Kutafakari kuhusu Yoh 6,
44-51
Ili tupate uelewa mzuri kuhusu andiko hili
hatuwezi kusahau yale aliyosema Mtakatifu Geronimo: “Yule anayepuuza Maandiko
Matakatifu anayepuuza nguvu na hekima ya Mungu. Kuyatojua Maandiko ni kumtojua
Kristo.” Katika kifungu kingine anasema kwamba “Neno la Mungu ni mkate wa
Kristo, nyama ya Kondoo, mwili wake na damu yake”. Hivyo, tunafahamu kwamba
tunaweza kutumia andiko la leo kwa ajili ya Ekaristia lakini tena kwa ajili ya
Neno la Mungu lililo mkate ulioshuka mbinguni. Tuko na uhusiano wa ndani kati
ya Ekaristi na Neno: tunala na kushiba neno lilifanyika mwili (Yoh 1, 14).”
Yesu anaongea na wenzake wa Galilaya katika sinagogi ya Kafarnao naye
ndiye maana ya kashfa kama ilivyotokea katika Nazareth. Yeye ndiye Mungu wa
kawaida anayehusika kwa hali ya kibinadamu hata kusababisha kashfa. “Wayahudi
hawakiri mtu awe na uwezo hali ya kimungu (kushuka kutoka mbinguni) na asili ya
kibinadamu ya Yesu ambayo wote walijulikana, haijumuishi asili ya kimungu
yoyote. Labda, Yesu alikosa akikubali kuishi kama watu wa kawaida?
Wakati yeye anasema: “mimi ndiye mkate
ulioshuka kutoka mbinguni”, anaongelea hali yake kama Neno milele la Mungu
ambalo lilifanyika mwili katika hali ya kibinadamu likiipandishia hali hii na
kuizalisha hali mpya. “matumizi ya mkate ama chakula kama mifano yajulikana
katika Maandiko. Manabii watumia kwa ajili ya Neno la Mungu (Am 8, 11; Is 55,
1-11). Maandiko ya Hekima yatumia kwa kuongelea Hekima ama akili (Meth 9, 1-6; Ben
Sir 15, 3; 24, 18.21-22).” Yesu ndiye Hekima ya Mungu ambaye ufunuo wa biblia
unaongea kama kuwa ni mtu (Yoh 1, 1s).
Yeye anajifunua kwa wasikilizaji wake kama
chakula kilichoshuka kutoka mbinguni si kwa binadamu tu bali kwa ajili ya uzima
wa ulimwengu mzima. Tukumbuke maneno haya, yaani, “Kwa maana jinsi hii Mungu
aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila mtu amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa milele (Jo 3, 16)”. Mwana anajitoa kama chakula
kinachodumu hadi uzima wa milele kwa sababu ya mapenzi ya Baba aliye uhai na kusababisha
uzima ndani ya kila mtu anayempokea Mwanawe. Maneno haya ni umuhimu katika
mafundisho ya Yesu kama mwokozi na mkombozi wa dunia. Anatuokoa kwa kujitolea
mwenyewe.
Tafakari yetu ni pia kuhusu Ekaristi takatifu
iliyo uwepo hai na kweli wa Yesu miongoni mwetu. Yeye anasema kwamba twamwendea
yeye kwa sababu tunavutwa na Baba na tena kumwamini yeye ni kipimo ili tuwe na uzima
wa milele ulio uzoefu wa kufufuka katika siku ya mwisho. Uzoefu huu ni
ukamilifu wa ushirika wetu na Mungu, aliye chemchemi ya uhai na furaha milele.
Fumbo la kazi ya Kristo linasisitiza kwamba yeye alikufa kwa sababu hakutaka
kuwaacha wafuasi wake na kufufuka ili abaki pamoja nasi, kutulisha kwa mwili
wake na kutuonyesha njia ya uzima wa
milele. Kwa maneno mengine anataka tuishi kutokana na mfano wake.
Yesu anaongea kuhusu uzima bila mwisho na
kwamba uko kwa watu wote. Huu ni maonyesho ya kujisalimisha kwake kwa hiari,
kuendeleza uwepo wake miongoni mwa wanadamu na kufundisha njia ya utimizaji kabisa.
Hiyo ni Ekaristi kama zawadi kubwa ya Mungu ambaye hataki kubaki mbali na
binadamu. Ekaristi ni hazina ya kanisa, uwepo maalum ya mume wake na alama ya
uzoefu wake wa kiroho kama mke wa mume aliye Kristu. Linaishi kwa sababu ya
Kristu. Vivyo hivyo ni kwa wote ambao wanashiriki mkate mmoja na kikombe
kimoja. Kupitia Ekaristi Yesu anatuingiza na kutuchukua kwake ili tuishi naye.
Yeye anakaa ndani yetu nasi ndani yake. Anatuunganisha naye, kutuhusisha katika
ushirika sawa kati yake na Baba. Bila shaka kwamba matokeo ni pia undugu wenye
nguvu na mwafaka miongoni mwetu. Yesu anashughulika na hali ya wanadamu wasio
na chakula na kutualika kushiriki katika hisia zake tunapopokea Ekaristi.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário