Kutafakari kuhusu Lk 15, 1-32
Sura ya kumi na tano ya toleo la Luka inajulikana sana miongoni mwa mifano
ya Yesu. Hii inaitwa sura ya Mifano ya huruma. Tuko na mifano mitatu, yaani
mfano wa Kondoo aliyepotea (4-7), wa Sarafu iliyopotea (8-10) na Mwana mpotevu (11-32).
Mifano hii inaonyesha tabia ya huruma ya Mungu kwa wenye dhambi na furaha ya kupata
tena kitu kilichopotea. Kwa kufahamu nia ya Yesu alipoisimulia mifano hii
tunahitaji kutafakari kwanza kuhusu mazingira ambayo Yesu aliishi.
Katika muktadha ule, baadhi ya
watu walijiona waliostahili wokovu wa Mungu kuliko wengine kwa sababu ya
uaminifu wao kwa Sheria. Walichukua mamlaka ya kuwatenganisha watu, wakiwapanga
kama wema au wabaya. Mamlaka haya hayatoki kwa Mungu kwa sababu kipimo ni
ubaguzi. Walisahau kwamba mbele ya Mungu hakuna yeyote aliye na haki kuliko
mwingine. katika njia yake ya kupenda Mungu hakuna ubaguzi. Kwa upande wake watoza
ushuru na wenye dhambi ni watoto wake kama vile ndio Mafarisayo na Waandishi. Kipimo
cha kuishi kwa ushirika na Mungu sio sheria bali uzoefu wa undugu.
Ingawa
yako matukio mengi katika Agano la Kale, ambayo yanaonyesha njia maalum ya
Mungu ya kutenda, ni “katika Yesu Kristo kwamba huruma ya Mungu imepata kuwa
hai na yenye kuonekana, na hata ilifikia kilele chake katika Yeye... Yesu ni
uso wa huruma ya Baba. Kila kitu ndani
yake kinaongelea huruma. Hakuna chochote kwake kinachopungukiwa na huruma (Baba
Mt Francisco).” Kama
alama ya huruma ya Mungu, Yesu ana chaguo wazi sana, kulingana na maneno ya
waliompinga yeye, yaani “Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao”.
Kweli, Yesu alikuwa na njia
maalum ya kuongelea huruma ya Mungu, yaani katika Yesu jambo la huruma lilionyeshwa
“kwa neno lake, matendo yake na kwa
nafsi yake yote.” Yeye alitumia ishara nyingi za makaribisho,
akithibitisha lengo la ujumbe wake na ukweli wa mafundisho yake. Kwa kweli,
watozaushuru wengi, makahaba na wengine waliokataliwa na jamii, walijiona kukaribishwa
na Yesu na tena kubadilishwa kwa sababu ya mkutano na huruma ya Mungu.
Mfano wa mchungaji anayepoteza
kondoo wake tuko na ishara ya Mungu Baba ambaye ana macho maalum kwa kila mtu
naye hapumziki mpaka kukutana na aliyepotea na kumhusisha tena katika ushirika
wake. Katika mfano wa sarafu iliyopotea Mungu ni kama mama mmoja anayetumia juhudi
na nguvu zote ili kukuta kitu alichopoteza naye anapopata hiki anafanya
sikukuu. Katika mfano wa mwana mpotevu, macho yetu yamlenga baba aliye mhusika
mkuu wakati wote. Uhusiano wake wa mapendo kwa vijana wake ndio umuhimu wa
tukio hili. Kulingana na Yesu, Mungu ni kama baba mmoja aliye na watoto wawili na
kushiriki nao zawadi zake kwa njia sawa. Yeye anawapenda wote na kutaka wajione
katika uzoefu wa familia kwa kushiriki katika
furaha yake ya baba. Utunzaji na ulinzi wake ni maana nzuri ili wabaki pamoja naye
daima.
Yule ndogo alichukua nafasi ya
kuenda zake akiacha ushirika wa baba yake. Yeye alifanya hivyo sio kwa sababu hajihisi
kupendwa bali kwa sababu alihisi mwenye uhuru. Ndio hivyo uzoefu ya upendo wa
Mungu Baba, yaani unaheshimu kila mtu na kumruhusu kuchagua kwa uhuru kabisa
njia yenyewe ya maisha yake. Tunapotenda dhidi ya Mungu kupitia dhambi, Yeye anajihisi
ameachwa na kusalitiwa, lakini hashindwi kutupenda. Yeye anashughulika sana kwa
ajili ya maisha yetu kwa kutupa ulinzi na utunzaji wake. Kwa hivyo kwa
kufikiria upendo wake kwetu tunahisi majuto na hamu ya kurudi tena kwake. Ingawa
tunashindwa kuishi kama wana, Mungu hashindi kuishi na kutenda kama Baba mwema
kamwe.
Katika mfano huu yuko pia mwana
mkubwa ambaye hajihisi mwana wala ndugu. Kosa la utoto ni kwa sababu anajiona kuwa
ni mfanyakazi; kosa la undugu ni kwa sababu anamkataa ndugu yake mdogo. Tabia
ya huyo mwana mkubwa inaizuia furaha kamili ya baba na ukamilifu wa sikukuu. Kumrudia
Mungu ni maana ya furaha kubwa kwake. Lakini furaha yake itakuwa kubwa zaidi ikiwa
wale ambao wanajiona watoto wake waweze kushiriki katika hisia zake kuwahusu
wengine. Hataki kwamba tuwe na wivu kuhusu njia yake ya kupenda bali tutende
kama yeye alivyo. Kwa hivyo Yesu alisema, “Muwe na huruma kama Baba yenu
alivyo.” Upatanisho na wengine ni kipimo ili uhusiano wetu na Mungu uwe kweli. Hii
ni njia ya kweli ya toba iliyo mwendo wa muda
mrefu na huanza mioyoni mwetu. Turuhusu kuguswa na huruma ya
Mungu ili tuweze kuwa vyombo vya huruma hii kwa wale wanaohitaji msamaha wetu.
Nenhum comentário:
Postar um comentário