sábado, 21 de julho de 2018

MCHUNGAJI MWEMA ANAYAJUA MAHITAJI YA KONDOO



Tafakari kuhusu Mc 6, 30-34


       Andiko hili tunaweza kukuta pia katika injili nyingine (Luka na Mathayo); kila mmoja wao huleta vipengele maalum ambavyo anafanya hadithi hii kuwa nzuri hata zaidi. Kuhusu vipengele vilivyo sehemu zinazokutwa katika injili tatu, tuko na mashua, mkutano wa mwalimu na watu na matumizi ya andiko hili kabla ya kuzidisha ya mikate. Kuhusu tabia zingine, ikiwa tunachukua pia Luka 9, 10-11 na Mathayo 14, 13-14 tunaona kwamba ndiye Marco tu anayetaja kwamba “wanafunzi hakuwa na nafasi hata ya kula chakula”. Luka anaufuata mpango wa Marco, kwa kosa la kipengele kilichotajwa na hata ile huruma ya Bwana, lakini anataja jina la mahali ambapo walikwenda, yaani, Bethsaida. Mathayo, hata hivyo, hataji kushiriki kwa wanafunzi wala wanafunzi mashuani, tena wala jina la mahali, lakini anaongelea huruma ya Bwana mbele ya hali ya watu, kama Marco alivyo.

     Tunaguswa sana tukiona Yesu ambaye hakutumia tu wanafunzi wake kwa kazi bali alipatikana pia ili kusikiliza maelezo ya uzoefu wao. Hakika yeye aliutambua uchovu wao na haja ya kuwafundisha zaidi. Hivyo, aliwaalika kwenda naye kwenye mahali pa faragha. Hapo tunaona maelewano kati ya hamu ya Bwana ya kuwafundisha zaidi na haja ya wanafunzi wake ya kuingiza zaidi pendekezo la Bwana. Watu wengine walioangalia kutoka nje hawakuweza kuelewa uhusiano huu; waliweza kuelewa tu kwamba kupitia mwalimu yule na wanafunzi wake, ndiye Mungu aliye miongoni mwa watu wake, akichukua hali yao kwa upendo. Kweli, wakati walishuka kutoka mashua na kukutana na watu waliwatangulia, mara Yesu moja alielewa sababu ya utafutaji wao na kuwaonea huruma kwa sababu yeye ndiye Mchungaji mwema na kuyajua mahitaji ya kondoo.

     Kupitia kusikiliza kwake kwa macho na mwaliko ili waende peke yao naye kwenye mahali pa faragha, Yesu anaonyesha upendo kwa uhusiano na wanafunzi wake kama mama na watoto wake. Yeye anataka kubaki peke yake na wanafunzi ili kushughulika kwa ajili ya maisha yao na malezi yao. Nafasi hii waliyokuwa pamoja na Bwana itatumika kwa ajili wafanane zaidi maisha yao na yake. Yesu alijua kwamba haikuwezekana kufika mahali huko kulingana na mpango wake kwa sababu ya umati wa watu waliowatangulia kufika. Kisha, yeye alibadilisha mpango wake na nafasi ya pekee alikuwa nayo ili kuwako peke yake na wanafunzi wake ilikuwa ile mashuani. Hakika ilikuwa ni nafasi maalum ya kuimarisha uhusiano na kuanza tena kushiriki kwa wanafunzi na kusikiliza makini kwa Bwana. Yeye alichukua fursa hii ili kusisitiza jambo fulani zaidi ya yale aliyofundisha kabla ya kuwatuma kuinjilisha au kusahihisha baadhi ya mabadiliko kutoka kilichokuwa muhimu kweli. 

      Yesu anatualika kuingia mashuani pamoja naye na kukaa naye. Mashua hii si kusimama katikati ya “bahari ya maisha” lakini yasonga kuelekea umati unao na kiu kwa ajili ya Mungu na ya neno lake. Mashua hii ni mwaliko kwa urafiki na ukaribu. Tunafanya uzoefu wa kubaki pamoja na mwalimu si kwa kujifunza mafundisho fulani bali kutafakari maisha yake na kuingiza pendekezo lake ili tuwe kulingana na matarajio yake na baada ya kuwa wanaamini wa kweli tutaweza kutangaza kwa wengine. Vinginevyo, hatutapata mafanikio kazini. Kulingana na Fr. Raniero Cantalamessa, "Yule anayetangaza Neno hatagusa moyo wa wengine ikiwa Neno halikugusa moyo wake bado.” Neno hili ni Yesu, ambaye anataka kujaza maisha yetu ya maana na kutufungua kwa wengine. Ikiwa tunabaki naye zaidi, tena zaidi tunajiona kuelekezwa kwenye wengine. Ikiwa tunamwangalia yeye zaidi, tena zaidi mtazamo wetu kwenye wengine utakuwa wa upole na wa huruma.

   Pamoja na Yesu mashuani tunakueleza kwenye wengine sio ili kuwahukumu, lakini kuwaangalia tofauti tukijihusisha katika hali yao. Mbele ya hali ngumu ya watu ambao wanaonekana wamepotea na kuwa na kiu ya ndani ya kusikiliza Neno la kweli la Mungu, Yesu anatoa msaada wa kiroho kupitia maneno yake na baadaye anatoa pia msaada wa kimwili kupitia mikate na samaki. Lakini katika andiko hili, kwa muda, Mchungaji Mwema anatoa kuanza chakula kamili kwa sababu anajua haja ya kundi lake. Maudhui ya mazungumzo ya Mchungaji amejaa upole na huruma yangalikuwa nini? Askofu na Shahidi Oscar Romero alisema kwamba Yesu angalizungumza kwao “kwamba wokovu hutoka kwa Mungu peke yake, tena kwamba Mungu anatupenda, tena kwamba Mungu hatuachi, tena kwamba tupendane, tena kwamba tusitawanye.”

     Tuweze kuleta tangazo hili la furaha, kwanza kabisa kupitia maisha yetu yaliyobadilishwa na mkutano na Yesu Mchungaji Mwema na kisha, kwa maneno yetu pia.

Fr Ndega

Nenhum comentário: