Kutafakari kutoka su Mit 9,
1-6; Waef 5, 15-20; Yoh 6, 51-58
Yesu ndiye
chakula ambacho Mungu alitupa na kuendelea kutupa ili tuwe na maisha kamili. Kutoka
Umwilisho wa Neno mpaka msalaba na Ufufuko, maisha ya Yesu yalikuwa kujitolea
daima kama chakula cha Mungu kwa ajili ya maisha ya watu wake. Ekaristi
takatifu tunayosherehekea inatuhakikishia kwamba ukarimu wa Mungu haumaliziki,
kweli utaendelea hata milele. Kila siku Kristo hufanya upya ishara yake ya
upendo kwa ajili ya wokovu wetu. Yeye mwenyewe anatualika kwa karamu ya uzima,
anajitoa kama chakula na kututumikia kama yule ya pekee ambaye anaweza kujaza
moyo wetu unaomtamani Mungu na uhai wake sawa. Lengo la Ekaristi ni kufananisha
maisha yetu kidogo kidogo kulingana na maisha ya Yule tunayepokea.
Andiko la kwanza
linaongea kwamba hekima ya Mungu imewakaribia wanadamu ili kuingizwa nao. Mwenye
hekima ni yule anayekaribisha hekima hii na kuishi kulingana na msukumo wake. Kwa
hekima ya kimungu tuko na nafasi kamili, chakula kamili ili tubadilishe mawazo
yetu na kutembea kuelekea kwake. Hekima hii ndiye Mwana aliyefanyika mwili na
kujitoa ili tumle kwa ajili ya kuishi kama wenye hekima sio wajinga, kulingana
na yale anayosema Mtakatifu Paulo katika andiko la pili. Mapenzi ya Bwana ni
tuweze kutumia vizuri wakati ambao tumepewa tukitafuta kula hii “Hekima
iliyofanyika mwili” kwa ajili yetu ili tuishi kwa sababu yake.
Katika injili
Kristo aliwaalika wasikilizaji wake kuukaribisha ufunuo juu ya utambulisho wake
kama chakula kilichoshuka kutoka mbinguni si kwa binadamu tu bali kwa ajili ya
uhai wa ulimwengu wote. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata
alimtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uhai wa
milele (Jo 3, 16)”. Mwana anajitoa kama chakula kinachodumu hadi uzima wa
milele kwa sababu ya mapenzi ya Baba aliye chemchemi ya uzima. Yeye ndiye
anayesababisha uzima ndani ya kila mtu anayempokea Mwanawe. Tunaongea hapa
kuhusu kiini cha mafundisho ya Yesu kama mwokozi na mkombozi wa ulimwengu,
lakini wasikilizaji wa Yesu hawakuweza kuelewa kwa sababu walijua hali ya Yesu
ya kibinadamu. Kweli alikuwa na ugumu wa kukubali kwamba mwenzao huyu alishuka
mbinguni wala kuwa chakula kwao. Lakini ugumu wao haukumzuia Yesu ya kufunua
njia iliyojaa maana kwa maisha yao.
Yesu anaongea
kuhusu uzima bila mwisho unaopatikana kwa wote. Inawezekana kuupokea uzima huu
kwa kuula mwili wake na kuinywa damu yake, kwa sababu yeye ndiye uhai na huishi
ndani ya wale wanaompokea. Yesu anatenda ishara hii ya upendo kwa uhuru kabisa
na kulenga kukaa miongoni mwa wanadamu na ndani ya kila mtu. Hiki ndicho kipimo
cha kupata uzima. Hilo ndilo fumbo la Ekaristi takatifu. Ndiyo zawadi kutoka
kwa Mungu ambaye hataki kuishi mbali na binadamu. Ekaristi ni hazina ya kanisa
na kiini cha uzoefu wake. Ekaristi inalifanya Kanisa na Kanisa linaishi kwa
Ekaristi. Kulingana na Mtaguso Mkuu wa Vatikano wa pili, “matendo yote ya
Kanisa yatoka kwa Ekaristi na kulenga Ekaristi”. Ndivyo hivyo kwa sisi sote
tunaoumega mkate mmoja na kunywa kikombe kimoja. Uzoefu huu ni ukamilifu wa
ushirika wetu na Mungu na msukumo kwa ahadi yetu ya kindugu.
“Tunapokula
chakula cha kawaida mwili wetu unaingiza chakula hiki ili uwe na afya nzuri.
Hivyo, chakula kinaingizwa na mwili wetu. Kuhusu Ekaristi, chakula cha uzima,
matokeo ni tofauti: wakati tunampokea Yesu, ni sisi tunaoingizwa naye”. Kwa
maneno mengine, Yesu anatuingiza, anatuchukua kwake ili tuishi naye na kwa
sababu yake. Yeye anakaa ndani yetu nasi ndani yake. Yeye anatuunganisha naye,
kutuhusisha katika ushirika sawa anaoishi na Baba. Katika uzoefu huu
tunabadilika kuwa yule tunayempokea kwa ajili ya ukuaji wa mwili mmoja. Hivyo,
wakati tunaposherehekea Ekaristi kwa kina mahusiano kati yetu yabadilika na
sisi tunakuwa vyombo vya umoja, upatanisho na amani kulingana na hisia za
Kristo.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário