Kutafakari kuhusu Mt 21, 28-32
Tunaendelea na
habari kuhusu mwaliko wa Mungu ili watu wote wafanye kazi katika shamba lake la
mizabibu. Uamuzi wetu sio daima kulingana na matarajio yake, hata hivyo,
anaendelea kutualika. Katika kifungu cha leo Yesu anausimulia mfano mwingine
ambao unaleta kama wahusika wakuu familia fulani ambapo baba mmoja alikuwa na
watoto wawili na kumwomba kila mmoja mfanye kazi katika shamba lake la mzabibu.
Kila mmoja alijibu kwa njia tofauti na baadaye alibadili jibu lake. Yule ambaye
alijibu ‘hapana’, alifikiri vizuri, akatubu na kuamua kufanya kazi. Yule ambaye
alijibu ‘ndio’, hakuenda baadaye. Yule aliyefanya mapenzi ya baba ndiye yule
ambaye alienda kufanya kazi, hata baada ya wakati fulani.
Akisimulia mfano huu,
Yesu anaongelea tabia tofauti mbele ya mapenzi ya Mungu. Mwana mmoja anawakilisha
viongozi wa Wayahudi na mwana mwingine anamaanisha watoza ushuru na makahaba. Hotuba wa
Yohana ilikuwa na nguvu ya kuwathibitishia wasikilizaji wake. Bila shaka kwamba
kama ilivyotokea na manabii wa zamani, uwezo huu wa kuthibitishia ulitokana na
uzoefu wa kweli wa Neno la Mungu. Miongoni mwa wasikilizaji wa Yohane walikuwapo watoza
ushuru na makahaba na viongozi wa Wayahudi. Kikundi cha kwanza ingawa
walikataliwa na jamii kwa sababu ya maisha yao ya wenye dhambi, watakuwa wa
kwanza wa kukaribishwa katika maisha mapya maana walimwamini Yohane na
kuyakubali mapendekezo yake.
Tabia ya viongozi
wa Wayahudi ilikuwa tofauti, yaani, walimpinga Yohana Mbatizaji na pendekezo
lake la kutubu. Yohane alikuwa mpatanishi tu. Ndilo Neno la Mungu ambalo lina
nguvu lenyewe ili kuugusa moyo wa watu na kuubadilisha. Uhusiano ambao vikundi
hivi viliishi na Yohana unaendelea vivyo hivyo na Yesu. Mimi nataka kusisitiza
kwamba Yesu
haidhinishi maisha ya dhambi ya watoza ushuru na makahaba, bali tabia yao ya
kukaribisha vizuri ujumbe wake, wakitambua ukweli wa hali yao na kuuomba
msamaha. Hilo ndilo jibu ambalo linampendeza Mungu na kuwapa nafasi ya
kuokolewa.
Wakati wa Yesu, namna hii ya watu
waliwekwa katika kikundi maalum la wenye dhambi. Kuchanganyika nao kulimfanya
mtu apate dhambi yao pia. Yesu alichanganyika nao, akivuka mipaka iliyowekwa na
watu kwa sababu kwake mapenzi ya Mungu ni muhimu zaidi kuliko sheria ya
usafi/uchafu. Wakati tunajifikiriwa ubora au waliostahili zaidi kuliko wengine
tunaweka mipaka kwa mafanikio ya mapenzi ya Mungu na hali yetu inakuwa mbaya
zaidi kuliko kabla. Kupitia
Neno lake tunaweza kugundua mapenzi yake na kuyapanga maisha yetu kulingana na
mapenzi haya.
Ndiye Mungu ambaye anachukua nafasi ya kuwalika
watu, lakini anangoja na kuheshimu jibu la kila mtu. Kufanya kazi katika shamba
la mzabibu kunamaanisha kuingia katika ufalme. Mapenzi ya Mungu ni kuwaokoa
wote lakini uamuzi ndio wa watu. Mtu ambaye anajiona wa kwanza atakuwa wa
mwisho. Mungu anataka kwamba maneno na chaguzi zetu ziwe kulingana na mapenzi
yake kwa sababu hataki mtu akufe bali atubu na kuwa na uzima wa milele. Hasa
kwa wale ambao wanamfuata Yesu, mapenzi ya Mungu yapaswa kuwa kama chakula cha
kila siku kama yalivyo kwa Yesu mwenyewe. Ikiwa mapenzi ya Mungu ni kipimo cha
wokovu hakuna mtu ambaye astahili kuliko wengine. Yeye atupe unyenyekevu ili tutambue
hali yetu kama wenye dhambi na mapenzi yake yawe chakula cha maisha yetu kama
ilivyotokea na Mwanae.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário