kutafakari
juu ya Mt 21,1-11; Is 50,4-7; Waf 2,6-11; Mt 26,14-27,66
Tunaingia katika wiki muhimu sana kwa Jumuiya
za Kikristo. Hii ni wiki inayojumuisha matukio makuu ya imani yetu, kueleza kwa
ishara nyingi na kwa kina vipindi vya mwisho vya maisha ya Yesu kama binadamu
hapa duniani na kutualika kwa ukimya na kutafakari. Hii ni pia nafasi ya
kufanya upya ahadi yetu kama wafuasi wa Yesu na kuimarishwa na mifano yake ya
uaminifu na uamuzi.
Tunaalikwa kumfuata Yesu anayeingia kama mshindi
katika Yerusalemu ili kukamilisha kazi yake ya upendo. Kwa kweli, hakuja juu ya
farasi kwa kiburi na kwa jeshi yenye nguvu kama walivyofanya majenerali wakiingia
mijini, lakini amepanda punda, na kuja kwa wema na rehema kama imetokea wakati
wa maisha yake yote. Yesu anajua sana nini itatokea nawe, hata hivyo hakukata
tamaa. Kinyume, anaonyesha uhuru wa Mwana mpendwa aliyepelekwa kuokoa wanadamu.
Kama tunakumbuka kuingia kwake katika “Mji wa amani”, sisi pia tunakumbuka
mateso na kifo chake katika mji huu ulio na mazoea ya kutenda kwa ukatili dhidi
ya wajumbe wa Mungu. Hivyo kifo chake sio hatima, bali matokeo ya kazi ya kinabii
aliyeishi kwa uaminifu hadi upeo.
Kama tunavyojua, nabii Isaya anatoa nyimbo nne
kuongea juu ya utambulisho na kazi ya Watu la Mungu, ambao pia wanaitwa
“Mtumishi wa Mungu.” Nyimbo hizi ziliandikwa wakati wa utumwa wa Babeli nasi
tunaweza kuzipata katika sehemu ya pili ya Kitabu cha Isaya. Andiko tunalotumia
hapo unafahamika kama ‘wimbo wa tatu’ na kulingana na huu, mtumishi anaishi
wito wake kama zawadi inayotoka kwa Mungu kwa ajili ya kutoa maisha mapya kwa
ndugu zake. Kwa sababu ya uaminifu wake, aliaibishwa, alikataliwa na kuteseka
sana, lakini hakukata tamaa, kwa sababu aliona ukaribu na utunzaji wa Mungu. Mtumishi
huyo ni mfano ya Yesu ambaye kwa utambulisho wake na hali ya binadamu, alijinyenyekeza,
akaaibishwa, akateseka na kuuawa maana ya uaminifu wake kwa Mungu. Imani yake ya
kimwana katika Mungu ndiyo maana ya uaminifu wake. Kwa njia ya utupu aliupata
utukufu. Njia ya unyenyekevu, ya ishara ndogo na ya kuchagua kinachoonekana
bila maana kwa jamii ndizo ishara halisi zilizo tabia za wanaoendelea kazi
yake.
Kulingana na masimulizi haya ya Mathayo, Yesu
anafikiria kuwa kukamatwa kwake, mateso na kifo chake kitakuwa kashfa kwa
wanafunzi wake, maana bado walikuwa na mawazo ya Masihi mwenye nguvu na
umaarufu. Hata hivyo, anaongeza kusema - kama kawaida - kuhusu ufufuko wake na baadaye
atafanya upya ahadi nao kutoka mahali ambapo yote yalianza, yaani kutoka Galilaya.
Kwa Yesu hakuna maonyesho ya upendo kubwa kuliko kutoa maisha yake kwa ajili ya
marafiki zake, hata wakati wao wametoroka (isipokuwa wanawake na mwanafunzi mpendwa).
Katika kilio chake, yaani “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?”, yeye
alionyesha uchungu ambao alihisi kweli kama mwanadamu, yaani, uchungu wa
kuachwa, uchungu wa vitendo viovu, uchungu wa dhambi za binadamu, n.k. Ghafla, wakati
yote yalionekana yamefanyika bila mafanikio, tuko na tangazo kubwa la imani: “Kweli
mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
Yesu aliachwa na marafiki zake, lakini yeye
hakuwako peke yake msalabani wala wakati wa kazi yake. Maneno yake mwenyewe yanashuhudia
kuhusu hayo, yaani “Yule aliyenituma yuko pamoja nami, hakuniacha peke yangu,
kwa maana mimi nafanya yanayompenda yeye (Yoh 8.29).” Hivyo “kilio” ambacho
Mathayo anaweka mdomoni mwa Yesu kinapaswa kufahamika kwa uhusiano na
kujisalimisha kwake mikononi mwa Baba, kulingana na toleo la Luka, iliyo tabia
yake daima, yaani “Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu (Lk 23,46).”
Vinginevyo, tungekuwa kukana sio tu kazi yake kwa ushirika na Baba bali pia uaminifu
wa Baba huyo.
Fumbo la mateso na kifo cha Yesu halionyeshi
uchungu kama jambo la kwanza kwa kutafakari bali upendo wake mkubwa hadi upeo.
Kifo hakikuwa kulazimishwa kwa Yesu, bali yeye alikubali kwa hiari. Yesu alijua
kwamba alikuwa akifanya jambo sahihi na hivyo mateso yake ni mwanzo wa ushindi
wake juu ya mauti, akifufua matumaini yote ya maskini na ya wanadamu wakosefu.
Mateso ya Mwana wa Mungu yanatualika kutafakari
juu hali ngumu ya mateso ya binadamu. Kama Mungu alijibu kwa ufufuko mbele ya
kifo cha Mwanawe, tunaweza kuhitimisha kwamba Mungu hataki mateso wala mauti ya
watu. Yeye hawaachi wale wanaoteseka wala hanyamazi mbele ya mateso yao. Kristo
alichukua kwa nafsi yake uchungu wa watu wote wa nyakati zote. Yeye anaendelea
kuteseka wakati sisi tunahisi maumivu na majaribio katika safari yetu. Mfano
wake unatuimarisha tuwe na kuwepo ufanisi maishani mwa watu wanaoteseka zaidi
kuliko sisi. Misalaba ya mshikamano na huruma tunayoitwa kuchukua kila siku
kama yeye alivyo inafanya kujitolea kwetu kuwe ishara ya upendo pia kama
ushiriki katika mateso yake kwa ajili ya wokovu wa watu wote.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário