terça-feira, 27 de setembro de 2016

HALI YA MASKINI INATUHUSU SISI


Kutafakari kuhusu Lk 16, 19-31

     Mungu anashutumu kutofautiana na unafiki katika safari ya watu wake na anapendekeza njia tofauti. Kulingana na somo la kwanza, utumwa katika safari ya Waisraeli ulikuwa matokeo ya kosa la uhusiano mwema na Mungu na la ahadi ya kuujenga undugu. Ibada yao ilibadilika kuwa jambo bila maana, yaani haikuonyesha tena ukarimu wa moyo wala haikusababisha mabadiliko katika uhusiano miongoni mwa watu na katika jamii. Walio na nguvu waliishi kwa kutofautiana mbele ya hali ya wengine na matendo ya nje hayakuihusu tabia ya ndani. Wakitenda hivi walivutia hali mbaya kwa maisha yao. Lakini tunajua kwamba Mungu hakuwaacha watu hawa, akitenda kwa uaminifu hasa kuhusu hali ya maskini na wasio na nguvu kwa maana maisha yao yanathamini sana kwa Bwana. Somo la pili linaonyesha ushuhuda wa Mtakatifu Paulo kuhusu Timotheo. Kulingana na ushuhuda huu haiwezekani kuwa mtu wa Mungu kwa kulitumia jina tu. Utambulisho wa mtu wa Mungu wa kweli unaonyeshwa kupitia kufuata haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu na upole.   

       Kama tujuavyo, mifano ni sehemu ya ajabu ya ufundishaji wa Yesu. Kupitia mfano yeye anaweka rahisi na kupatikana kwa wote siri za Ufalme wa Mungu. Katika andiko hili, Yesu anasimulia mfano wa mtu tajiri na Lazaro maskini anawaonya wasikilizaji wake kuhusu hali ijayo iliyo matokeo ya chaguzi za watu katika wakati huu. Mtu tajiri ni ishara ya walio na mazoea ya kuitumainia mali bila kuguswa na hisia kuhusu kile kinachotokea kandokando yao. Hao walichagua kwa nafsi yao njia ambayo itawaongozea mauti. Lazaro ni ishara ya walio maskini ambao wameachwa bila ulinzi na utunzaji; wanapiga kelele ili wapate nafasi ya kuishi kwa heshima. Tena Lazaro ni pendekezo la kuishi tofauti, kuyalenga maisha katika thamani za kweli. Huyo ni ishara ya uvumilivu, ya mapigano na mwaliko wa kumtumainia Mungu ambaye katika riziki yake hawaachi wale ambao wanamwamini.

       Kupitia mfano huu Yesu anatukumbusha kuhusu hali ya kikatili ambayo ipo katika jamii yetu, yaani kutokuwa na usawa kati ya watu. Katika mafundisho yake, Kanisa limeshutumu hali hii mara nyingi kwa kusema, “Hali mbaya ya jeuri imezaa matajiri walio na utajiri zaidi daima juu ya maskini walio maskini zaidi daima.” Hali hii ni tofauti kabisa na matarajio ya Mungu ambaye, kulingana na wema wake, ananyesha mvua kwa wenye haki na wasio na haki, tena kwa walio wema na kwa wabaya ili vitu vyote alivyoumba kwa wote vipatikane kwa wote. Mfano mzuri tunapata katika Wimbo wa Bikira Maria ambao unaishuhudia njia ya ajabu ya Mungu ya kutenda, yaani yeye huwashusha wakuu na kuwapandisha wadogo ili waweze kuishi pamoja kama ndugu na kwa usawa wa haki na wa heshima. Mungu anajitambulisha na hali ngumu ya wasio na nguvu na ya maskini. Udhalimu wote unaofanyika kwao unamgusa Mungu ndiye kuwepo katika upande yao. Katika wakati ujao, baada ya hali ya dunia, hali itakuwa tofauti, yaani waliopokea mambo mema katika maisha yao bila ahadi na hisia kuhusu hali ya wengine wataumizwa na wale waliopata mabaya kama Lazaro alivyo, watafarijiwa. Yeyote ambaye anatumia mali yake ili awadharau wengine anatupa maisha yake takatakani kwa sababu maisha hayamaanishi mali mengi bali uwezo wa kutenda mema. Kuhusu mambo haya Mt. Yohana Calabria alikuwa na haya ya kusema: “Maskini wako ili matajiri waokoke/waokolewe”. 

     Hali ya maskini ina uhusiano na sisi sote, kwa sababu “dhambi ya jamii ni matokeo ya kiasi cha dhambi za kibinafsi”. Basi, ni lazima toba/mabadiliko sio kwa ajili ya dhambi za kibinafsi tu, bali pia kuchukua jukumu kuhusu dhambi ya kijamii. Mwendo huu unaweza kwanza kupitia tabia ya kuacha njia ya ukusanyaji ambayo kwa kawaida inatuongoza kuwa na kutofautiana kuhusu hali ya wengine. Tunaalikwa kuchukua njia ya unyenyekevu inayokihusu kitu kidogo na kutufanya kuguswa na hisia kuhusu wale wasio na kitu. Mungu anatuokoa maana ya upendo wake, lakini anathamini sana juhudi zetu kama alivyosema Baba Mt. Benedito wa kumi na sita: “kwa kweli, wokovu ni zawadi iliyo neema ya Mungu, lakini ili uwe ufanisi katika maisha yangu unadai ridhaa yangu, ambayo inaonyeshwa kupitia matendo, yaani kupitia utayari wa kuishi kama Yesu alivyo kwa kuufuata mfano wake.” 

Fr Ndega

quarta-feira, 21 de setembro de 2016

NEGRITUD Y SEGUIMIENTO DE JESÚS


Fuimos bendecidos por Dios con este mes que dedicamos en honor a la Biblia o a la Palabra de Dios, especialmente presente en la biblia. En esta reflexión, queremos recibir las provocaciones de la Palabra de Dios para ver como estamos y que es lo que debemos hacer para seguir verdaderamente a Jesús.

Jesús nos llama a seguirlo, pero no quiere que lo sigamos de cualquier manera. No podemos seguirlo a partir de un “oí decir”, sino por convicción, que nace de un encuentro personal con él mismo. Según el documento de Aparecida, no seguimos una idea o una doctrina, sino una persona: Jesucristo. Lo que sabemos sobre él no es fruto de nuestras ideas, sino un recibir de aquello que él mismo reveló sobre sí, estando entre nosotros. Jesús no vino para morir en la cruz, sino para salvarnos. Su compromiso profético lo llevó a la cruz. Él la abrazó por amor, para que ella no sea más señal de muerte para nadie. Su gesto fue recibido por Dios, que respondió con la resurrección. Por lo tanto, por detrás de la cruz, aparentemente señal de muerte, está el gesto de amor de Cristo que conduce a la vida. Él no paró en la cruz, pues detenerse en la cruz es dejarse dominar por las fuerzas de la muerte de la sociedad injusta, pero él simplemente venció la muerte, conduciéndonos a la vida plena por la resurrección. Por este motivo, la cruz pasa a ser parte de su vida y misión.

Aceptando la cruz, Jesús le da un nuevo significado y la propone como condición para todos los que desean seguirlo. Para seguirlo verdaderamente, necesitamos estar dispuestos a cargar también la cruz. Necesitamos entender la cruz como parte de un proceso de madurez en el seguimiento y como señal de nuestra entrega en vista del bien de los demás; como consecuencia de nuestra fidelidad a Jesús y a su proyecto. Es necesario, primero, renuncia a sí mismo y eso exige cambio de vida y de mentalidad, o sea, no da para decidir por Jesús y continuar actuando de la misma manera que antes. Después, debe asumir cada día la cruz de sus propias dificultades y ser solidario/a con la cruz de los otros. Traicionamos nuestra vocación de seguidores y seguidoras de Jesús cuando preferimos ser cruz en la vida de los otros, en vez de ayudarlos a cargar sus cruces.

Cuando hablamos en biblia y en pueblo negro, vemos que tienen muchas cosas que ver, pues, parte de las historias bíblicas sucedieron en África y envuelven africanos. José, hijo del patriarca Jacob fue recibido en África (Egipto) y allá fue valorizado con su talento de intérprete de sueños – para el pueblo africano, la revelación de Dios se da también a través de los sueños. Moisés fue iniciado en los conocimientos africanos (ciencia egipcia) y se volvió poderoso en palabras y obras. Jeremías estaba preso en una cisterna, durante la invasión de Babilonia a Jerusalén y fue salvado por Ebed Melec, un africano, empleado del Rey. Jesús fue recibido en África (Egipto) para escapar de la persecución de Herodes y cuando conducía la cruz al monte Calvario, fue ayudado por un africano, llamado Simón, de la ciudad de Cirene, de Libia. Un funcionario de la reina Candase, de Etiopía, fue evangelizado y bautizado por Felipe, de suerte que cuando la naciones europeas invadieron África, ya existía el cristianismo allí. Es por eso que todavía hoy existen en África las Iglesias Apostólicas Tradicionales (de los primeros siglos) y la Iglesia Católica Romana (de los tiempos de la colonización).

En tiempos de colonización la biblia fue utilizada por los colonizadores para justificar la esclavitud y se insistía mucho en la figura melancólica de Jesús, excesivamente dulce, que aceptó el sufrimiento porque era voluntad de Dio, de manera que todo intento de fuga o de desobediencia al señor de esclavo era actuar contra las enseñanzas de Jesús y, por lo tanto, quedar impedidos de recibirlo en la eucaristía. Esta situación incidía a la comunidad negra actitudes de conformación al sufrimiento, a la esclavitud. Aquellos que hablaban de la Biblia y de la cruz de Cristo aumentaban el peso de la cruz de los oprimidos en vez de ayudarlos a cargar sus cruces. La biblia es utilizada, entonces, como instrumento de opresión y obstáculo en la lucha por la dignidad y la libertad. El problema no está en la Biblia en sí misma, sino en quien está con la Biblia en la mano y se atreve a hablar de ella.

A lo largo de todo este período, la propia comunidad negra había percibido que aquellos que catequizaban dejaban mucho que desear sobre el verdadero significado del mensaje que llevaban.  A partir de su propio descubrimiento sobre Jesús, la comunidad negra se dio cuenta de su identificación y solidaridad en relación a los pobres y todos los que sufren; y su compromiso en vista de la transformación de esta realidad. Descubrieron que sus señores catequistas habían vaciado la biblia de su fuerza profética. Redescubrieron, entonces, la biblia como fuente de liberación y de vida nueva. La presencia de afrodescendientes siguiendo fielmente a Jesucristo, viene marcando significativamente la vida de la Iglesia, contribuyendo, de forma dinámica, para que ella cumpla con fidelidad la misión que recibió. En contrapartida, esta Iglesia “Madre” ha buscado realizar un discipulado reparador, reconociendo los límites de la evangelización pasada, apoyando e incentivando la comunidad negra en sus justas reivindicaciones en vista de la vida plena, profecía del Reino de Dios.

Axé.

Padre Josuel Ndega

Traducción: Nómade de Dios.

NON SI PUÒ SERVIRE DUE PADRONI


Riflessione su Lc 16, 1-13

       Dio desidera per il suo popolo lunga vita e dignità. Tutte le cose che non vanno in questa direzione vengono da lui rifiutate. Così, tramite il profeta Amos, nella prima lettura, Dio ha condannato tutte le forme di oppressione che impediscono di vivere come popolo di Dio, soprattutto la situazione di violenza contro i poveri e gli affamati. La loro sofferenza è una dimostrazione che abbiamo una società ingiusta dove esistono persone potenti, che hanno proprietà e ricchezze, mentre altre non hanno il sufficiente per vivere. Anche noi se non siamo attenti, diventiamo collaboratori di questa ingiustizia sociale, che è il risultato di un accumulo di peccati personali. A proposito di questo Papa Francesco dice: "Il consumismo ci ha indotti ad abituarci al superfluo e allo spreco quotidiano di cibo... Ricordiamo bene, però, che il cibo che si butta via è come se venisse rubato dalla mensa di chi è povero, di chi ha fame!" La situazione di queste persone era una priorità nella missione di Gesù che ha preso l’impegno di essere povero per arricchire tutti con la sua povertà.

       Nella seconda lettura, San Paolo ci consiglia di pregare per tutti gli uomini specialmente per coloro che hanno l'autorità di condurre e di governare: ministri della Chiesa, capi di governo e così via, affinché possano fare il loro lavoro bene, così che tutti possiamo vivere una vita di serenità e di pace. Noi siamo di Dio, e pertanto, l’autorità che i capi hanno sulle nostre vite è solo una partecipazione nella missione di Dio stesso che vuole che tutti gli uomini siano salvati e che conoscano la verità. È anche nostra responsabilità che facciano un buon lavoro e questo è gradito a Dio. Continuando la nostra riflessione, abbiamo una parabola in cui Gesù ci parla della necessità di essere fedeli nel compito che abbiamo ricevuto da Dio. Ciò che abbiamo appartiene a Dio, per cui ogni bene viene da lui. Lui ci affida la custodia di tutto e aspetta che noi agiamo secondo la sua volontà. Non siamo i proprietari, ma gli amministratori dei doni di Dio, per questo dovremmo usare i soldi non come fine nella vita, ma come strumento per produrre buone condizioni per tutti.

         Viviamo in una società dove il denaro è la misura di tutto e tutto dipende dal denaro. Si tratta di un potente mezzo di vita per molte persone. I cristiani, che comportamenti devono avere di fronte alla ricchezza? Coloro che seguono Cristo dovrebbero essere onesti in tutte le cose e avere il giusto comportamento in relazione alla ricchezza. La mancanza di un giusto rapporto con questa ci conduce a dimenticare la cura per la famiglia, l’attenzione alla propria salute, una vera relazione con Dio e con gli altri. Spesso nel rapporto con Dio c’è qualcosa che non va bene a causa del nostro desiderio di avere sempre più ricchezze. Gesù non sta dicendo che il denaro non è importante, ma dice che non possiamo lasciarci prendere e schiavizzare dal denaro. Gesù vuole che ognuno comprenda che soldi non possono garantirci i valori che generano vita e felicità. Noi possiamo usare i soldi per servire Dio, ma non possiamo usare Dio per trovare soldi. Su questo dobbiamo essere vigili perché questo può accadere e spesso senza che ce ne rendiamo conto. Il denaro è pericoloso perché può farci insensibili all’ amore di Dio e ai bisogni degli altri.

       Il denaro ci aiuta a vivere, ma ha messo anche persone lontane tra loro. Il denaro può costruire una casa ma anche può distruggere famiglie. Attraverso il denaro possiamo comprare vestiti, cibo e così via, ma possiamo anche produrre privilegi, corruzione e discriminazione. Non possiamo permettere che i soldi siano motivo di differenza tra di noi, conducendoci a discriminare gli altri. Tra noi sappiamo quanto il denaro è stato importante, soprattutto per quanto riguarda l'offerta per l'edificazione e manutenzione della chiesa-tempio e per le molte attività della evangelizzazione. Ringraziamo Dio per l'uso del denaro come espressione di generosità per il bene delle nostre comunità. Chiediamo la grazia di usare il denaro che abbiamo non come strumento di discriminazione, ma piuttosto come uno strumento di solidarietà, costruendo fraternità. 

Don Josuel Ndega
Revisione: Signora Giusi






domingo, 18 de setembro de 2016

HATUWEZI KUWATUMIKIA MABWANA WAWILI


Kutafakari kuhusu Lk 16, 1-13


       Mungu anatarajia kwa watu wake maisha marefu na kwa heshima. Mambo yote ambayo hayaisaidii hali hii yanakataliwa na Mungu. Hivyo, kupitia nabii Amos, katika somo la kwanza, yeye (Mungu) anashutumu aina yote ya ukandamizaji ambao uliwazuia watu waishi kama watu wa Mungu hasa hali ya udhalimu dhidi ya maskini na wenye njaa. Mateso yao yadhihirisha kwamba tuko na jamii ya kijeuri ambapo wako baadhi ya watu wenye nguvu kwa sababu wanamiliki mali na pesa nyingi wakati wengine wengi hawana kilicho cha kutosha kwa kuishi. Sisi pia kama si makini tunaweza kusaidia ili hali ya udhalimu wa kijamii uongezeke kwa sababu dhambi ya kijamii ni matokeo ya kiasi cha dhambi za kibinafsi. Kuhusu hayo Baba Mtakatifu Francisco asema: “Ulaji umetuongoza kutumia vitu bure pamoja na ubadhirifu wa chakula cha kila siku... Tunapaswa kukumbuka kwamba chakula ambacho sisi hutupa takatakani ni kama ikiwa tulikuwa tumeiba kutoka meza ya walio maskini na wenye njaa.” Hali ya watu hawa ilikuwa kipaumbele katika kazi ya Yesu ambaye alichukua ahadi ya kuwa maskini ili kuwatajirisha wote kwa umaskini wake.    

         Katika somo la pili, Mt. Paulo anatushauri kuwaombea watu wote hasa wale ambao wako na mamlaka ya kuongoza na kutawala, yaani Viongozi wa Kanisa, Serikali na kadhalika. Hao wanapaswa kufanya kazi yao vizuri ili tuweze kuishi maisha ya utulivu na amani. Sisi ni wa Mungu na kwa hivyo, kazi ya viongozi wote kwa ajili ya maisha yetu ni ushiriki katika utawala wa Mungu mwenyewe ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Ni jukumu letu ili watawale vizuri nayo inampendeza Mungu. Tukiendelea kutafakari kwetu, tuko na mfano ambao Yesu alisimulia kuongea kuhusu mahitaji ya kuwa mwaminifu katika jukumu ambalo tumepokea kutoka kwa Mungu. Kile kilicho nacho kinatoka kwa Mungu kwa sababu vyote vyatoka kwake. Anatukabidhi utunzaji wa vyote na kutarajia tupate kusimamia zawadi zake kulingana na mapenzi yake. Sisi sio walio na mali bali wasimamizi wa zawadi za Mungu. Hivyo, tunapaswa kuitumia pesa sio kama lengo la maisha, bali kama chombo cha kuizaa hali nzuri kwa wote.

          Tunaishi katika jamii ambapo pesa ni kipimo cha kila kitu na pia inaonekana kwamba pesa inatutawala. Kila kitu ambacho tunahitaji hakiwezekani kupata bila pesa. Hii ni nguvu na maana ya kuishi kwa watu wengi. Je, Wakristo wanapaswa kuwa na tabia gani mbele ya utajiri? Wale wanaofuata Kristo wanapaswa kuwa waaminifu katika mambo yote na kutumia tabia kamili kuhusu pesa. Kutokuwa na tabia kamili kuhusu jambo hili kunatuongoza kusahau uangalifu kwa ajili ya familia, utunzaji kwa afya yenyewe, uhusiano wa kweli na Mungu na kadhalika. Mara nyingi uhusiano wetu na Mungu unasumbuliwa kwa sababu ya hamu ya kuwa na pesa na mali nyingi. Yesu hasemi kwamba pesa si muhimu, lakini asema kwamba haiwezi kutushika na kutumiliki. Yesu anataka tufahamu kwamba pesa haijengi thamani za kweli ambazo zinazaa uzima na furaha. Tunaweza kuitumia pesa ili kumtumikia Mungu, bali hatuwezi kumtumia Mungu ili tupate pesa. Tunapaswa kuwa macho kwa sababu hali hii inaweza kutokea na mara nyingi bila tuweze kuitambua hiyo. Pesa ni kitu ambacho kinaweza kututumia na kutubadilisha kuwa wasio na hisia kwa ajili ya Mungu na kwa mahitaji ya wengine.     


       Pesa inatusaidia kuishi lakini imewaweka watu mbali sana wao kwa wao. Pesa inaijenga nyumba lakini inaweza kuharibu familia. Kupitia pesa tunaweza kuinunua nguo, chakula na kadhalika, lakini pia inaweza kuzaa upendeleo, ubaguzi na utoaji rushwa. Hatuwezi kuruhusu kwamba pesa iwe chombo cha tofauti kati yetu, kutuongoza kuwabagua wengine. Kati yetu tunajua jinsi vile pesa imekuwa muhimu, hasa kuhusu sadaka ya ukarimu kwa ajili ya kulijenga kanisa-hekalu na kwa ajili ya mahitaji mengi katika kazi zetu za uinjilishaji. Tunamshukuru Mungu kwa matumizi ya pesa kama maonyesho ya ukarimu kwa manufaa ya jumuiya zetu kwa kulijenga Kanisa la Bwana. Tena tumwombe neema ya kuwa na tabia kamili mbele ya pesa kutumia ishara hii si kama chombo cha ubaguzi, bali kama chombo cha undugu.   

Padre Josuel Ndega

sábado, 10 de setembro de 2016

MUNGU ANAFURAHI SANA TUNAPOMRUDIA YEYE


Kutafakari kuhusu Lk 15, 1-32

Sura ya kumi na tano ya toleo la Luka ni maarufu miongoni mwa mifano ya Yesu. Hii inaitwa sura ya Mifano ya huruma. Tuko na mifano mitatu (Kondoo aliyepotea: 4-7; Sarafu iliyopotea: 8-10; Mwana mpotevu: 11-32). Mifano hii inaonyesha tabia ya huruma ya Mungu kuhusu wenye dhambi na furaha ya kukutana tena na yule ambaye alipotea. Kwa kufahamu nia ya Yesu alipoisimulia mifano hii tunahitaji kutafakari kwanza kuhusu mazingira ambayo Yesu aliishi. Katika muktadha huo, baadhi ya watu walijiona waliostahili wokovu wa Mungu kwa sababu ya uaminifu wao kwa Sheria. Walichukua mamlaka ya kuwatenganisha watu, wakiwapanga kama wema au wabaya. Mamlaka haya hayatoki kwa Mungu kwa sababu kipimo ni ubaguzi. Walisahau kwamba mbele ya Mungu watu wote ni sawa. katika njia yake ya kupenda Mungu hambagui yeyote. Kwa upande wake watoza ushuru na wenye dhambi ni watoto wake kama vile ndio Mafarisayo na Waandishi. Ikiwa hao wanaweza kuzaa undugu, tena wataweza kuishi katika ushirika na Mungu, anayekaribisha kila mtu ili awaokoe wote.

          Ingawa yako matukio mengi katika Agano la Kale, ambayo yanaonyesha njia maalum ya Mungu ya kutenda, ni “katika Yesu Kristo kwamba huruma ya Mungu imepata kuwa hai na yenye kuonekana, na hata ilifikia kilele chake katika Yeye... Yesu ni uso wa huruma ya Baba. Kila kitu ndani yake kinaongelea huruma. Hakuna chochote kwake kinachopungukiwa na huruma (Baba Mt Francisco).”  Kama alama ya huruma ya Mungu, Yesu ana chaguo wazi sana, yaani, “Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao”. Maneno haya yalisemwa na wale waliompinga Yesu. Kwa kweli, Yesu alikuwa na njia maalum ya kuongelea huruma ya Mungu, yaani katika Yesu jambo la huruma lilionyeshwa “kwa neno lake, matendo yake na kwa nafsi yake yote.” Yeye alitumia ishara nyingi za makaribisho, akithibitisha lengo la ujumbe wake na ukweli wa mafundisho yake. Kwa kweli, watozaushuru wengi, makahaba na wengine waliokataliwa na jamii, walijiona kukaribishwa na Yesu na tena kubadilishwa kwa sababu ya mkutano na huruma ya Mungu.

          Katika mfano wa mwana mpotevu, ingawa tuko na tukio la kijana mdogo na hisia za kijana mkubwa, macho yetu yamlenga baba wa vijana hawa wawili ndiye aliye mhusika mkuu wakati wote. Uhusiano wake wa mapendo kwa vijana wake, ambao wote ni wapotevu kwa njia tofauti ndio umuhimu wa tukio hili. Kulingana na Yesu, baba huyo ni kama Mungu ambaye ana watoto tofauti na kushiriki nao zawadi zake kwa njia sawa. Yeye anawapenda wote na kutaka watu wote wajione wakiwa katika familia, kushiriki kwa furaha yake kama Baba. Katika familia hii anautoa utunzaji na ulinzi ili wawe na maana nzuri ili kubaki naye daima. Wakati yeyote anapoamua kutenda kinyume naye na kubaki mbali sana naye, sio kwa maana mtu huyo hajihisi kupendwa, bali ni kwa sababu anajiona mwenye uhuru. Kama huu ni uzoefu wa upendo wa Baba: huu ni wa hiari na kuuzaa uhuru. Sisi pia tunahisi mbali sana na Mungu wakati sisi hutenda kinyume naye, yaani, tunapomkosea. Yeye anajihisi ameachwa na kusalitiwa, lakini haachi kutupenda. Kama yule baba, Mungu anashughulika sana na maisha yetu. Anakuja kututafuta ili kutupa sisi ulinzi na utunzaji wake. Kwa hivyo tunahisi majuto na kivutio cha kuishi tena uzoefu wa ushirika tumeopoteza. Ingawa mara nyingi tunakataa utambulisho wetu wa wana, kwa dhambi zetu, Mungu haukatai utambulisho wake wa Baba kamwe.

         Katika mfano huu yuko pia mwana mkubwa ambaye hajihisi mwana, kwa sababu anajiona kuwa ni mfanyakazi, wala hajihisi ndugu, kwa sababu anamkataa ndugu yake mdogo. Tabia ya huyo mwana mkubwa inaizuia furaha kamili ya Baba na ukamilifu wa sikukuu. Kumrudia Mungu ni maana ya furaha kubwa kwake. Lakini furaha yake haiwezekani kuwa kabisa ikiwa hatushiriki katika hisia zake kuhusu wengine. Hataki kwamba tuwe na wivu kuhusu njia yake ya kupenda; anataka kwamba tutende kama yeye alivyo. Kwa hivyo Yesu alisema, “Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo.” Upatanisho na wengine ni kipimo ili uhusiano wetu na Mungu uwe kweli. Hii ni njia ya kweli ya toba iliyo mwendo wa muda mrefu na huanza mioyoni mwetu. Kupitia Ekaristi hii, turuhusu kuguswa na huruma ya Mungu ili tuweze kuwa vyombo vya huruma hii kwa wale wanaohitaji msamaha wetu.

Fr Ndega 
Mapitio na marekebisho: Serah

domingo, 4 de setembro de 2016

KUMFUATA KRISTO KWA KUPANGA MAMBO YA KESHO


Kutafakari kuhusu Lk 14: 25-33

     Umati wa watu waliandamana na Yesu, lakini sio wote waliokubaliana naye. Alipoitambua hali ya kutokuwa na ahadi na makubaliano, aligeuka, akiwakazia macho na kuzungumza nao. Maneno yake yalikuwa nafasi ya kutafakari kwa kweli maana ya safari yao. Ingawa Yesu alikuwa maarufu, kwa sababu ya mambo mema kwa ajili ya watu, utume ambao Yesu alichukua kutimiza mapenzi ya Mungu hauleti umaarufu. Watu walichanganyikiwa kuhusu Yesu kwa sababu hawakumjua bado na kumfuata kwa njia yoyote. Kama Yesu hakuwa na nia ya kumdanganya yeyote, aliongea nao kwa uwazi sana kuhusu maana ya kumfuata na matokeo ya uamuzi huu. Kusema hivyo kulikuwa tabia yake ya kawaida kama alivyofanya kwa ajili ya wale kumi na wawili, yaani aliwajulisha masharti ili wawe wanafunzi wake wa kweli. Kutoka kwao, Yesu hakutarajia werevu ama upumbavu, bali kupatikana na hatia. Hawawezi kumfuata Yesu kwa sababu walipokea habari tu ya kuwa ni vizuri kufanya hivyo. Yesu anatarajia zaidi, mabadiliko ya ndani.

           Andiko hili ni mwaliko wa kuchukua ahadi ya kumfuata Kristo kwa kupanga mambo ya kesho, yaani kuwa na uwezo wa kuona mbele ili kutenda vizuri ama Kuwa na utoaji ili kuepuka kufaragua. Ni vizuri kuota ndoto lakini ndoto hii inapaswa kuihusu hali halisi mtu anayoishi, vinginevyo itakuwa udanganyifu tu. Yesu anataka kuepuka kwamba safari ya wafuasi wake iwe pasipo maana ama udanganyifu. Ni lazima utambuzi, hekima, kupanga na uamuzi. Mungu mwenyewe anatupa mfano wa kuwa na mipango ya muda mrefu ili tupate mafanikio katika safari yetu kama wafuasi wa Yesu. Yeye Mungu alipanga kumtuma mkombozi ndiyo maana miaka ilihesabiwa kwa kurudi nyuma maneno kabla ya Kristo (K.K) kuzaliwa yakitumika. “... wakati maalum ulipotimia, Mungu alimtuma Mwanawe aliyezaliwa na mwanamke... ili apate kuwakomboa waliokuwa chini ya sheria.” (Wagalatia 4: 4-5). “Hata baadhi ya wakulima hutegemea mvua inyeshe hata kama hawajaandaa shamba mahali pa kupanda mbegu kama za mahindi au maharagwe.” Kupanga mambo ya kesho ni muhimu.

         Yesu alisema, “Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” Kama ilivyotekea katika vifungu vingine, Yesu aliwapendekezea watu mpango wa maisha nao mpango huu unajumuisha kujinyima, kwa sababu yeyote anayekutana na Yesu kwa kweli amekwisha pata hazina ya kweli kwa maisha yake wala hawezi kubaki alivyo, yaani mambo mengine hayana maana tena. Kwa maneno mengine, Yesu anataka kuwa kipaumbele maishani mwa wanaoamua kumfuata. Hakuna jambo lingine ambalo liweze kuitoa maana ya kweli kwa maisha yao ila Yesu mwenyewe. Wanafunzi wa Yesu wa kweli walimtegemea Mungu katika mambo yote kama Yesu alivyo. Yeye alishiriki na wanafunzi wake ufalme wa mbinguni na kuwajulisha njia ya msalaba ili waweze kufanya mapenzi ya Baba yake. Kupitia njia hii, tunatambua kwamba Kumfuata Yesu hakuuleti upendeleo au hadhi, bali mateso na kujisalimisha kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Basi, yeyote ambaye anataka kuishi shwari na bila ahadi hawezi kumfuata Yesu. Tena yeyote ambaye anatamani kumfuata Kristo bila msalaba hatamfuata Yeye kwa kweli kamwe.

         Kupitia njia ya unyenyekevu na utupu Yesu alipata utukufu. Kupitia njia hii utambulisho wa wanafunzi na mwalimu Yesu unatokea. Kwa upande wa Kristo msalaba ulikuwa sehemu muhimu katika mwendo wa kufanya mapenzi ya Mungu na kudhihirisha mpango wa upendo wake. Kwa upande wetu kama wanafunzi, kuchukua msalaba ni ishara ya utayari wetu kwa kuruhusu kuongozwa na Mungu na kuyakaribisha mapenzi yake kwa maisha yetu. Kwa kufikia lengo hili tunapaswa kujikana nafsi yetu, yaani kujisahau sisi wenyewe ili wengine waweze kukumbukwe. Tunapaswa kujikana ili Mungu aweze kujifunua kwa nguvu yote ya upendo wake. Kujiondoka kutoka katikati/mahali muhimu ili wengine waweze kuwa na nafasi zaidi. Kwa maneno mengine, tunapaswa kuwafikiria wengine kuwa wamuhimu zaidi kuliko sisi wenyewe. Kama haiwezekani kumfuata Kristo bila msalaba, mfano wake wa uaminifu kwa mpango wa Mungu utuimarishe ili tuchukue msalaba wetu wa kila siku, kumfuata kwa uaminifu na kufanya mapenzi ya Mungu.

Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Serah