Kutafakari kuhusu Isa 50:5-9; Yak 2,14-18 Mk 8:27-35
Mtumishi wa Bwana
anajiona kuimarishwa kwa sababu ya uhakika wa upendo na utunzaji wa Mungu daima
maishani mwake. Uhakika huu unamfanya imara mbele ya mateso mengi. Yule ambaye
anamtumainia Bwana habaki kuchanganyikiwa na mwenye udanganyifu kwa sababu “uaminifu
wa Bwana ndio nguvu yetu”. Mtakatifu Yakobo anawaomba Wakristo wawe walio halisi
katika njia ya kuamini. Imani inayoonyeshwa kwa maneno peke yake siyo kweli. “Maneno
yatoweka hata ikiwa yanaonekana yawe na imani. Matendo yanaiweka halisi kwa kuifanya
iwe iko na sasisha”. Basi, ndiyo matendo mema ambayo yadhihirisha ukweli wa
imani yetu. Madre Teresa wa Kaukuta alikuwa na haya ya kusema: “Kila tendo la
upendo linalofanyika kwa moyo linaweka halisi imani kwa kumkaribia Mungu”.
Yesu alikuwa
anatembea pamoja na wanafunzi wake. Walipofika karibu na Kaisaria Filipi aliwauliza
maswali kuhusu utambulisho wake kulingana na mtazamo wa watu. Majibu yalikuwa
ishara ya kwamba mawazo kuhusu Yesu hayakuwa wazi sana kwa upande wa watu.
Ingawa hayakuwa wazi kwa watu, ni lazima kuwa tofauti kwa mitume kumi na wawili,
kwa sababu kwa Yesu haikuwa muhimu sana yale ambayo watu walifikiri, bali imani
na kukiri kwa wafuasi wake. Petro alidhihirisha yale ambayo wanafunzi wengine
kumi na mmoja walijua pia: Yesu ni Masiya wa Mungu. Lakini hawakuweza kuitangaza
habari hii kwa sababu ya kosa la maana kamili. Yesu alitambua kwamba wafuasi
wake walihitaji kujua kwa kina maana ya utume wake kama Masiha na masharti kwa kumfuata
kwa kweli.
Mawazo ya wafuasi
wa Yesu kuhusu Masiya yalifuata matarajio ya Wayahudi wengine, yaani, Masiya wa
kisiasa atakayetumia nguvu zake za kimungu ili kuwakomboa Wayahudi toka ukoloni
wa Warumi. Bila shaka Yesu alikataa mawazo hayo kwa kuonyesha njia tofauti ya
kutimiza mpango wa Mungu, yaani kupitia mateso, kifo na kufufuka. Njia aliyochagua
Yesu ni ile ya mtumishi wa Bwana wa nabii Isaya. Utambulisho wa mtumishi huyo
ni kuwa makini kwa sauti ya Mungu ili aweze kufanya mapenzi yake kwa kutumikia
kabisa. Kwa kufanya mapenzi ya Mungu mtumishi huyo alipaswa kuteseka na kufa,
lakini alisimama upande wa Mungu ambaye alimsaidia akimfanya mshindi. Itikio la
Petro lilidhihirisha upinzani dhidi ya njia ya maisha Yesu aliyochagua ili atimize
mapenzi ya Mungu. Uamuzi wa Yesu ulikuwa katika ushirika na Baba yake na upinzani
dhidi ya njia hii ni upinzani dhidi ya mapenzi ya Mungu.
Wanafunzi wa
kwanza walihitaji mwendo wa muda mrefu ili kujifunza kumhusu Yesu na kuyafahamu
mapendekezo yake sawasawa. Yesu alimkemea Petro lakini alimwalika afuate
mtazamo wa Mungu ili awe mwanafunzi wa kweli. Kidogo kidogo wote walitambua
kwamba kwa kujitoa kama Yesu alivyo, walipaswa kuzifuata hatua tatu, yaani,
kujikana wenyewe, kuichukwa misalaba yao na kumfuata Yesu. Kwa maneno mengine,
walipaswa kuyabadilisha maisha yao kabisa. Wale ambao hukutana na Yesu
hawakubaki walivyo na hawawezi kumwomba Yesu atende kulingana na mapendekezo
yao. Mwendo wapaswa kuwa tofauti. Kwa kumfuata Yesu kweli tunapaswa kupatikana
kwa mambo yote kwa ajili ya ufalme wa Mungu kwa kuyaingiza mapendekezo ya Yesu.
Tunapaswa kufananisha maisha yetu kulingana na njia ya Yesu ya kuishi na kuchukua msalaba kama yeye alivyo.
Injili siku ya
leo inatusaidia kutafakari kuhusu njia ambayo tumechagua ili kumfuata Yesu. Je,
hii ni njia ya kweli? Tunatambua kwamba Kumfuata Yesu hakuuleti upendeleo au
hadhi, bali mateso na kujisalimisha kwa ajili ya injili. Basi, yeyote ambaye
anataka kuishi kwa shwari na bila ahadi hawezi kumfuata Yesu. Yeyote ambaye
anatamani kumfuata Kristo bila msalaba hatamfuata Kristo kwa kweli kamwe.
Kupitia mambo hayo tunaweza kujiuliza maswali: Je, Kristo gani tumemfuata? Mawazo
au kitu gani tunahitaji kujinyima bado ili tuweze kumfuata Yesu kikamilifu? Maisha
yetu ya kawaida ni ishara ya kwamba tumekuta hazina yetu ya kweli? Tuishi wito
wetu wa wanafunzi wa Yesu kwa shauku na furaha kwa sababu Mungu ndiye mwaminifu
na kuwa tayari daima kutusaidia hasa wakati tuko na ugumu wa kubeba msalaba wetu.
Tumwaminie yeye kwa sababu uaminifu wake ni nguvu yetu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário