Kutafakari kuhusu Is 49,3.5-6; 1Cor 1, 1-3; Yoh 1, 29-34
* Ubatizo wa mtoto Tamele na miaka kumi na mitano ya padre Josuel Ndega
Tunataka kutafakari kuhusu shuhuda tatu ambayo
inatusaidia kuishi vizuri wito wetu, yaani, kwanza, ushuhuda wa Mungu kuhusu
mtumishi wake (somo la kwanza); pili, ushuhuda wa mtakatifu Paulo kama mtume
kwa mapenzi ya Mungu (somo la pili); na tatu, ushuhuda wa Yohane Mbatizaji juu
ya Yesu kama Mwana kondoo wa Mungu (injili). Tutalenga ushiriki wetu katika
upadre wa Kristo.
Kuhusu ushuhuda wa Mungu, huu ni mmoja wa
nyimbo ya mtumishi wa Bwana iliyoandikwa wakati wa utumwa wa Babeli nasi
tunaweza kuukuta wimbo huu katika sehemu ya pili ya kitabu cha Isaya. Ni jambo
la ajabu njia ya Mungu ya kuongea kuhusu mtumishi wake. Kwanza kabisa kuna mpango.
Mungu wetu hatendi kwa njia yoyote. Yeye anajua mtumishi wake kwa maana yeye
mwenyewe alimwandaa tangu tumboni mwa mama yake na kumjulisha kwa upendo kwa
sababu maisha ya mtumishi huyo yanampendeza. Mtu aliyeamua kuwa padre alichagua
kuwa mtumishi na maisha yake yanampendeza Mungu kwa sababu hatafuti nafsi yake
mwenyewe bali utukufu wa Mungu. Uhusiano wa upendo na Bwana wake ni maana ya uaminifu
katika safari yake ya wito (cf. 1Sm 2,35). Huu ndio uzoefu unaozaa utambulisho
na kutoa maana kwa utume, ukimsaidia kuishi wito wake kwa furaha. Kutafakari
kuhusu wimbo huu ni nafasi ya kufanya upya ahadi yangu kama mtumishi nikimshukuru
Mungu kwa zawadi ya upadre na kwa maana yupo pamoja nami daima.
Maandiko matakatifu yanashuhudia kuhusu uaminifu
wa Mungu kwa ajili ya watumishi wake kama njia yake mwenyewe ya kutenda na kama
njia kamili ya kufanya mapenzi yake. Anajua kuhusu udhaifu ya watumishi wake;
kwa hivyo, anabaki karibu na kutenda pamoja nao ili wawe waaminifu. Uaminifu wa
Mungu ndio mwaliko ili tufanye vivyo hivyo. Huu ndio muhtasari wa maisha ya
Mtakatifu Paulo katika somo la pili. Yeye anajua sana kwamba wito wake kama
mtume wa Yesu Kristo ni mapenzi ya Mungu. Mtakatifu Paulo aliishi wito wake kwa
hamu sana na kwa upatikanaji kabisa kwa ajili ya kuinjilisha. Ushuhuda wake wa
maisha unatusaidia sana kufahamu maana ya ushiriki wetu katika upadre wa Kristo
kupitia ubatizo. Kama wabatizwa sisi ni washiriki wa mwili wa Bwana nasi tunaalikwa
kutenda kwa ajili ya kulijenga kanisa, ambalo ni mwili wake. Katika kila mmojawapo
aliyebatizwa tunatambua uwepo wa kanisa zima. Kile kinachotokea katika maisha
ya mmoja wetu ni jukumu la mwili mzima. Wito wetu tunaishi katika jumuiya moja,
lakini kwa ajili ya kanisa zima.
Mfano mwingine muhimu sana ni ushuhuda wa
Yohana mbatizaji. Yeye aliweza kumtambua Yesu kama “Mwana kondoo wa Mungu
aondoaye dhambi za dunia”, kwa sababu alikuwa macho kwa msukumo wa Mungu kama
vile imetokea daima (tumboni mwa mama Elizabeth, jangwani, mtoni Yordani na
kupita kwake Yesu, kulingana na andiko la leo). Kubatizwa ni kushiriki uhai wa
Mungu kwa kuingia katika mwendo wa Roho Mtakatifu anayesababisha kuzaliwa upya na
furaha kubwa katika familia yetu ya kiroho, yaani Kanisa. Kulingana na Baba
mtakatifu Fransisko, “Kila mtoto anayezaliwa ni zawadi ya furaha na matumaini,
na kila mtoto anayebatizwa ni muujiza wa imani nayo ni sikukuu kwa familia ya
Mungu.” Jina linalotajwa wakati wa ubatizo linapokea maana mpya na utambulisho
mpya. “Mungu mwenyewe anataka jina lako liwe jina lake la pili. Uingizwe katika
orodha hii: Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Anna,
Mungu wa Daudi,” Mungu wa Clementina, Mungu wa Josafá, Mungu wa Maria, Mungu wa
Tamele.
Yohane alisema mara mbili kwamba hakumjua Yesu,
lakini kwa msukumo wa Mungu, aliweza kumtambua Mwanawe. Na baadaye Yohane
alisema “niliona na kushuhudia”. Kuwa padre ni kuwa shahidi wa yale anayotenda
Mungu duniani na maishani mwa watu. Padre ni mtu anayetafuta kumjua Mungu daima
ili aweze kumtambua na kumwonyesha kwa wengine. Padre ni chombo cha huruma kwa
maana yeye kwanza ameguswa na huruma hii. Upadre ni kama “Ubuntu”, yaani huu ni
uzoefu ambao mtu anajiona mmoja na wenzake wa jumuiya, kwa maana kuwa padre ni
kuwa ndugu kati ya wenzake na kwa ajili ya uhai wao. Tumshukuru Mungu kwa
upadre!
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário