Kutafakari kuhusu Kut 16: 2-4, 12-15; Waef. 4: 17, 20-24; Yoh. 6: 24-35
Ingawa wana wa
Israeli walikuwa watumwa katika Misri, wakawa na vyakula vingi hata washibe.
Walipoacha utumwa kwa nguvu ya Mungu, wakapata utambulisho mpya kama Watu wenye
uhuru. Utambulisho huu mpya ulileta baadhi ya changamoto kama kuishi jangwani, kuwa
na chakula kidogo ama kutokuwa na chakula, kutokuwa na maji, utekaji wa watu
wengine, na kadhalika. Kwa hivyo, walikuwa na mwelekeo wa kulalamika. Lakini, katika
mazingira haya magumu Waisraeli hawakuwa peke yao, kwa sababu Mungu aliyewakomboa
aliendelea kuandamana nao maana yeye ndiye mwaminifu kwa ahadi zake. Aliwalisha
kwa mana sio kwa sababu ya malalamiko yao tu bali hasa kwa maana yeye ndiye
macho kwa mahitaji ya watu wake hata kabla ya kumwombe kitu. Hakika walikuwa na
ugumu wa kuelewa ufundishaji wa kimungu. Akitoa mana, Mungu aliwaonyesha upendo
na utunzaji wake na kutangaza zawadi kubwa zaidi itakayotimizwa na Mwana wake
aliye “Mana ya kweli”.
Mt. Paulo
anafanya tofauti wazi kati ya maisha ya mtu kabla ya ubatizo na ya kutoka
ubatizo. Kabla ya ubatizo mtu huishi kama mtumwa kwa maisha ya zamani na njia
ya ubatili. Kupitia ubatizo mtu anabadilishwa kabisa kwa kupokea maisha mapya
katika Kristo, yamejaa maana. Ndiyo hali ya ubatizo wetu. Mbele ya jaribio ya
kuishi kama kabla ya utambulisho huu, tunasaidiwa na neema ya Mungu ili kufananisha
maisha yetu kulingana na njia ya kuishi ya Mwanawe aliyeweza kutoa maana
ulimwenguni kwa kujitolea kwake.
Yesu alitenda
ishara kubwa ya kuzidisha mikate na samaki kwa ajili ya kuwalisha watu,
akiwaonyesha hisia mbele ya mahitaji yao. Baada ya kula hata kushiba watu
walitaka kumfanya Yesu mfalme wao. Kulingana na mawazo ya jamii matokeo hayo ni
ishara ya mafanikio ya kazi na njia kamili ya mtu ambaye anakuwa maarufu.
Lakini Yeye akijua mpango wao alitoroka akienda mlimani peke yake. Kisha watu
walimtafuta na walimkuta na wanafunzi wake katika Kapernaumu. Kulingana na Yesu
hawakufahamu ishara na hawakuwa na nia kamili ya kumtafuta. Hatimaye,
aliwaalika kumkubali yeye kama mkate wa kweli kutoka kwa Mungu ambaye anautoa
uzima kwa ulimwengu. Yeyote ambaye anakuja kwake na kumwamini yeye hataona njaa
na kiu kamwe.
Yesu alikuwa na
hisia mbele ya mahitaji ya watu na kujaribu kuutoa mwelekeo mpya kwa maisha yao
kupitia uzoefu wa huruma na kushirikiana, lakini maana ya tumbo lao, wakawa kama
“vipofu” na bila uwezo ili kuelewa maana ya ishara. Hawakupata mafanikio katika
kumtafuta Yesu kwa sababu ya kosa la maana kamili. Kweli nia ya Yesu akiwalisha
watu ilikuwa kuonyesha hisia yake na kuwaandaa kwa mafundisho yake kuhusu mkate
tofauti na kweli. Yeye anatoa chakula kinachodumu mpaka uzima wa milele ambacho
ndiye yeye mwenyewe. Anadhihirisha pia kwamba siyo Musa ambaye aliwapa watu
mana, lakini ndiye Mungu. Mana ni mfano tu wa zawadi kubwa iliyo Mwana wake
ambaye Mungu alimtoa kwa uzima wa ulimwengu. Kweli “zamani, Mungu alitoa mana,
leo hii Yesu mwenyewe amejifanya mkate, chakula chetu na chemchemi ya uzima.”
Basi, chakula
hiki ndicho Ekaristi takatifu iliyo ishara kubwa ya upendo wa Mungu na
maonyesho ya kujitolea kwake Kristo kwa hiari. Maadhimisho ya Ekaristi ni
ufanisi maishani mwetu ikiwa tunasherehekea kama maonyesho ya upendo. Wale tu
wanaopenda kweli wanaweza kujitolea kwa ajili ya wengine kama Kristo alivyo.
Upendo tu unazaa ushirika na “vitu tu vinavyofanyika kwa upendo vinadumu”.
Kupitia Ekaristi tunabadilishwa kabisa kuwa kama Yule tunayeadhimisha kwa
kukubali ahadi ya kuishi maisha mapya yaliyo matokeo ya mkutano naye. Hivyo, baada
ya kila maadhimisho ya Ekaristi tunapewa changamoto ya kurudia shughuli za kila
siku kama mashahidi wa Yule ambaye anayatoa maisha yake kwa upendo ili watu
wote wawe na uzima wa milele.
Kupitia Neno la
Mwanawe na kujitoa kwake katika Ekaristi, Mungu anaendelea kuwalisha watu wake
na kuwaonyesha upendo na utunzaji wake. “Yesu ni mkate unaotushibisha, maji
yatulizayo kiu yetu, ni Yesu pekee awezaye kutuliza hamu ya mioyo yetu” inayotamani
milele. Tunapaswa kujiuliza daima ikiwa tunamtafuta Yesu na nia hii ama na
mvuto wowote. Hatuwezi kupata mafanikio katika kumtafuta Yesu ikiwa lengo letu
ndilo kumkawisha katika uhusiano umefungwa ili atumikie mivuto yetu ya ubinafsi
bali tunapaswa kumtafuta kwa ajili ya kumjua nzuri na kumpeleka kwa wengine.
Kulingana na Papa Francisco, “furaha ya mkutano yetu na Bwana haitakuwa kamili
ikiwa hatuishiriki na wengine”. Tunaalikwa kuongoza kutafuta kwetu kuhusu Yesu
kulingana na mawazo yake yaliyo mawazo ya kujitolea, ya ukarimu na ya upendo.
Basi, tuendeni kukutana na Yesu ili kujifunza kutoka kwake jinsi ya kujifanya
“chakula” kwa ajili ya wengine.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário