Kutafakari kuhusu Lk 14: 25-33
Umati wa watu waliandamana na Yesu, lakini sio
wote waliokubaliana naye. Alipoitambua hali ya kutokuwa na ahadi na makubaliano,
aligeuka na kuwalekeza baadhi ya maneno. Maneno yake yalikuwa nafasi ya
kutafakari kwa kweli maana ya safari yao. Ingawa Yesu alikuwa maarufu, kwa
sababu ya mambo mema aliyofanya kwa ajili ya watu, utume ambao Yesu alichagua
kutimiza mapenzi ya Mungu hauleti umaarufu. Watu walichanganyikiwa kuhusu Yesu
kwa sababu hawakumjua bado na kumfuata kwa njia yoyote.
Kama Yesu hakuwa na nia ya kumdanganya yeyote,
aliongea nao kwa uwazi sana kuhusu maana ya kumfuata na matokeo ya uamuzi huu. Njia
hii ya kusema ilikuwa tabia yake ya kawaida kama alivyofanya kwa ajili ya wale
kumi na wawili, yaani aliwajulisha masharti ili wawe wanafunzi wake wa kweli.
Kutoka kwao, Yesu hakutarajia werevu ama upumbavu, bali kupatikana na hatia. Hawawezi
kumfuata Yesu kwa sababu walipokea habari tu ya kuwa ni vizuri kufanya hivyo.
Yesu anatarajia zaidi, yaani mabadiliko ya ndani.
Andiko hili ni mwaliko wa kuchukua ahadi ya
kumfuata Kristo kwa kupanga mambo ya kesho, yaani kuwa na uwezo wa kuona mbele
ili kuepuka kufaragua. Ni vizuri kuota ndoto lakini ndoto hii inapaswa kuihusu
hali halisi mtu anayoishi, vinginevyo itakuwa udanganyifu tu. Yesu anataka
kuepuka kwamba safari ya wafuasi wake iwe pasipo maana ama ya udanganyifu. Ni
lazima utambuzi, hekima, kupanga na uamuzi.
Mungu mwenyewe anatupa mfano wa kuwa na mipango
ya muda mrefu ili tupate mafanikio katika safari yetu kama wafuasi wa Yesu.
Yeye Mungu alipanga kumtuma mkombozi, kulingana na yaliyoandikwa: “... wakati
maalum ulipotimia, Mungu alimtuma Mwanawe aliyezaliwa na mwanamke... ili apate
kuwakomboa waliokuwa chini ya sheria.” (Wagalatia 4: 4-5). “Hata baadhi ya
wakulima hutegemea mvua inyeshe hata kama hawajaandaa shamba mahali pa kupanda
mbegu kama za mahindi au maharagwe.” Kupanga mambo ya kesho ni muhimu.
Yesu alisema, “Basi, kadhalika kila mmoja wenu
asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” Kama ilivyotekea
katika vifungu vingine, Yesu aliwapendekezea watu mpango wa maisha unaojumuisha
kujinyima, kwa sababu yeyote anayekutana na Yesu kwa kweli amekwisha pata
hazina ya kweli kwa maisha yake wala hawezi kubaki alivyo, yaani mambo mengine
hayana maana tena kama kwanza. Kwa maneno mengine, Yesu anataka kuwa kipaumbele
maishani mwa wanaoamua kumfuata. Hakuna jambo lingine ambalo liweze kuitoa
maana ya kweli kwa maisha yao ila Yesu peke yake.
Wanafunzi wa Yesu wa kweli walimtegemea Mungu
katika mambo yote kama Yesu alivyo. Yeye alishiriki na wanafunzi wake ufalme wa
mbinguni na kuwajulisha njia ya msalaba ili waweze kufanya mapenzi ya Baba yake.
Kupitia njia hii, tunatambua kwamba Kumfuata Yesu hakuuleti upendeleo au hadhi,
bali mateso na kujisalimisha kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Basi, yeyote anayetaka
kuishi bila ahadi hawezi kumfuata Yesu. Tena yeyote ambaye anatamani kumfuata
Kristo bila msalaba hatapata kumfuata kwa kweli kamwe.
Kupitia njia ya unyenyekevu na utupu Yesu
alipata utukufu. Utambulisho wa wanafunzi wa mwalimu Yesu unapaswa kufuata njia
sawasawa naye. Kwa upande wa Kristo msalaba ulikuwa sehemu muhimu katika mwendo
wa kufanya mapenzi ya Mungu na kudhihirisha kwa mpango wa upendo wake. Kwa
upande wetu kama wanafunzi, kuchukua msalaba ni ishara ya utayari wetu kwa mapenzi
ya Mungu kwa kujitolea kama Kristo. Kwa kufikia lengo hili tunapaswa kujikana
nafsi yetu, yaani kujisahau sisi wenyewe ili wengine waweze kukumbukwe.
Tunapaswa kujikana sisi wenyewe ili Mungu aweze kujifunua kwa nguvu yote ya
upendo wake. Tunapaswa pia kujiondoka kutoka katikati/mahali muhimu ili wengine
waweze kuwa na nafasi ya kwanza. Kwa maneno mengine, tunapaswa kuwafikiria
wengine ni wamuhimu kuliko sisi wenyewe. Kama haiwezekani kumfuata Kristo bila
msalaba, mfano wake wa uaminifu kwa mpango wa Mungu utuimarishe katika safari
yetu ya yetu ya kujitolea kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário