Kutafakari kutoka Hes 11:25-29; Mk
9:38-43, 45, 47-48
Mungu hawabagui watu kwa maana anapenda na katika upendo hakuna ubaguzi. Matarajio
yake ni watu wake wote wawe manabii, wakisikiliza neno lake na kuongea katika
jina lake. Kupitia Roho wake Mtakatifu, anatuimarisha tuwatendee wote mema
kulingana na mapenzi yake, akidhibitisha kwamba upendo wake hauna mpaka. Mbele
ya Mungu hakuna mtu wa heshima kuliko wengine. Yeye hakubali umaarufu au
ubaguzi, bali anatarajia ahadi kwa njia yake ya kufikiri na kutenda. Anatenda
hivyo kwa sababu ya upendo Wake mkubwa.
Mtakatifu Yakobo anakosoa kwa nguvu watu wanaokuwa tajiri kwa njia ya
udhalimu kwa kukanusha mishahara kwa wafanya kazi. Mungu anapinga hali ya
udhalimu na kosa la usawa kati ya watu. Yeye ndiye tayari kutenda kwa ajili ya
walio waathirika wa udhalimu na kumwomba kwa imani. Ukosoaji huu unatumika pia
kwa wote ambao wajikabidhi katika mali ambayo anayo kuliko riziki ya Mungu. Mtu
anapokufa hawawezi kuchukua mali chochote pamoja naye; kwa hivyo tabia ya
kuongeza mali kwa nafasi yake mwenyewe haina maana.
Wanafunzi wa kwanza walijaribu kumkataza mtu fulani ya kufanya mwujiza kwa
jina la Yesu kwa sababu hakuwa mmoja wao. Walifanya hivyo kwa mamlaka gani?
Yesu hakukubaliana na tabia hii na kuwaambia kwamba mtu anayetenda mema kwa
jina lake (Yesu) hawezi kumtendea vibaya. Kisha akiendelea kwa mafundisho yake,
alisema kwamba watu wanaosaidia wafuasi wake watapokea tuzo kwa sababu ya
utambulisho wake na wale waliotumiwa kwa jina lake. Yesu anawakumbusha pia
kwamba mambo yote wanayofanya wale wanaomfuata yapaswa kuwaimarisha watu kumwamini
Kristo. Ni lazima kuepuka Kashfa kwa sababu tabia hii inavuruga imani na kukana
utambulisho wa wanaomfuata Yesu.
Tumetafakari kuhusu ugumu wa wanafunzi wa Yesu kuelewa na kuyapokea
mafundisho yake. Kujaribu kumkataza mtu fulani ambaye alifanya mema kwa jina la
Yesu ni ishara ya ugumu ya kumfahamu Yesu na mapendekezo yake. Maana ya kuwa mfuasi
wa kweli wa Yesu siyo maneno tu, bali ni matendo mema hata kama yeyote
hahudhurii kikundi. Badala ya kuwakataa wengine ambao wanatenda mema kwa jina
la Yesu, wanafunzi wake wanapaswa kujikataa wenyewe. Kuwa mwanafunzi wa Yesu kunamaanisha
kuishi imani iliyoonyeshwa kwa matendo. Kwa Yesu wale wanaosikiliza Neno la
Mungu na kuweka vitendoni ndio mama na ndugu zake na wanafunzi wake. Hivyo yule
aliyetenda mema kwa jina la Yesu anaweza kufikiriwa kama mwanafunzi wake.
Mtazamo wa wanafunzi ndio tofauti na ule wa mwalimu wao kwa sababu lengo lao
sio kukaribisha bado bali ubaguzi.
Kitu muhimu katika dini au imani ni matendo na siyo maneno tu. Matendo
husema zaidi kuliko maneno. Wakristo wa kwanza ndio mfano halisi kwa sababu waliweza
kuwavutia wengine si kwa maneno, bali kwa njia yao ya maisha. Kuhusu hao watu
walisema: “Mwone kama wanavyopendana”! hali hii iliwezekana kwa sababu ya
upendo wao ulionyeshwa kupitia ridhaa wao kwa wao, kushiriki pamoja, uvumilivu
katika maombi pamoja na unyenyekevu wa moyo. Kuhusu hayo Sinodi ya Afrika
imesema: “Sharti muhimu la kuhubiri ni ushuhuda wa maisha”. Mwanafunzi wa kweli
wa Yesu hawezi kuwa na ubaguzi na kuamini kuwa watu wa kundi lake pekee ama
kanisa lake ndiyo wanafunzi pekee wa Yesu na kwamba ndio hao peke yao ambao wameokolewa.
Hatuwezi kufikiri kwamba Yesu ni mali yetu. Ikiwa tunahisi karibu na Yesu, hatuwezi kuishi mbali sana na ndugu zetu, kufungwa
kabisa kwa hali kandokando yetu na hata kufikiri kwamba tunakuwa na mamlaka ya
kuwazuia wengine watende kwa jina la Yesu. Tuko mbele ya kosa kubwa. Tuwe macho
kuhusu baadhi ya uzoefu ambao unatufungua kwa Mungu lakini unatufunga kwa
wengine. Ikiwa imani yetu haituongozi kukutana na wengine na kutambua mema
ambayo wanaweza kufanya imani yetu ni utenganisho. Basi, ili Mungu atufundishe
kutambua mwendelezo wa kazi zake mbele ya matendo mema ya Wakristo na
kusaidiana kwa wema wa wote.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário