“Vijana,
imani na utambuzi wa wito”
UTANGULIZI
Mwongozo huu unalenga kutuimarisha ili kusoma
na kujifunza Waraka wa kimwisho wa Sinodi ya Maaskofu juu ya vijana ambayo yalifanyika
katika Roma kati ya siku ya 3 na ya 28 ya Oktoba. Mbele ya utajiri wa maudhui
haya, tunaweza kusema kwamba tuna mikononi mwetu kitu cha thamani kubwa, “kwanza
kwetu”, kulingana na Papa Francisco. Waraka huu imegawanywa katika sehemu 3,
sura 12, aya 167 na kurasa 60. Jambo ambalo linaongoza waraka mzima ndilo tukio
la Wanafunzi wa Emau.
SEHEMU I - «ALITEMBEA PAMOJA NAO»
I.
KANISA LINALOSIKILIZA
Kusikiliza
na kuona kwa huruma: Sinodi inasisitiza thamani ya
kusikiliza. Mambo yote huanza kutoka kusikiliza kwa huruma: vijana wanataka
kusikilizwa, kutambuliwa na kusindikizwa na wachungaji na walei wataalamu kwa
upatikanaji na uvumilivu.
Utofauti
wa mazingira na tamaduni: inaita makini yetu kuhusu ulimwengu
wingi na mabadiliko yake. Huu, kwa upande mmoja inawezesha maisha, lakini kwa upande
mwingine inazalisha kutengwa na kubaguliwa. Ni muhimu kurejea nguvu ya
imani.
Mtazamo
mmoja kuhusu Kanisa leo: sehemu hii inazungumza kuhusu
hamu ya elimu ya Kanisa ambalo linakusudia malezi kamili ya vijana. Shule na
vyuo vikuu vina jukumu lao, lakini parokia lazima pia kufikiri kwa njia mpya kazi
yake ya kiuchungaji ili iwe na kuvutia zaidi kwa vijana.
II. VIUNGO
MUHIMU TATU
Upya wa
mazingira tarakimu: hii ni hali ambayo imejienea, ndiyo
wavu wa fursa, lakini pia huleta pamoja nayo upande wa giza. Ni lazima tuingie
katika hali hii kukabili kwa ujasiri uhusiano kati ya imani na changamoto za
wakati huu wa sasa.
Wahamiaji
kama dhana ya wakati wetu: hilo ndilo jambo ambalo
linaonyeshwa kwa njia wingi. Wahamiaji wengi ni vijana wenye kasoro, waathirika
wa kila aina ya vurugu. Jukumu la kinabii la Kanisa limeelezwa na Papa Francisco
kwa kutumia vitenzi nne: “kukaribisha, kulinda, kukuza na kuunganisha”.
Kutambua
na kujibu dhidi ya kila aina ya matukano: kuchukua kwa
umakini ahadi na ukweli na kuomba msamaha. Kukabiliana na hali hii mbaya kwa
maamuzi ya ukali. Sinodi ilionyesha pia shukrani na kutia moyo kwa wale ambao
walikuwa na ujasiri wa kulaani hali hii.
III.
UTAMBULISHO NA MAHUSIANO
Familia
na mahusiano kati ya vizazi: inaongea juu ya familia
kama rejeo la kipendeleo, kwa kusisitiza jukumu la wazazi na uhusiano kati ya
vizazi. Lengo hapa ni kushirikiana imani na kusaidiana katika ushuhuda.
Mwili
na Affectivity: kipindi hiki kinatukumbusha mabadiliko
punde ambayo yaleta uhuru fulani juu ya mambo haya. Maadili wa kimwili wa
Kanisa inafikiriwa na watu wengi kama hukumu. Ni lazima kupendekeza kwa vijana anthropolojia
ya affectivity na sexuality ambayo iweze kutoa thamani kamili kwa usafi wa moyo
kwa ajili ya ukuaji wa mtu katika hatua zote za maisha. Kuhusu ushoga, ni
muhimu kuwasaidia vijana kuunganisha sehemu ya sexuality katika nafsi zao
wenyewe, kwa kuongezeka mahusiano mazuri na wengine kwa ajili ya kujitolea.
Aina za
kuwa na kasoro: hali hii inatokea mbele ya kosa la
kazi - ambalo linapunguza uwezo wa vijana wa kuota – mbele ya vurugu na mateso,
yanayosababisha kubaguliwa. Sinodi inapendekeza mabadiliko ya moyo na
mshikamano.
IV.
KUWA KIJANA LEO
Vipengele
vya utamaduni wa kijana punde: Inatuomba kuthamini shughuli
za michezo za vijana, ambazo zinaleta zenyewe uwezekano wa kielimu, wa kimalezi
na wa jumuisho. Hasa muziki inachukuliwa kama chombo cha nguvu ya kuinjilisha
na rasilimali kubwa ya kiuchungaji, kwa sababu inatoa vijana fursa ya kuonyesha
vipaji vyao.
Maisha
ya kiroho na ucha Mungu: vijana wanaja kutoka miktadha
ya kidini ya wingi na hii inadhihirisha utafiti mkubwa ya kidini. Wangependa
kukutana na Yesu Kristo, hasa kwa njia ya liturjia hai na kweli, ambayo uzuri
wa ishara, huduma ya kuhubiri na ushiriki wa jumuiya wasema kweli ya Mungu na hayo
yote yapendezwa nao sana.
Ushiriki
na Protagonism: vijana wanataka kuwa wahusika wakuu;
wanaomba waweze kuwa waamilifu katika uinjilishaji wa wenzao. Wanataka jumuiya
za kikanisa ziwe za kindugu na kweli zaidi ambapo wajihisi kuunganishwa, waweze
kuchukua majukumu na kuthaminiwa.
SEHEMU II - «MACHO YAO YALIFUNGULIWA»
Pentekoste
mpya: Roho Mtakatifu anafanya upya Kanisa na maisha ya
kila mwamini.
I.
KARAMA YA UJANA
Yesu
kijana miongoni mwa vijana: inaongea kuhusu ujana wa Yesu
kwa kuwaalika wote kuangalia yeye. inafikiria kwamba kutoka kuangalia kwake tu
inawezekana uzoefu kweli wa Mungu. Kutotulia kuzuri kwa vijana ni zawadi kubwa.
Hao ni “mahali pa kitheolojia”, yaani, mahali ambapo Mungu yupo na kutoka huko
anaongelea Kanisa na ulimwengu.
Kuwa
mtu mzima: inasisitiza umri wa ujana kama umri wa maamuzi.
Ni jukumu letu kuwasaidia vijana kuishi kuwepo yao iliongozwa na ishara ya
misheni kwa kutumia mafunzo ambayo yaweza kutoa changamoto na kuvutia. Tunapaswa
kuwapa maana ya kweli ya mamlaka na kuwasaidia kuanzisha mahusiano ya kifamilia
kwa njia ya kiinjili.
kuitwa kwa
uhuru: injili ambayo Kanisa linatangaza ni injili ya
uhuru. Kristo hafuti uhuru lakini anaikomboa, yaani, yeye anatoa uhuru wa kweli
na wa kijukumu, ambayo haiwezi kuishiwa bila undugu na mshikamano, hasa kwa
ajili ya walio wa mwisho wa jamii.
II.
FUMBO LA WITO
Utafiti
wa wito: dhana ya wito inahusiana na ile ya misheni.
Kila maisha ni wito nao unamhusu Mungu. Wito sio jambo binafsi ambalo mtu linasimamia
kwa uwezo wake peke yake. Kila wito wa kibatizo ni mwito wa utakatifu. Ni
muhimu kusaidia mazingira kwa ajili ya kuendeleza utamaduni wa kweli wa wito
katika jumuiya zote za Kikristo.
Wito wa
kumfuata Yesu: maisha ya Yesu bado yaendelea kuwa
msukumo na kuvutia siku hizi. Ndiyo rejeo ambalo linapendekeza changamoto kwa
vijana wote. Akidhihirisha fumbo la Baba na upendo wake, Yesu alifunua
kikamilifu mtu kwa nafsi yake mwenyewe na kuonyesha wito wake mkubwa sana.
Katika maana hii, Bikira Maria, mwanamke kijana, anatolewa kama mfano kwa
sababu ya uwezo wake wa kukaribisha mwito wa Mungu na kumsaidia kwa ajili ya mipango
yake.
Wito na
miito: wito na utume wa Kanisa ni kusaidia ushirika na
Mungu na miongoni mwa watu wote. Kwa ajili ya hali hii, yeye hutegemea namna
nyingi za karama zinazo maonyesho ya utambulisho wake na zawadi za neema ambazo
Roho hufufua daima Kanisani kwa ajili ya kulifanya upya. Kutoka ubatizo, sisi sote
tumeitwa kwa utakatifu kwa mantiki ya imani na kujitolea unaoonyeshwa katika
kila uamuzi wa maisha mtu anaofanya: ndoa, utawa, daraja, “single”, nk.
III.
UTUME WA KUANDAMANA
Kanisa linaloandamana: likifanya kazi yake ya mama, Kanisa huitwa kuwa karibu, kusaidia na
kuandamana na safari ya vijana kuelekea maamuzi ya kweli. Kuandamana ni kuumega
mkate pamoja na mahali pa kwanza pa mwendo huu ndiyo jumuiya yenyewe ambapo “wavu”
wa mahusiano unaweza kumsaidia mtu katika safari yake na kutoa njia ya
mwongozo. Kwa ajili ya utumishi huu, wanaitwa watu wote walio muhimu katika
hali mbalimbali ya maisha ya vijana. Hii inajumuisha pia kuingizwa katika
jamii.
Kuandamana
kwa kijumuiya, kwa kikundi na kwa kibinafsi:
kuandamana ni Misheni ya kufanyika sio kwa kibinafsi tu lakini pia kwa kikundi.
Katika kuandamana kwa njia ya kiroho, mtu anajifunza kutambua, kutafsiri na
kuchagua katika mtazamo wa imani, kusikiliza kile Roho analopendekeza ndani ya
maisha ya kila siku. Mwendo huu unaimarisha kutafuta sakramenti ya Upatanisho,
kwa kuchukua jukumu na kuukaribisha utofauti kama fursa ya ushirika wa kidugu
na ukuaji wa kubadilishana.
Walioandamana
wa ubora: shemasi Filipo anatolewa hapa kama mfano wa
kuigwa: yeye anapatikana kwa Roho, anapata njia ya kuingia kwa uhusiano, anafanya
maswali ambayo yasababisha uamuzi na kutoka nje ya tukio kwa unyenyekevu. Hivyo,
yule anayeandamana anapaswa kuwa mtu uwiano, anayesikiliza, anayeamini na kusali;
anajiona mtu wa udhaifu. Kwa sababu hii, anajua jinsi ya kukaribisha na
kusahihisha kwa njia ya kindugu, bila tabia ya kuwamiliki wala kuwadanganywa watu. Ni muhimu
kutafuta malezi maalum kwa ajili ya utumishi huu.
IV.
SANAA YA KUTAMBUA
Kanisa,
mazingira kwa ajili ya kutambua: kutambua ni mwendo wa
kiroho ambao mtu, kikundi au jumuiya hutafuta kutambua na kukubali mapenzi ya
Mungu katika halisi ya hali yake mwenyewe. Katika historia ya Kanisa, mwendo
huu umekuwa na maana mbalimbali lakini mambo mengi ni sawa kati yao. Utambuzi
hauwezi kupunguzwa kuwa mwelekeo binafsi peke yake bali ni jambo ambalo
linajumuisha jumuiya nzima ambayo kwa nuru ya Neno yasikiliza lile Roho analopendekeza
kupitia uzoefu wa kiroho wa wanashiriki wake.
Dhamiri
katika mwendo wa utambuzi: dhamiri ni mahali maalum pa uhusiano na Mungu, ambamo sauti yake ndimo.
Hii haimaanishi “kujitambua”, lakini inathibitisha uwepo wa kimungu. Malezi ya dhamiri
ni kazi ya maisha yote na kuhitaji utunzaji wa ndani: ukimya, sala, sherehe ya
sakramenti, mafundisho ya Kanisa na matendo mema.
Mazoezi
ya utambuzi: utambuzi unafahamika kama kazi ya dhamiri
na njia ya kweli ya sala. Kwa kila mtu ambaye anaanza mwendo huu inahitajika
uhusiano wa ndani na Bwana, mkutano mara kwa mara na mtu wa uongozi wa kiroho,
sherehe ya sakramenti, tamaa ya moyo ya kusikiliza sauti ya Roho na nia ya
kuweka utaratibu katika maisha yake mwenyewe. Jukumu la uamuzi huu huthibitishwa
na uzoefu wa kindugu na utumishi kwa maskini.
SEHEMU III - «AKAONDOKA BILA KUCHELEWA»
Kanisa
kijana: picha ya Kanisa kijana tunaloota ndiye Maria Magdalena,
ambaye akiishi upendo maalum kwa ajili ya Bwana, alienda kukutana na wanafunzi
wengine na kusababisha harakati yao kwenye Yesu. Hivyo, Kanisa anataka kufikia
vijana wote, kutembea pamoja nao na kupitia yao, kusikiliza sauti ya Bwana anayetuomba
mabadiliko ya moyo na kufanya upya miundo. Vijana wote, bila kuacha hata mmoja,
ndimo moyoni mwa Mungu na tena moyoni mwa Kanisa.
I. “SYNODALITY”
YA KIMISIONARI YA KANISA
Mabadiliko
daima: vijana wanaomba wote watembee pamoja katika mwendo
wa “kisinodi” daima. Kutoka Mkutano Mkuu huu na kutoka Waraka wa tukio hili, Mabaraza
ya Maaskofu na Majimbo ya Kanisa yaalikwa kuendelea mwendo wa utambuzi kwa njia
ya kishiriki na ya jukumu la kindugu kwa ajili ya kufafanua suluhu maalum za kiuchungaji.
Njia kwa
ajili ya utume: “sinodi” ni njia kwa ajili ya misheni ambayo
inaomba tupite kutoka “mimi” kwa “sisi”, kwa kuzingatia nyuso mbalimbali,
hisia, asili na tamaduni. Inahitajika kuthamini karama nyingi mbalimbali ambazo
Roho huwapa wote kwa kuepuka clericalism
na kuishi mamlaka kama utumishi. Ni lazima iwe njia ya “sinodi” pia mazungumzo
ya kiekumeni na ya kidini: kuwa na parresia
kwa kuongea na unyenyekevu kwa kusikiliza.
II.
KUTEMBEA PAMOJA KATIKA MAISHA YA KILA SIKU
Kutoka
miundo kwa mahusiano: haja ya kutembea pamoja inahusu
sio tu Kanisa kwa ujumla, lakini juu ya yote kila jumuiya moja. Hii inamaanisha
kupita kutoka mantiki ya kumngoja mtu fulani afanye kitu kwa kufanya pamoja.
Tunapaswa kufikiri upya kazi ya kiuchungaji ya parokia na miundo yake ambamo yatokee
mahusiano ya kweli kwa ajili ya kusaidia uzoefu maalum maishani mwa vijana.
Maisha
ya jumuiya: jumuiya zetu zinaonyesha alama ya
utofauti, mozaiki ya nyuso nyingi. Hii inaruhusu vijana waingizi katika maisha
ya kijamii, kwa kuleta furaha ya injili. Katika tangazo na katekesi ni muhimu
kufanya upya ahadi kwa ajili ya lugha na mbinu, lakini bila kusahau muhimu sana:
mkutano na Bwana, kupitia uzoefu wa kiliturujia ambayo vijana wanakua katika hisia
ya Diakonia, kwa kutafuta kujitolea
na utumishi njia ya kukutana na Bwana.
Kazi
kwa ajili ya Vijana inayolenga wito: Kanisa linaitwa
kuwa nyumba kwa ajili ya vijana, ambapo mtu anaishi hali ya familia kupitia imani
na amini. Kama wito ni kiini ambapo mambo yote ya mtu ni yajumuisha, ndio
kupitia hali ya wito ambapo uchungaji wote unapata msingi wa muunganisho. Kwa
sababu hii kazi ya kiuchungaji nzima ya Kanisa ifanyike kwa kulenga wito, hasa ile
ya vijana.
III.
MSUKUMO MPYA WA KIMISIONARI
Changamoto kuchukuliwa: mazingira ya kitarakimu – kujaza na injili tamaduni na mienendo
yake; wahamiaji – kuwakaribisha, kuwalinda,
kuwasaidia na kuwaunganisha; wanawake
katika Kanisa – mabadiliko ya kijasiri ya mawazo ya kitamaduni na
mabadiliko katika kazi ya kiuchungaji; sexuality
– kupendekeza kwa vijana anthropolojia ambayo itoe thamani kamili kwa usafi
wa moyo kwa kuwasaidia kuunganisha hali ya sexuality katika nafsi zao wenyewe;
kuhusu uchumi, siasa, kazi – kusaidia
na kuandamana ushirikiano wa vijana katika dunia hii ya kazi; Miktadha kati ya tamaduni, tena kati ya dini
mbalimbali na mazungumzo ya kiekumeni - vijana Wakristo wanaitwa kuwa wamoja,
kwa kujifungua pia kwa vijana wa mila nyingine na kushika nao mazungumzo ya
kweli ambayo yalenge kuheshimiana na kuponya kutoka chuki na ubaguzi.
IV. ELIMU
KAMILI
Katika ulimwengu ambapo kila kitu ni
kushikamana, inahitajika njia mpya ya mtazamo wa malezi ambao unaweza kuziunganisha
hali tofauti za mtu. Uwepo wetu katika shule na vyuo vikuu unapaswa kuwa na
maana kwa kulenga mtazamo wa malezi kamili ya vijana. Ni muhimu kuthamini
uzoefu wa kimisheni wa vijana kwa kuwekeza kwa ukarimu hamu ya kielimu, wakati wa
muda mrefu na pia rasilimali za kiuchumi. Mwishowe, Sinodi iliandaliwa
mapendekezo matatu ili kuusukuma upya: kufanya nyakati ya malezi ya walei, watawa
na mapadre pamoja; kujumuisha katika maandalizi ya upadre ama maisha ya Utawa
maandalizi maalum kuhusu kazi ya kiuchungaji kwa ajili ya vijana; ndani ya mwendo
wa utambuzi kuwa safari ya kimalezi kupitia uzoefu wa kijumuiya.
HITIMISHO
Sinodi inatukumbusha kwamba sisi wote tumeitwa
kuwa watakatifu na kupitia wito huu mmoja tu inawezekana kuendeleza aina
tofauti za maisha. Vijana wanahitaji watakatifu wanaozalisha watakatifu
wengine, hivyo inaonyeshwa kwamba “utakatifu ni uso mzuri sana wa Kanisa.” Hata
vijana wanaweza kutufundisha mengi kuhusu huu. Kupitia utakatifu wa vijana,
Kanisa linaweza kufanya upya hamu yake ya kiroho na nguvu yake ya kitume.
Vijana wanatufanya kurudi kwa upendo wetu wa kwanza.
Fr Ndega