Tafakari kutoka Ezekieli
14: 11-12.15-17; 1Kor
15: 20-26.28; Mt
25: 31-46
Maandiko haya yasema kwamba Mungu ni
kama Mfalme Mchungaji ambaye anawajali
wana kondoo wake na kuwa na upendo maalum hasa kwa ajili ya wasio na nguvu.
Tabia yake ni kipimo cha matendo yetu. Upendo na huruma kwa wenzetu walio na shida ya
kimwili ndio kipimo ili tuweze kuingia katika ufalme wake.
Tutafakari kuhusu fumbo la Ufalme huu na kukaribisha
mifano ya huruma ya Kristo kama msukumo ili tufanye vivyo hivyo.
Kwa jina la
Mungu, Nabii Ezekieli anawashutumu viongozi wa Watu wa Israeli kwa sababu
tabia yao ya kutowajibika ilisababisha
uhamisho wa Babeli, yaani, kipindi cha
huzuni na mateso kwa
watu hawa. Lakini katika ujumbe wake, nabii anatangaza
pia utunzaji wa Mungu kwa ajili ya
watu hawa. Yeye atawaongoza kwenye hali
mpya kama vile mchungaji kwa ajili wa wana kondoo wake. Unabii huu unapata
mafanikio yake kwa ukombozi toka
uhamisho. Unabii huu ndio pia tangazo la kazi ya Yesu Kristo kama Mchungaji Mwema aliyesalimisha ili wanadamu wote wapate maisha mengi.
Kulingana na Mtakatifu Paulo,
Yesu alishinda nguvu zote duniani, kupitia kifo chake na ufufuo wake,
akiwaokoa wanadamu wote na kuanzisha
Ufalme wa Mungu Baba yake. Wanadamu
wote wanaalikwa kuingia katika ufalme huu. Lakini ni lazima kuungana na Kristo na kutenda kulingana na mapendekezo yake ili Mungu awe yote
katika wote.
Andiko hili ya Injili linajulikana kama “Hukumu ya
mwisho” na wengi kati yetu wanapendelea kumfikiria Yesu kama “hakimu” atakayekaa kitini chake akiwahukumu wanadamu, kuwatuza wengi na kuwaadhibu wengine
kama wafalme wa ulimwengu walivyo. Lakini hatuwezi
kusahau yale aliyosema, yaani “Mungu hakumtuma Mwana
ulimwenguni ili kuwa hakimu wake,
lakini kwa kuwa mkombozi wake” (Yohane 3, 17).
Hivyo, lengo lake sio kuhukumu bali kuokoa kwa sababu ya upendo na
huruma yake. Basi, inawezekanaje kufahamu andiko hili la Mathayo linaloongea
kuhusu hukumu? Kwanza kabisa aina hii ya andiko ndiyo ya kifunuo ambayo inatumia
ishara nyingi ili kuongea kuhusu hali iliyokuwa ikitokea katika wakati ule.
Wainjilisti wanaonyesha kwamba Yesu alikataa cheo cha mfalme katika wakati wa utukufu, na
kukubali katika wakati
wa kushindwa, mfano msalaba. Upinzani
wake kwa cheo
hiki ulikuwa kwa sababu ya mawazo
ya kisiasa ya watu kuhusu suala hili. Yeye
anatumia mfano wa mfalme katika
andiko hili ili kuelea maana kamili
ya Ufalme na lengo lake kama
Mfalme. Ufalme wake sio kutoka ulimwengu huu nao hauwezi kuonekana (kama ndipo huko au ndipo hapa). Yesu
hakufafanua Ufalme wa Mungu ni nini, lakini alisema kwamba ndio tayari kati yetu nasi tunaweza kuhisi tukio
lake kwa kupitia matendo mema kwa ajili ya wengine. Yesu
ndiye mfalme aliyekubali msalaba kama kiti chake cha enzi alipoonyesha ishara
kubwa ya upendo kwa ulimwengu. Hukumu imekwisha anza kwa sababu mfano wake wa
kupenda na kuwa na huruma ni kipimo cha kutenda.
Mfalme
huyo anataka kuwakusanya watu wote kuzunguka naye katika
ufalme wake kama mchungaji anavyofanya kwa kundi lake. Yeye anajitambulisha na ndugu
wadogo na kuyaanzisha matendo ya upendo na huruma kwa
ajili yao kama kipimo cha wokovu. Maneno yake yanatusaidia tufanye
utambuzi na chaguzi zetu zinatuhukumu. Aina ya mahusiano yetu na
wale walio na shida na wadogo inatuhukumu. Sehemu ya mwisho ya hukumu itakuja
kwa wote nayo inapaswa kuwa ukamilifu wa maisha yetu kwa sababu mambo yote
ambayo tumeishi ndiyo maandalizi kwa wakati huu. Tutakapokutana na Mungu,
hatutaulizwa ikiwa tumeshiriki katika dini fulani wala mara ngapi tulienda
kanisani, bali kiasi gani tuliweza kupenda. Kwa hivyo tuko na ishara za Kristo
kwa ajili ya wadogo kama mfano. Mambo yote ambayo tunaweza kufanya kwa ajili
yao ndiyo kwa Kristo tunayofanya. Hatuhitaji kuacha ubinadamu wetu ili kukutana
na Mungu. Yeye mwenyewe anajiruhusu kukuta katika ubinadamu wetu, hasa wakati
ubinadamu huu unateseka. Ndizo chaguo zetu zitakazoamua mwelekeo wa maisha yetu.
Tusisahau kwamba mapenzi ya Mungu ni kwamba maisha yetu yapate ukamilifu na kwa
hivyo anakaa ndani yetu kwa njia ya Roho wake. Tumpe nafasi ya kutenda kwa
sababu, “Ikiwa Mungu yumo ndani yetu, tutafanya yale mema hata kwa kupita kwetu
tu”.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário