Kutafakari kuhusu Am 8, 4-7;
1Tm 2, 1-8; Lk 16, 1-13
Mungu anatarajia kwa watu wake maisha marefu
na ya heshima. Mambo yote ambayo hayaisaidii hali hii yanakataliwa na Mungu.
Hivyo, kupitia nabii Amos, katika somo la kwanza, yeye (Mungu) anashutumu aina
yote ya ukandamizaji ambao uliwazuia watu waishi kama watu wa Mungu hasa hali
ya udhalimu dhidi ya maskini na wenye njaa. Mateso yao
yadhihirisha kwamba tuko na jamii ya kijeuri ambapo wako baadhi ya watu wenye
nguvu ambao wanamiliki mali na pesa nyingi wakati wengine wengi hawana kilicho
cha kutosha kwa kuishi.
Kama dhambi ya kijamii ni matokeo ya kiasi cha
dhambi za kibinafsi, hivyo, hata sisi tuko na jukumu katika hali hii ya
udhalimu. Kuhusu hayo Baba Mtakatifu Francisco asema: “Ulaji
umetuongoza kutumia vitu chepesi pamoja na ubadhirifu wa chakula cha kila
siku... Tunapaswa kukumbuka kwamba chakula ambacho sisi hutupa takatakani ni
kama ikiwa tulikuwa tumeiba kutoka meza ya walio maskini na wenye njaa.” Hali
ya watu hawa ilikuwa kipaumbele katika kazi ya Yesu ambaye alichukua ahadi ya
kuwa maskini ili kuwatajirisha wote kwa umaskini wake.
Katika somo la pili, Mt. Paulo anatushauri
kuwaombea watu wote hasa wale ambao wako na mamlaka ya kuongoza na kutawala,
yaani Viongozi wa Kanisa, Serikali na kadhalika. Hao wanapaswa kufanya kazi yao
vizuri ili tuweze kuishi maisha ya utulivu na amani. Sisi ni wa Mungu na kwa
hivyo, kazi ya viongozi wote kwa ajili ya maisha yetu ni ushiriki katika
utawala wa Mungu mwenyewe ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua
yaliyo kweli ama Aliye ukweli. Ni jukumu
letu ili watawale vizuri nalo linampendeza Mungu.
Tukiendelea kutafakari kwetu, tuko na mfano
ambao Yesu alisimulia kuongea kuhusu mahitaji ya kuwa mwaminifu kuhusu jukumu
ambalo tumepokea kutoka kwa Mungu. Kile kilicho nacho kinatoka kwa Mungu kwa
sababu vyote vizuri vyatoka kwake. Anatukabidhi utunzaji wa vyote na kutarajia
tupate kusimamia zawadi zake kulingana na mapenzi yake. Sisi sio walio na mali
bali ndio wasimamizi tu wa zawadi za Mungu. Hivyo, tunapaswa kuitumia pesa sio
kama lengo la maisha, bali kama chombo cha kuizaa hali nzuri kwa wote.
Tunaishi katika jamii ambapo pesa ni kipimo cha
kila kitu na pia inaonekana kwamba pesa inatutawala. Kila kitu ambacho
tunahitaji hakiwezekani kupata bila pesa. Hii ni nguvu na maana ya kuishi kwa
watu wengi. Je, Wakristo wanapaswa kuwa na tabia gani mbele ya utajiri? Wale
wanaofuata Kristo wanapaswa kuwa waaminifu katika mambo yote na kutumia tabia
kamili kuihusu pesa. Kutokuwa na tabia kamili kuhusu jambo hili kunatuongoza kusahau
haja ya uangalifu kwa ajili ya familia, utunzaji kwa afya yenyewe, uhusiano wa
kweli na Mungu n.k.
Mara nyingi uhusiano wetu na Mungu unasumbuliwa
kwa sababu ya hamu ya kuwa na pesa na mali nyingi. Yesu hasemi kwamba pesa si
muhimu, lakini asema kwamba haiwezi kutushika na kutumiliki. Yesu anataka tufahamu
kwamba pesa haijengi thamani za kweli ambazo zinazaa uzima na furaha. Tunaweza
kuitumia pesa ili kumtumikia Mungu, bali hatuwezi kumtumia Mungu ili tupate
pesa. Tunapaswa kuwa macho kwa sababu hali hii inaweza kutokea na mara nyingi bila
tutambue hiyo. Pesa ni kitu ambacho kinaweza kututumia na kutubadilisha kuwa
wasio na hisia kwa ajili ya Mungu na kwa mahitaji ya wengine.
Pesa inatusaidia kuishi lakini imewaweka watu
mbali sana wao kwa wao. Pesa inaijenga nyumba lakini inaweza kuharibu familia. Kupitia
pesa tunaweza kuinunua nguo, chakula na kadhalika, lakini pia inaweza kuzaa
upendeleo, ubaguzi na utoaji rushwa. Hatuwezi kuruhusu kwamba pesa iwe chombo
cha tofauti kati yetu kwa kutuongoza kuwabagua wengine. Kati yetu tunajua jinsi
vile pesa imekuwa muhimu, hasa kuhusu sadaka ya ukarimu kwa ajili ya kulijenga
kanisa-hekalu na kwa ajili ya mahitaji mengi katika kazi zetu za kuinjilisha.
Tunamshukuru Mungu kwa matumizi ya pesa kama maonyesho ya ukarimu kwa manufaa
ya jumuiya zetu kwa kulijenga Kanisa la Bwana. Tena tumwombe neema ya kuwa na
tabia kamili mbele ya pesa kwa kutumia ishara hii si kama chombo cha ubaguzi,
bali kama chombo cha undugu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário