Kutafakari kuhusu Isaya 63: 16-17; 64: 1, 4-8; 1Wak 1, 3-9; Mk 13: 33-37
Kulingana na liturjia ya
Kanisa Katoliki, tunaanza wakati mpya uitwao Majilio. Wakati huu unajumuisha
wiki nne: wiki mbili za kwanza tunatafakari kuhusu kuja kwa Bwana mara ya pili
katika mwisho wa umri. Ujio wake kama Bwana wa maisha yetu na wa historia unalenga
kuimarisha matumaini yetu ili kushiriki katika furaha yake. Wiki mbili zingine
zinatukumbusha Ujio wa kwanza wa
Yesu na kutuandaa ili tusherehekee sikukuu ya kuzaliwa kwake katika Krismasi.
Masomo ya leo ndio mwaliko
wa kukesha
ili tutambue na kuzikaribisha ishara za uwepo wa Bwana katika hali yetu ya kila siku. Ndio mwaliko pia wa
shukrani maana Bwana anakuja kukutana nasi daima ili kutupa wokovu wake. Matukio yote makuu yahitaji maandalizi mema na ndani ili kusherehekewa mema. Hivyo ndivyo Majilio kama maandalizi ya tukio kuu la Krismasi.
Katika somo la kwanza, nabii Isaya anamwomba
Mungu kwa njia ya imani na upendo,
akimtambua kama Baba. Nabii huyo anaongea kwa kutambua
vipengele viwili: kwanza, uaminifu wa Mungu anayewaokoa watu
wake na kingine ni kosa la uaminifu wa watu kwa ajili ya Agano. Upinzani dhidi ya maongozi ya waliotumwa na Mungu uliwafanya watu wajione mbali na Mungu. Maombi
ya nabii ni faraja na msaada ili kufufua matumaini
katika Bwana ambaye yuko tayari kutoa nafasi mpya kwa yeyote anayetaka
kumrudia yeye. Tuchukue nafasi hii inayotupwa.
Katika somo la pili, Paulo
anamshukuru Mungu, kwa sababu ya
tendo la neema yake katika
jumuiya ya Wakorintho, ambayo imezaa
matunda mazuri kama jibu la tendo hili. Jumuiya hii inatarajia
ujio wa Bwana sio kwa njia yoyote bali kwa imani halisi iliyo
maonyesho ya ahadi yao kwa karama ilizopokea. Matakwa ya
Mtakatifu Paulo ni
kwamba jumuiya hii iendelee kwa imara katika ujumbe uliotolewa kuhusu Yesu na kukua kwa imani kwake anayeaminika.
Katika Injili Yesu anaongelea fumbo la
Kuja kwake. Ni sehemu ya mpango wa
hekima na wema wa Baba. Hii ni nafasi ya wokovu na sio ya hofu. Wokovu ni zawadi
ya Mungu; hakuna hata mmoja anayeustahili. Sote tunaalikwa kukesha. Yesu
analinganisha ujio wake na mfano wa mtu ambaye alifunga safari na kuikabidhi
nyumba yake kwa watumishi wake. Kila mmoja alipokea jukumu fulani na wote
waliombwa kukesha. Hapo ni muhimu kipengele cha wakati.
Kulingana na lugha ya Kigiriki wakati ndio Kronos na Kairos. Neno ambalo andiko hili linatumia ndilo Kairos linalomaanisha
wakati mwafaka, nafasi ambayo Bwana anatupa ili tuwe wenye furaha. Tunaalikwa
ni watumishi na katika biblia, watumishi ni wale waliotoa maisha yao kwa ajili
ya mpango wa Mungu. Bwana alitukabidhi mpango wake ili tuutekeleze maishani
mwetu na jamii yetu. Yeye anatarajia tutende jukumu hili kwa uaminifu kwa sababu
anataka kukutana nasi ili kutuzawadisha kwa kushiriki naye furaha yake.
Anatarajia kukaribishwa vizuri,
kulingana na maneno yake mwenyewe: "Mimi nasimama mlangoni na kubisha hodi. Mtu akisikia sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia nyumbani
kwake na kula chakula pamoja naye,
naye atakula pamoja nami” (Apocalypse 3, 20). Kulingana na andiko
hili Bwana Yesu atakuja usiku, yaani kama mwanga ili kufukuza giza, huzuni na
kuanzisha hali mpya kabisa maishani mwetu. Turuhusu kuangazwa na mwanga wake.
Kuja kwake Bwana badala ya
kuwaogopesha watu, kunayaimarisha matumaini katika wokovu wake, kwa sababu yeye ni Mwokozi na kuja ili kuokoa. Safari
ya Kikristo ni safari ya furaha ili kukutana naye kwa sababu yeye huja daima kukutana na sisi.
Maonyesho halisi ya makaribisho yetu kwa Bwana ndio utumishi wetu
katika jumuiya kwa ukarimu na furaha.
Hivyo, Majilio ni wakati wa kufanya upya ahadi yetu na
Bwana, katika mwendo wa mabadiliko daima. Kuhusu hili,
Bwana anatuambia tena: "Wewe unayo saburi,
umestahimili taabu nyingi kwa ajili ya jina langu, wala hukuvunjika moyo. Lakini ninalo jambo moja dhidi
yako: wewe hunipendi tena sasa kama pale
awali. Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukatubu na
kufanya kama ulivyofanya pale awali” (Ufu
2, 3-5a). Kusali zaidi na
kupatikana ni tabia za mwanafunzi wa
kweli anayejua Bwana wake naye uko tayari daima ili kumkaribisha.
Kukesha kwa uaminifu na ukarimu ni
ishara halisi ya matarajio yetu kwa ujio wa Bwana.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário