Kutafakari
kuhusu Kutoka 24: 3-8; Ebr 9: 11-15; Mk 14: 12-16, 22-26
Siku ya leo tunaalikwa kuadhimisha sikukuu ya Mwili
na Damu ya Kristo, lililo fumbo la imani yetu. Hii ni nafasi maalum kuonyesha
shukrani yetu na upendo wetu kwa zawadi kuu ya Ekaristi takatifu. Hii ni siku
ya kutafakari kuhusu uwepo wa kweli wa Kristo katika ishara za mkate na divai. Ekaristi
takatifu ni fumbo la kujisalimisha kwake kwa upendo kwa wokovu wa ulimwengu. Ekaristi
ni adhimisho la fumbo la Mungu ambaye anawatumikia watu wake, yupo karibu nasi
na ndani yetu. Hilo ni fumbo la ushirika ambao tunahusishwa kama washirika
katika uhai wake. Ekaristi ni sakramenti ya Agano jipya na milele kupitia hilo Kristo
anatuunganisha naye na miongoni mwetu wenyewe kama wana wa watu wapya wa Mungu
lililo Kanisa.
Masomo ya leo yanaongea kuhusu hali hii. Kulingana
na somo la kwanza, agano ambalo Mungu alianzisha na watu wake lina kama msingi
Neno lake ambalo watu alikubali kama mwongozo ili waweze kuishi kulingana na
matarajio yake Mungu. Katika mwendo huu ni muhimu uwepo wa Musa kama mpatanishi
mwema ili maneno ya Mungu yatangazwe kwa watu kikamilifu. Damu ya wanyama waliotoa
kwa Mungu ikanyunyizwa juu ya watu ikithibitisha ahadi kati ya Mungu na watu
wake. Somo la pili
linaongea kwamba Kristo ndiye mpatanishi wa kipekee wa agano jipya na milele.
Ukuhani wake ni mkubwa kuliko
ukuhani wa agano la kale kwa sababu una asili ya Mungu. Yeye hakuhitaji kumtolea
Mungu damu ya sadaka ambayo inatoka kwa wanyama, bali alijitoa kama sadaka
kamili na kupitia damu yake wanadamu wote walipata wokovu.
Injili inasimulia tukio la Karamu ambayo Yesu akitumia
ibada ya Wayahudi, alianzisha Ekaristi takatifu. Fumbo
la usiku ule lilifunua hamu ya kiini ya moyo wa Yesu. Kweli Yeye alitaka
kusherehekea pasaka na wanafunzi wake kwa sababu alikuwa na jambo muhimu la mwisho
la kudhihirisha kwao. Aliwapa
mafundisho yake ya mwisho akiwaalika kubaki kuungana naye kwa ajili ya
mafanikio ya kazi yao: “Bila mimi hamwezi kufanya chochote”. Basi, kwa kutarajia, akihisi mwenye uhuru kabisa kwa kujitolea mwenyewe kwa
ajili ya wale ambao aliwapenda mpaka upeo, "alitwaa mkate na kikombe,
akashukuru, akawapa, akasema: twaeni huu ndio mwili wangu na hii ndiyo damu
yangu. Vitendo hivi vya Yesu na wanafunzi wake vilivyofanyika katika hali ya
kifamilia na amini ya kubadilishana kama mwaliko wa kuchukua ahadi pamoja.
Mkataba kati ya Mungu na watu wake katika agano la
Sinai ulikuta maana yake kamili na Yesu ambaye alifanya mkataba mpya, akianzisha
Agano jipya kati ya Mungu na Watu wake wapya. Akitumia Ibada ya Wayahudi, Yesu alianzisha Ibada mpya, yaani
Mlo wa Ekaristi, akitangaza kwa Wafuasi wake ukombozi kamili ambao ulikuwa
ukija na kwamba alitamani kwa shauku kushiriki na marafiki zake. Katika karamu
hii ya mwisho, Yesu alijitoa kama chakula na kinywaji, akionyesha maana ya
kujisalimisha kwake kwa hiari msalabani. Kujisalimisha kwake kwa upendo na
hiari kunakuwa tabia kamili na sharti kwa yeyote anayetaka kumfuata. Wanafunzi
wake wakati watakaposherehekea Kuumega Mkate wataendelea mwendo huu kama
ushiriki katika kujisalimisha kwa mwalimu Yesu wakipokea nguvu ili kujitolea wenyewe
kama yeye alivyo.
Huu
ndio msingi wa misa takatifu yote. Hili ni maana ya imani yetu. Tunaalikwa
kuadhimisha fumbo la Mwili na Damu ya Kristo kwa upendo na ahadi sawa Kristo
alikuwa nayo aliposherehekea pamoja na wanafunzi wake. Yeye alianzisha Ekaristi
akiutoa mwili na damu yake katika ibada, akiandaa wanafunzi wake kwa
kujisalimisha kwake msalabani. Katika sakramenti hii Kanisa linaukuta
utambulisho wake wa kweli kwa sababu linafanya upya ahadi yake na Yule aliye
kichwa chake. Katika kila Ekaristi takatifu Kanisa linahisi moja na Kristo ili kuleta
uzima wake duniani kote. Hii ndiyo Sakramenti inayolifanya Kanisa; hii ndiyo msingi
na lengo la kazi yake.
Katika Ekaristi uwepo wa
Yesu ni hai na ufanisi. Yeye mwenyewe katika kila maadhimisho ya Ekaristi anatufanya
kuona mabadiliko ambayo tunahitaji ili kuwa mashahidi wenye furaha wa ufufuko
wake. Tunapoadhimisha Ekaristi tunabadilishwa kuwa kama Yule ambaye tunamsherekea
kwa kukubali ukweli wa Fumbo hili kama “Pasaka ya Kristo katika pasaka yetu na
pasaka yetu katika Pasaka ya Kristo”. Hivyo, baada ya kila adhimisho ya
Ekaristi tuna changamoto ya kurudia shughuli za kila siku kama mashahidi wa
Kristo anayetoa maisha yake kwa upendo ili wote wawe na maisha kamili. Basi, tumshukuru
Mungu kwa uzoefu wa udugu tunaoishi katika kila misa takatifu tunayoadhimisha. Neema
yake itusaidie kuishi uhusiano wa ndani na Yesu ili maisha yetu yawe kama vile
yake, ‘ekaristi’ ili kulisha ulimwengu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário