Kutafakari toka Kutoka 22, 20-26; 1Thes 1, 5-10; Mt 22,
34-40
Maandiko Matakatifu yanashuhudia uhusiano maalum kati ya
Mungu na watu wake. Mungu alitaka kuanzisha agano na watu hawa akiwapa miongozo
kadhaa ili watende mema na kujenga hali nzuri kwa maisha yao. Ndiyo katika hali
hiyo kwamba Amri kumi zilizaliwa kama njia za uzima. Hakuna jambo lingine muhimu
katika safari yao ya waliochaguliwa ila kuishi Amri za Sheria kwa uaminifu. Kweli
kwa Watu wa Israeli Sheria ni kama Neno la Mungu na Neno la Mungu ni Sheria.
Wakati wao husema “Sheria ya Mungu ni kamili, faraja kwa roho”, wanaongelea
Neno la Mungu (Torati).
Kuna uhusiano wa ndani kati ya Sheria na Neno, kwa sababu
amri za Sheria zinaonyesha utunzaji na upendo wa Mungu kwa watu wake. Ndiyo
njia yake ya kutenda ambayo ilileta ukombozi na utambulisho kwa watu wa
Israeli. Mungu anatarajia tu watu hawa waweze kutenda kama yeye kati yao hasa
kwa ajili ya wanyonge (yatima na mjane) na wageni wanaohitaji msaada. Msingi wa
amri ni moyo na nia ya Mungu wa kihuruma. Kutii kwa amri ni chanzo cha baraka
kinachoelekeza kwa uzima, bali kutotii kunaelekeza kwa mauti.
Kwa bahati mbaya, pamoja na Sheria kuu, Wayahudi waliweka
sheria nyingi, akichukua lengo kutoka jambo muhimu lilioanzishwa na Mungu. Amri
kumi za awali zilikuwa amri mia sita kumi na tatu. Watu maskini walichukuliwa kama
wenye dhambi kwa sababu hawakuweza kukariri amri hizi zote na kwa hiyo, hawakuziweka
vitendoni. Hata hivyo, walijua muhimu ya Sheria. Hili ni jibu la Yesu aliposema:
“upende Bwana Mungu wako na moyo wako wote, na akili yako yote, na nguvu zako
zote” (Dt 6: 4-5) “na jirani wako kama unavyojipenda mwenyewe” (Lev. 19: 18).
Kumpenda Mungu ni amri ya kwanza ya zote, lakini Yesu aliiunganisha
na upendo kwa jirani, kuonyesha kwamba haiwezekani kumpenda Mungu bila kumpenda
jirani. Yakobo katika waraka wake anamfikiria kama mtu mwongo anayesema kwamba
anampenda Mungu na kutompenda jirani. Kutoka kumpenda Mungu amri ya kumpenda
jirani inabubujika kama matokeo. Chanzo ni Mungu daima kwa sababu ndiye aliyetupenda
kwanza. Ni kutokana na upendo wa Mungu kwetu tunaweza kuwapenda wengine halisi.
“hiyo ni changamoto kwa tamaduni zote hasa katika Afrika, ambapo uaminifu kwa
familia na mila unakuzwa mara nyingi kama amri ya kwanza.”
Uwepo na kazi ya Yesu
miongoni mwetu yaonyesha kwamba kwa kupitia upendo peke yake binadamu anaweza kupata
mafanikio kabisa kwa maisha yake. Bila shaka, kwamba kuwa mwana wa dini ama kuhudhuria
misa ni ishara ya upendo kwa Mungu kama kipaumbele katika maisha yetu. Hata
hivyo, katika mwisho wa maisha yetu tuliulizwa sio kuhusu dini ama misa bali
kuhusu upendo kwa wengine. Kipimo cha upendo wetu kwa Mungu kinaonyeshwa katika
njia kama tunavyowapenda wengine. Anapenda kweli yule anayetamani tu wema wa
yule anayependa, hata wakati hastahili. Hivi ndivyo Mungu anatupenda, yaani kwa
ukarimu na bure.
Muhimu kwa Yesu ni kumpenda Mungu, kwa kupenda jirani pia.
Ufundishaji wake wa ajabu ulibadilisha amri hizi mbili kuwa moja peke yake,
yaani: tupendane kama alivyotupenda. Kama vile Mungu ametupenda katika Kristo, hivyo
tunapaswa kupenda kutoka kwa Kristo. Yeyote anayependa kulingana na njia hii
amefahamu muhimu ya Sheria na ya maisha, kwa sababu yeyote anayefuata Yesu
hafuati sheria au mafundisho, bali anamfuata Mtu.
Basi, uaminifu wa tangazo
la Wakristu duniani ni katika kupenda wengine kama ndugu. Tunampenda Mungu
wakati tunapompa mahali pa
kwanza katika maisha yetu, kwa kutafuta kwanza ufalme wake na haki yake.
Tunapenda jirani wakati chaguzi zetu zinalenga kusaidia maisha na undugu juu ya
kila kitu katika jamii. Tunaonyesha upendo wetu kwa Mungu kwa
njia halisi sana wakati tunapochagua
kuhudhuria jumuiya badala ya kuchukua ahadi ya kibinafsi na tena wakati
tunapatikana kuwasaidia wengine kwa sababu ya hali fulani ya huzuni na mateso.
Hivyo, ilisemwa kuhusu Jimuiya za kwanza: “Oneni wanavyopendana”. Hali hii
iliwezekana tu kwa sababu walibakia umoja katika upendo wa Mtu aliyewaita. Tufanye
vivyo hivyo.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário