Tafakari kuhusu Ez 2, 2-5;
2Kor 12.7-10; Mk 6, 1-6
Mungu anachukua nafasi daima ya kujifunua naye
hahitaji matukio ya ajabu kujionyesha kwa watu. Njia yake ya kutenda
inasababisha kushangaza kwetu daima, kwa kushinda matarajio yetu ya kibinadamu.
Mantiki na mawazo yake ni tofauti kabisa na yetu. Hii ni mantiki ya unabii
katika siku za nyuma na hata leo. Mungu anatumia kama wapatanishi watu wanyenyekevu
ambao tunawakutana kwa kila siku na hali ya kawaida ili kuwasiliana nasi. Kwa kuitambua
hali hii ni muhimu kujua zaidi ya hali iliyoonekana (binadamu anaangalia hali
inayoonekana, lakini Bwana huona ndani ya moyo); ni lazima kuwa na uwezo wa
kuona kwa moyo kabla ya kwa macho. Hivyo tu tunaweza kutambua yale ambayo Bwana
anafanya katika maisha yetu.
Watu wa Israeli walifukuzwa katika uhamishoni wa
Babeli naye Ezekieli ambaye alikuwa mmoja wa kuhani alienda pamoja nao. Wakati
ambapo uharibifu wa Yerusalemu uliyasababisha mashaka kuhusu uaminifu na ahadi ya
Mungu, Ezekieli aliitwa kuwa nabii wa Mungu aliye hai kati ya watu ambao
waliasi dhidi ya Bwana. Utume wa Nabii Ezekieli ulikuwa kuwasaidia watu kuelewa
kwamba uharibifu wa Yerusalemu ambao uliutabiriwa na kuutimiza ulikuwa matokeo
ya dhambi zao. Kwa sababu ya hayo nabii Ezekieli alipata upinzani mkubwa lakini
alisaidiwa na Roho wa Mungu ili kubaki mwaminifu katika kazi yake. Kwa sababu
ya uaminifu wa Mungu kwa ahadi zake, maudhui ya ujumbe wa kinabii pamoja na
tangazo la adhabu yatoa pia ahadi ya wokovu. Hivyo kazi ya nabii ndiyo kuwaimarisha
watu wawe na imani na tumaini.
Mtume Paulo alikuwa na nafasi ya kupokea ufunuo
kutoka kwa Mungu. Nafasi hii ilitokwa pamoja na upinzani ambao Mtume huyo
alikabiliana wakati wa utume wake. Alimwomba Mungu amweke huru toka mwiba huo,
na Mungu alimwambia: “Kwako neema yangu yatosha.” Kila mtu anayechaguliwa na
kutumwa kwa kazi fulani anapaswa ufahamu kwamba uvumilivu na uaminifu wake wategemea
siyo nguvu zake tu bali hasa neema ya Mungu ambaye anamsaidia kubaki imara. Zaidi
mtu anapata kuukiri udhaifu wake tena zaidi yeye anajiona mwenye haja ya neema
ya Yule ambaye alimwita. Kulingana na Mtakatifu Yohana Calabria, “Mungu hutumia
watu wanyenyekevu na wapole ili kutimiza mipango yake mikubwa kwa wanadamu.
Yeye hajui kufanya nini na wenye kiburi, kweli huwatoa mbali naye”.
Baada ya uzoefu mzuri kwenye ufuko wa bahari,
Yesu alirudi tena kijijini kwake na jumuiya yake, yaani, Nazareti. Huko ndipo
mahali ambapo Yesu angekaribishwa vizuri, lakini, haikutokea hivyo. Yesu alipata
upinzani kutoka wale waliodhani kwamba maarifa yao kuhusu asili ya kibinadamu
ya Yesu yalitosha ili kuwa uhusiano wa kweli na kina naye. Ni vigumu sana kwao
kutambua kazi ya Mungu katika mwenzao huyo waliyemwona kukua na kuishi nao hali
ya kawaida. Maarifa yao ya Yesu hayakuwa msaada bali kikwazo kwa kufungwa kwao
ili kupokea ufunuo Yesu aliowaletea. Kwa hitimisho, Yesu hakutimiza maishani
mwao aliyopanga kutenda kama yule aliye na kazi kudhihirisha uso wa huruma ya
Baba. Walidanganywa na maarifa yao wenyewe wa Mungu.
Ukosoaji mkubwa wa andiko hili ni kuhusu ugumu
wa kuamini. Kwa kuyajua mambo mengi ulimwenguni akili yatosha. Lakini hatuwezi
kusema sawa kuhusu uzoefu wa Mungu. Tunapaswa kuwa macho kwa sababu mawazo ama
mifano ya Mungu ambayo alijifunza kwa akili yetu inaweza kutuzuia kumjua kweli.
Hatuwezi kuridhika na kujua mambo juu ya Mungu; ni lazima kumruhusu yeye ajifunue
mwenyewe kwetu kwa nguvu zote za upendo wake. Kwa kupata hayo inahitaji imani.
Tunataka kupata mabadiliko ulimwenguni na katika maisha yetu, lakini katika
chaguzi na tabia zetu sio daima tunaonyesha kwamba tunaamini. Sisi bado tunaishi
kama watu ambao somo la kwanza liliongea: “Mataifa wa waasi, walioniasi mimi.” “Kweli
ikiwa siku hizi miujiza haitokei siyo kwa sababu haiwezekani bali haitokei kwa
sababu ya kosa la imani.”
Upinzani Yesu aliokabiliana miongoni mwa ndugu
zake na wananchi sio kwa maana ya kidini kuhusiana na matarajio ya Masihi
lakini pia kwa maana ya mahusiano ya kibinadamu sio tofauti sana na kile
kinachotokea mara nyingi katika mahusiano yetu na wengine. “Tuko na ugumu
mkubwa wa kuacha mipango yetu na njia yetu ya kuwahukumu wengine na hali
kandokando yetu! Mara nyingi tuko na haraka ya kuwahukumu kuhusu njia yao ya maisha,
nia yao na utambulisho wao. Hii si jukumu letu. Jukumu letu ni kujifunza daima
na kusikiliza kabla ya kuzungumza. Hakuna mtu anayekuwa shahidi ikiwa hafanyi uzoefu
na hakuna mtu anayekuwa nabii ikiwa haiwezi kusikiliza. Hata kwa ajili ya
chaguzi zetu za msingi uzoefu wa kusikiliza inakuwa rejeo ili tuweze kuwa na
utambuzi mzuri na kuamua kamili.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário