
namba ya mfano iliyomaanisha “muda mrefu.” Kabla ya Yesu tuko na baadhi ya
mifano ya Viongozi wa kibiblia ambao, kabla ya kuchukua kazi ama kabla ya tukio
muhimu, waliruhusu kuongozwa jangwani na kubaki bila kula chakula wakati wa muda
mrefu ili waweze kuandaliwa vizuri kwa ajili ya kazi aliyowakabidhi Mungu.
Tukumbuke ule muda wa siku arobaini ambao Musa alibaki milimani Sinai ili
azipokee Amri Kumi; na pia siku arobaini wa Eliya akitembea mpaka milima Horeb
ili akutane na Mungu na kuyapokea maelekezo ya kazi yake kama nabii. Namba
arobaini inatumika pia kuongea kuhusu kiasi ya miaka ambayo Waisraeli walibaki
jangwani kabla ya kuingia katika nchi ya ahadi. Kwa watu hawa wakati huu
ulikuwa wa utakaso na kukomaa. Lakini hawakuwa na uaminifu kama Yesu alivyo.
Uzoefu
jangwani ni maalum kwa ajili ya upweke, utakaso na kukomaa. Lakini jangwa ni
pia maisha yetu ya kawaida ambapo tumeongozwa na Roho Mtakatifu, lakini
tunajaribiwa kukata tamaa kwa sababu ya majaribio ya yule mwovu, kama
ilivyotokea na Yesu. Mshawishi alianza kutoka mambo madogo akichukua nafasi ya
kosa la nguvu mwilini mwa Yesu kwa sababu ya kufunga. Matarajio yote yalikuwa
dhidi ya namna ya kuwa masiha ambayo Yesu alichagua. Yesu alimshawishiwa
kutumia uwezo wake kwa manufaa binafsi badala ya upendo, huruma na utumishi kwa
wengine. Tena Yesu alishawishiwa kusifiwa badala ya kutangaza Mungu na Ufalme
wake. Majaribu matatu ya Yesu yanamaanisha majaribio yote ambayo yalikuwapo
maishani mwake nyakati zote za kazi yake. Hata hivyo, alipata kushinda yote kwa
sababu akaongozwa na Roho Mtakatifu na kuwa mtiifu kwa Baba yake.
Majaribu ya
mali, nguvu na utukufu Yesu aliyokabiliana nayo hayakumzuia ya kufanya mapenzi
ya Mungu. Kama ilivyotokea na Yesu, na Adam na Waisraeli, sisi pia tunashawishiwa
kuishi bila kumwamini Mungu. Mitego ya mshawishi inatuongoza kupendelea kutumia
mamlaka kuliko utumishi, kuamuru kuliko kutii, kudanganya kuliko kusaidia, kulazimisha
kuliko kupendekeza, kutafuta upendeleo kuliko kupenda, kuwa wanafiki kuliko
kuwa binadamu wa kweli. Kama Yesu amekwisha kumshinda adui ya Mungu, ndiyo chagua
yake msukumo ili chagua zetu ziweze kufanya tofauti. Kulingana na Mt. Agustino
“Ikiwa katika Kristo tumeshawishiwa, katika yeye tutamshinda shetani. Kristo
angeweza kumtupa mshawishi mbali sana naye; lakini ikiwa yeye hakuwa
ameshawishiwa hangetufundisha jinsi ya kushinda juu ya majaribu.” Kweli yeyote
ambaye anaufuata mfano wake wa kumtii Baba na kufunguliwa kwa msaada wa Roho
Mtakatifu anapata kufanya mapenzi ya Mungu na kushinda majaribio yote.
Fr Ndega
[1] Katika Jumuiya za
Kikristo umeanzika wakati wa toba unaoitwa Kwaresima. Kwaresima ni siku
arobaini za maandalizi kwa adhimisho la fumbo la Pasaka ya Kristo. Kutokana na
uzoefu wa Kristo jangwani, wakati wa kwaresima unalenga kuwa ni uzoefu wa
jangwa na kuwaalika waamini kuweka juhudi zaidi maishani mwao hasa kuhusu sala,
upendo na kutubu.
Nenhum comentário:
Postar um comentário