Tafakari kutoka Ezekieli
14: 11-12.15-17; 1Kor
15: 20-26.28; Mat
25: 31-46
Likiuhitimisha
Mwaka wa Kiliturujia, Kanisa linasherehekea Sherehe ya Bwana Wetu Yesu Kristo
Mfalme na kutukumbusha kwamba tamani lake ni tushiriki katika Ufalme wake. Maandiko
haya yaliyochaguliwa kwa siku hii yasema kwamba Mungu ni kama Mfalme-Mchungaji ambaye anawajali wana kondoo wake na kuwa na
upendo maalum hasa kwa ajili ya wasio na nguvu. Tabia yake ni kipimo cha
matendo yetu.
Kwa jina la Mungu, Nabii Ezekieli anawashutumu viongozi wa Watu wa Israeli kwa sababu tabia yao ya kutowajibika ilisababisha kipindi cha huzuni na mateso kwa watu hawa katika uhamisho wa Babeli. Lakini katika ujumbe wake, nabii anatangaza pia utunzaji wa Mungu kwa ajili ya watu hawa. Yeye atawaongoza kwenye hali mpya kama vile mchungaji kwa ajili wa wana kondoo wake. Kweli watu walikombolewa kutoka uhamisho. Lakini tukio hilo lilikuwa tangazo tu la kazi ya Yesu kama Mchungaji Mwema aliyesalimisha ili wanadamu wote wapate maisha mapya.
Kulingana
na Mtakatifu Paulo, Yesu amefufuka kama limbuko, yaani
kwa ajili ya kuwa wa kwanza wa wengi. Yeye alifungua kwetu mlango wa maisha
kamili na kweli. Alifanya hivyo akizishinda nguvu zote duniani, kupitia
kifo chake na ufufuo wake, akiwaokoa wanadamu na kuanzisha Ufalme wa Mungu Baba yake. Wanadamu wote wanaalikwa kuingia katika
ufalme huu. Lakini ni muungano na
Kristo ambao unatusaidia kufanya uzoefu wa ufalme huu.
Andiko hili ya Injili linajulikana kama “Hukumu ya
mwisho” na wengi kati yetu wanapendelea kumfikiria Yesu kama “hakimu” atakayekaa kitini chake akiwahukumu wanadamu, kuwatuza wengi na kuwaadhibu wengine
kama wafalme wa ulimwengu walivyo. Lakini hatuwezi
kusahau yale aliyosema, yaani “Mungu hakumtuma Mwana
ulimwenguni ili kuwa hakimu wake,
lakini kwa kuwa mkombozi wake” (Yohane 3, 17).
Hivyo, lengo lake sio kuhukumu bali kuokoa kwa sababu ya upendo na
huruma yake. Basi, inawezekanaje kufahamu andiko hili la Mathayo linaloongea
kuhusu hukumu?
Wainjilisti wanaonyesha kwamba Yesu alikataa cheo cha mfalme katika wakati wa utukufu, na
kukubali katika wakati
wa kushindwa, mfano msalaba. Upinzani
wake kwa cheo
hiki ulikuwa kwa sababu ya mawazo
ya kisiasa ya watu kuhusu suala hili. Yeye
anatumia mfano wa mfalme-mchungaji katika andiko hili ili kuelea maana kamili ya Ufalme wake na lengo lake kama Mfalme. kwanza kabisa, Ufalme wake sio kutoka ulimwengu huu wala haiwezekani kuuonwa na kusema ndipo
hapa au ndipo huko. Ufalme huu una tabia tofauti, yaani
haiwezekani kuonwa bali kuwepo.
Yesu hakufafanua Ufalme wa Mungu ni nini, lakini alisema
kwamba ndio kati yetu nasi
tunaalikwa kufanya uzoefu wa ufalme huu kwa kupitia matendo mema kwa
ajili ya wengine. Kweli ufalme unaonyeshwa na baadhi ya matendo letu, lakini
tuwe macho! Ufalme sio tendo tunalofanya bali ni tendo la Mungu katika maisha
yetu katika ulimwengu na katika historia. Yesu ndiye mfalme aliyekubali msalaba
kama kiti chake cha enzi alipoonyesha upendo wake kubwa kwa ulimwengu. Ndio Hukumu:
mfano wake wa kupenda na kuwa na huruma kama kipimo cha kutenda.
Mfalme
huyo anataka kuwakusanya watu wote kuzunguka naye katika
ufalme wake kama mchungaji anavyofanya kwa kundi lake. Yeye anajitambulisha na ndugu
wadogo na kuyaanzisha matendo ya upendo na huruma kwa
ajili yao kama kipimo cha wokovu. Aina ya mahusiano yetu
na wale walio na shida na wadogo inatuhukumu.
Sehemu ya
mwisho ya hukumu itakuja kwa wote nayo inapaswa kuwa ukamilifu wa maisha yetu
kwa sababu mambo yote ambayo tumeishi ndiyo maandalizi kwa wakati huu. Tutakapokutana
na Mungu, hatutaulizwa ikiwa tumeshiriki katika dini fulani wala mara ngapi
tulienda kanisani, bali kiasi gani tuliweza kupenda. Kwa hivyo tuko na ishara
za Kristo kwa ajili ya wadogo kama mfano. Mambo yote tunayoweza kufanya kwa
ajili yao ni kwa Kristo tunayofanya.
Hatuhitaji kuacha
ubinadamu wetu ili kukutana na Mungu. Yeye mwenyewe anajiruhusu kukuta katika ubinadamu
wetu, hasa wakati ubinadamu huu unateseka. Ndizo chaguo zetu zitakazoamua
mwelekeo wa maisha yetu. Tusisahau kwamba mapenzi ya Mungu ni kwamba maisha
yetu yapate ukamilifu na kwa hivyo anakaa ndani yetu kwa Roho wake. Tumpe nafasi
ya kutenda sababu, “Ikiwa Mungu yumo ndani yetu, tutafanya yale mema hata kwa
kupita kwetu tu”.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário