domingo, 22 de janeiro de 2017

WOTE WANAFURAHI KWA KIWANGO CHA NURU YAKO


Kutafakari kuhusu Is 8, 23-9,3; 1Cor 1,10-13.17; Mt 4, 12-23

      Nabii Isaya anaongelea wakati ujao wa utukufu na umejaa furaha katika safari ya watu wa Mungu. Mambo hayo yote yalitimia kwa nafsi na kazi ya Yesu. Yeye alianza kazi yake katika Galilaya, uliofahamiwa kama “mji wa wapagani” kwa sababu ya wengi wa wasio Wayahudi” ambao walikaa katika eneo hilo. Baada ya Yohane kuwekwa gerezani, Yesu hakuwa na hofu wa kukamatwa pia, bali alienda Kapernaumu na kuhudhuria katika hali ya watu, akiwaalika kwa toba/mabadiliko ya maisha. Yeye alitangaza ufalme wa Mungu sio kama hali mbali, bali ya karibu sana na hali ya watu kwa maana ufalme huu upo ndani yake Yesu mwenyewe.
  

     Yesu ni mwanga ambao watu hawa walimngojea kwa hamu sana. Pendekezo lake la toba lilikuwa mwaliko wa kupata kutoka gizani hadi kwenye nuru. Aliweza kufanya kazi peke yake, lakini alipendelea kuwaalika washirika ambao walijibu kwa upatikanaji kabisa. Kwa Yesu washirika wa kwanza wawili hawakutosha, kwa hivyo, aliendelea kutembea na kuwaalika wengine. Mwaliko wake una ahadi na kuomba ahadi kutoka jibu la watu. Watu walioitwa walikuwa wanyenyekevu wa Galilaya ambao walikuwa na desturi na hali ngumu ya maisha. Yesu aliwaona na kuangalia kwake kuelekeza kwenye ndani ya mioyo yao. Yeye aliangalia mbele na kuvutia kwa sababu alialika kuvua samaki tofauti na kubadilisha maisha. “Yesu alipomwona Simoni alilenga Jiwe kwa ajili ya kanisa lake; yeye alipomwona Yohane alimwona mtu mwenye tabia ya kiroho; na wewe, Je, anapokuona analenga nini?         
      Katika injili ya Yohane tunakuta kifungu ambacho kinasema, “nuru iliangaza gizani nazi giza hazikupata kuishinda.” Maneno haya ni tangazo la ushindi wa Kristo na wa wanaomfuata kwa ajili ya kupata nuru ya uzima. Akiwaita washirika, Yesu alishiriki nao nuru yake mwenyewe ili wawe nuru kama yeye alivyo. Ushuhuda wa waliomfuata Yesu ni nuru kwa maana unajaza na maana maisha ya watu. Nuru ilifanyika itie nuru na kufikia lengo lake wakati inapotoa nguvu na uhai kwa vyote. Ilitokea hivyo tangu mwanzo, yaani, wakati Mungu aliposema “nuru ifanyike”! Nuru ilifanyika na uhai ukatokea. Mwanga wa Mungu ni hekima yake, tena ni msukumo wake, pia ni Neno lake. Yeyote ambaye anaruhusu kuongozwa na nuru hii anaweza kuona vizuri ili afikie malengo yake.


       Ni vizuri kujua na kuhisi kwamba hatuko gizani tena. Mwanga mkubwa uliangaza kwetu na ilikuwa ni kwa uhuru kwamba Kristo ametuweka huru. Hili likawa jukumu la Kristo kwa maana yu mwaminifu. Kwa upande wetu, tunapaswa tutoke nguvu za giza kwa maana sisi hatujateketezwa kwa nguvu za giza. Hivyo, Mtakatifu Paulo asema: “kama wakati wa zamani mlikuwa wa giza, sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Muwe na tabia ya watoto wa nuru” (Ef 5,8). Anatukumbusha kwamba baadhi ya mgawanyiko kati yetu unazuia mwangaza wa nuru hii ukisababisha hali tofauti na ile iliyotakwa na Yesu kwa Kanisa lake. Inawezekana tuweze kuikuta njia tena, ikiwa tunachukua Kristo tena kama muhimu sana katika kila kitu tunachofanya.  Mara nyingi mgawanyiko unasababishwa kwa maana, katika safari yetu ya kuvua wanafunzi wapya, hatufanyi kwa ajili ya Kristo bali kwa ajili yetu wenyewe. Tunalitumia jina la Mungu kuwatendea watu mema. Hili ni sawa! Watu waliosaidiwa walijiona kushikamana nasi. Hii ni hatari! Kwa sababu ya kosa la utambuzi, wanabaki kuhusishwa kwetu kuliko kwa ajili ya Kristo peke yake. Na wakati Kristo sio umuhimu kati yetu, mgawanyiko unatokea. Tuwe macho kwa namna hii ya kuwavua wanafunzi. 

       Kama wafuasi wa Yesu, tumechukua jukumu la kuwa ni nuru. Wakati wa ubatizo wetu, yasemwa kwetu: “mtoto fulani, umeangazwa na Kristo aliye Mwanga wa ulimwengu. Tembea kama mtoto wa nuru.” Kila siku tumeangazwa na nuru ya Neno la Mungu ili tuweze kuwaangaza wengine kutoka nuru hii. Kulingana na Yesu uzoefu huu hauwezi kufichika. Siku ya leo yeye anasema kwetu, “nuru yenu iangaze mbele ya watu ambao wakiyaona matendo yenu mema wamtukuze Baba aliye mbinguni.” Furaha ya mkutano wetu na Bwana haiwezi kufichika. Yapaswa kutangazika. Uamuzi wa kuificha nuru inaonekana iwe tabia ya unyenyekevu, lakini inaonekana pia iwe aibu ama kosa la ujasiri na shauku. Hivyo, nuru haiwezi kutimiza lengo lake. Wakati matendo yetu yatendeka kwa ajili ya Mungu hatuna sababu ya kuyaficha hayo. Ikiwa tunahitaji kuficha baadhi ya matendo yetu ni kwa sababu nuru ya ukweli haiko. Siku moja ukweli wa matendo yetu utagundulika na utambulisho wetu wa kweli utadhihirishwa. Tukifikiria haja ya toba daima, tukaribishe Neno la Yesu kama nuru ili tuweze kuwaangaza wengine kutoka nuru hii ambayo imo ndani yetu.    

Fr Ndega




Nenhum comentário: