Kutafakari kutoka 2Waf 4,
42-44; Waef 4, 1-6; Yoh 6, 1-15
Uwepo na matendo ya Yesu huonyesha ukaribu wa kiamilifu
wa Mungu. Moyo wake una hisia kwa hali halisi ya wale wanaohitaji kwa sababu umejaa
upole na huruma. Yote anayoishi moyoni mwake, Yesu anashiriki na wanafunzi wake
ili wajifunze kutoka kwake jinsi ya kushinda kutojali na wasiangalie tu bali
watende pia. Hili ni jukumu la kila “mtu wa Mungu”, kama vile tunaweza kuona
katika andiko la kwanza ambalo Elisha anaeleza kwa mtumishi wake kwamba
kushiriki zawadi katika jumuiya ni kuweka matendoni kusikiliza ya faida la Neno
la Mungu. Hakuna mtu aliye maskini mno asiye na kitu cha kutoa. Kile
tulichonacho kinatoka kwa Mungu nasi tunapokishiriki kinazidika kwa sababu hakuna
yeyote aliyeweza kushinda ukarimu wa Mungu aliye tayari daima kutupatia zaidi.
Katika andiko la pili, Mtakatifu Paulo anawaalika Wakristo waishi kulingana na
wito ambao wameitwa. Mwaliko huu unatukumbusha kuhusu hali ya ubatizo wetu
kupitia huu tumekuwa mashahidi wa ubaba wa Mungu, ambaye anatenda daima ndani
yetu na kupitia kwetu. Basi, Maisha yetu yaweze kuonyesha tendo lake la
ukarimu.
Kwa
nguvu yake peke yake, Yesu angeweza kutatua tatizo la umati wenye njaa, lakini
alitaka pia wafuasi wake wafanye kitu mbele ya mahitaji ya watu. Hali hii ni
kitu cha kuchukua kwa ahadi/sharti. Kwa hili tunapata katika wainjilisti usemi:
“Wapeni ninyi chakula” (Mt 14, 16; Mk 6, 37; Lk 9, 13). Katika kifungu cha
Yohana, swali kwa Filipi linaonyesha kwamba lile aliloagiza Bwana halimaanishi tendo
ambalo wanafunzi watimize peke yao, bali ndio mwaliko wa kushiriki katika mpango
ambao Mwalimu alikwisha amua moyoni mwake umejaa upole na huruma. Kila ishara
na neno la Mwalimu ni fursa mpya daima ya kujifunza kwa wanafunzi wake. Lakini kwa
kuelewa lile Bwana aliamua kutenda ni lazima kufikiri kama vile yeye ambaye
hatoi nafasi ya kwanza kwa fedha ilipaswa kutumika lakini kwa haja ya watu.
Kipaumbele ni mawazo ya kutoa na sio ya ulaji na ya ubadhirifu. Kwa hivyo,
hatimaye mwalimu aliwaomba wakusanye vipande vilivyoachwa.
Sura ya VI ya injili ya Yohana huanza na hadithi
hii nzuri ya kuzidisha mikate na kuendelea na mazungumzo ya Yesu juu ya mkate
wa uzima. Kwanza kabisa, baada ya kupita ng’ambo ya ziwa na kupanda mlimani, Yesu
aliona umati mkubwa wa watu. Mbele ya mahitaji yao, mtazamo wa Yesu ni wa
huruma, yaani: ndio mtazamo wa mtu anayeona hisia sio kwa moyo tu bali anatenda
pia kwa hamu ili kubadilisha hali. Watu hawa walimfuata Yesu kwa sababu waliona
ishara alizofanya kwa ajili ya wagonjwa. Uhusiano wa Yesu na watu ulikuwa kweli
wa ajabu, hasa kwa ajili ya maskini na ya walioteseka. Hali hii ilivutia watu waone
katika yeye utimizaji wa ahadi za kimungu. Katika Yesu, Mungu atembelea watu
wake na kutembea nao. Watu hawa waliomfuata Yesu walikwisha choka wa kuona
kwamba hali yao haikuwa muhimu kwa upande wa viongozi wao. Walikuwa kama kondoo
wasio na mchungaji na kwa hivyo, walikuwa wenye njaa na kiu kwa kila maana.
Yohana naye ndiye pekee yake ambaye - katika
tukio hili la kuzidisha mkate - analitaja jambo la Pasaka: “Pasaka, sikukuu ya
Wayahudi, ilikuwa karibu”; na mwishowe, anaongeza kwamba Yesu “alienda tena
mlimani yeye peke yake”. Wakati huu hakukubali uwepo wa watu wala wa wanafunzi
wake kwa sababu hata hao pia hawakuelewa maana ya ishara. Ndiye Baba tu anaweza
kuelewa. Ndiyo muhimu kukumbuka kwamba Mwinjilisti Yohana anapendelea kutumia neno
“ishara” badala ya “muujiza”. Ishara zote ambazo Yesu hutimiza katika injili
hii ndizo tangazo la kutarajia la “Saa” yake, yaani, Pasaka yake kupitia hii atamtukuza
Baba na kuhitimisha kazi yake ya ukombozi. Ndiyo maana inatumika msemi “Pasaka,
sikukuu ya Wayahudi” mwanzoni mwa kifungu hiki ili kuonyesha kwamba chakula kilichotolewa
na Yesu, yaani, neno lake na mwili wake, kitakuwa Pasaka mpya.
Jibu la Filipi ni ishara ya kosa la ushirika
na moyo wa Yesu anayejua haja yetu kabla ya tumwombe kitu. Mara nyingi, kama Filipi,
sisi huchukua muda mrefu tukifikiri kuhusu kile hatunacho na hivyo, hatufanyi
mema na kidogo tunacho. Andiko hili inazungumzia pia ushiriki wa Andrea, ndugu
wa Petro. Yeye alimtaja mtoto aliyeleta kitu ili kushiriki na kikundi. Ishara
ya mtoto ya kutoa kitu ilimpendeza Mungu aliyekitumia kwa ajili ya manufaa ya
wote. Tena mara nyingi, kama Andrea, tunatambua kwamba zawadi ziko lakini hatuwezi
kuitambua thamani zao. Yesu analaumu tabia ya kutojali lakini anatuambia kwamba
ndizo ishara ndogo anazozifanya kwa moyo ambazo zinaweza kufanya tofauti. Yesu
anatualika kushiriki na wengine nafsi yetu bora kama zawadi zinazotolewa kwa
Mungu. Kwa wema wake, Yesu amekwisha amua kutumia zawadi tuliyo sisi wenyewe
ili kulisha dunia kwa sababu katika njia hii maisha yetu yanachukua maana.
Kukubali ahadi hii ni changamoto kubwa kwetu nayo ndiyo jukumu la kila
mwanamme/mwanamke anayejiona “mtu wa Mungu”.
Fr Ndega