Kutafakari kuhusu Mat 2, 14a.22-33;
1Pd 1, 17-21; Lk 24, 13-35
Yesu alishiriki uwezo wake na wanafunzi wake akiwawezesha
waendelee kazi yake. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu, hasa katika siku ya
Pentekoste, walitangaza kwa furaha uzoefu walioishi pamoja na mwalimu wao na
ushindi wake juu ya mauti kwa uwezo wa Mungu. Tangazo hili ni mwaliko wa
tumaini kwa sababu ushindi wa Yesu unatoa nafasi ya wokovu kwa wote. Kwa sababu
ya Kristo imani yetu na tumaini letu linamwelekea Mungu ndiye Baba na kutaka
tutende kulingana na mfano wa Mwanawe. Ingawa Yesu haonekani tena kwa macho,
yeye anaweza kutambuliwa kwa matendo yetu mema hasa tunaposikiliza neno na kusherehekea
Ekaristi.
Mazungumzo ambayo injili inatujulisha ni mamoja kati ya
mazungumzo ya ajabu na ya kamili ya Biblia. Hapo tuko na mwendo wetu wa upevu wa
imani na sehemu za sherehe ya Ekaristi takatifu, yaani hali ya jumuiya
inayokusanyika kwa jina la Bwana, uwepo wa Bwana Mfufuka anayetueleza Maandiko
Matakatifu na kuumega mkate kwa kutualika kuendelea kama yeye alivyo.
Tuko na wanafunzi wake wawili walikuwa wakielekea mji
uitwao Emau, Kilomita 11 kutoka Yerusalemu. Wanafunzi walihuzunika sana,
wamekata tamaa, wamekufa moyo na wakaiacha jumuiya na kurudi nyumbani, wakiwa
tayari kusahau kila kitu walichoshiriki pamoja na Yesu. Walitarajia Masihi
mtukufu na mfalme mwenye nguvu, lakini matokeo yalikuwa mbali sana na matarajio
yao: mtu mpendwa alishindwa na akafa msalabani. Hakukuwa chochote cha kufanya
isipokuwa kurudi kwa maisha waliyoyajua kabla ya kukutana na Yesu.
Ghafla alitokea mtu mgeni, ambaye alitembea pamoja nao na
kuongea nao kuhusu matokeo ya hivi punde, yaani Yesu aliye nabii mwenye nguvu
katika kazi na maneno mbele ya Mungu na watu, lakini alikuwa na mwisho
usiotarajiwa. Huyo Mtu Hija aliyatafsiri Maandiko ambayo yanazungumza kuhusu
Masihi. Walimsikiliza kwa uangalifu na mioyo yao ilianza kuchoma. Hatimaye,
wanafunzi walifika nyumbani na kumwalika: “Kaa pamoja nasi, Bwana”!
Baada ya kulikaribisha Neno la Mtu hija, walimkaribisha
nyumbani kwao. Yule mgeni alikubali kuingia sio kwa kukaa pamoja nao usiku
mmoja tu, bali kubaki nao daima. Wakati wao walikuwako mezani, mtu Hija
alifanya ishara inayojulikana, ishara ya karamu ya mwisho, wakati Yesu
alipoanzisha Ekaristi. Macho ya wanafunzi yalifunguliwa na kumtambua Bwana
Mfufuka. Hivyo Neno linaichoma mioyo; kuumega mkate hufanya kufungua macho.
Kristo alitoweka maana jumuiya imekwisha pata ishara halisi za uwepo wake,
yaani Neno lake na Mkate Uliomegeka. Asiyeonekana kwa macho, Bwana ndiye kuwepo
na kubaki daima. Sasa ni wakati wa kushuhudia.
Yesu yu hai na kuandamana na binadamu katika safari yetu,
ingawa hatambuliwi daima. Anajifanya kujulikana katika uzoefu wa kuumega mkate.
Kama wanafunzi wake tunahitaji kuwa pamoja naye, kujiruhusu kuandamana naye, kusikiliza
maneno yake na kumwalika kukaa nasi. Ni thamani yake kukaa nasi na kutuonyesha
njia ya kweli ya kuishi. “Ni maonyesho haya ambayo Wakristo wa kwanza walitumia
kuonyesha ushirika wao wa Ekaristi. Kwa kufanya hivyo walimaanisha kwamba wote
ambao wanakula mkate mmoja uliomegwa, yaani Kristo, wanaingia katika ushirika
pamoja naye na kufanya mwili mmoja naye” (CCC 1329).
Katika safari yetu ya imani hatuko peke yetu kamwe. Yesu
anatujia na kutembea pamoja nasi. Yeye anapatikana kwetu hasa wakati tunapokata
tamaa na kutaka kuacha ahadi yetu kabisa. Yeye anatusikiliza na kutuongoza kwa neno
lake ambalo linachoma mioyo yetu ili tuweze kumtambua katika Ekaristi na kuishi
hali hii katika uzoefu wetu wa kila siku. Ndio uzoefu huu unaotufanya kuwa
mashahidi wenye furaha na ujasiri wa uwepo wake hai na ufanisi kati yetu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário