Kum 4, 32-34.39-40; War 8, 14-17; Mt 28, 16-20
Tunaalikwa
kutafakari kuhusu fumbo la Utatu Mtakatifu. Utatu Mtakatifu ni fumbo la Mungu
aliye ushirika wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Yeye yu ushirika wa upendo
kwa maana Mungu ni upendo. Upendo ni tabia ya Mungu. Hivyo, “Mungu ni Utatu kwa
sababu ndiye upendo” (L. C. Susin). Mungu yu wa kipekee lakini haishi peke yake
kwa sababu alitaka kuwa na kuishi kwa ushirika. Uumbaji wote ni uenezi wa nafsi
na wa fumbo lake. Viumbe vyote vinaitwa kuingia katika mwendo huu wa upendo na
kuwa maonyesho ya wema wake. Tumsifu Mungu kwa ushirika wake wa upendo,
atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu...
Tunapofanya
ishara ya msalaba, yaani, “Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu”,
tunaonyesha hisia yetu ya kuwa miliki ya Mungu na tena tunaongea kuhusu ukweli
wa Mungu, ambaye yupo hapa na katika kila mahali. Yeye yu upendo aliye juu ya
vyote na ndani ya vyote. Hivyo, anapatikana kwa wote lakini yeye ni fumbo daima
kwa sababu hakuna lolote ambalo liweze kuweka mipaka kwako. Kulingana na
Mtakatifu Agustino, “Mungu ni wa milele mno hata wakati yeye anapopatikana kuna
yote ya kupatikana bado.” Kuna hadithi fulani ya Mtakatifu huyo ambayo
inatusaidia kutafakari fumbo la Utatu Mtakatifu kama fumbo si la kufahamiwa
bali la kukaribishwa. Ikiwa tunajifungua zaidi kwa fumbo hili tunaweza kuhisi
zaidi tendo lake ndani yetu.
“Siku moja
Mtakatifu Agustino, aliye mchungaji na mwalimu wa kanisa, alikuwa akitembea katika
pwani ya bahari, akijiuliza swali kuhusu fumbo la Utatu Mtakatifu, akisema,
“inawezekanaje Mungu kuwako kama Mmoja na Utatu wakati huo huo?” Ghafla,
alimwona mtoto mdogo aliyefanya shimo katika mchanga na kukimbia kwenye bahari,
akachukua maji kidogo na kuyaweka shimoni. Baada ya kuangalia mchezo huu wa
mtoto mdogo kwa mara nyingi, Agustino aliamua kumwuliza maana ya mchezo huo.
Mtoto mdogo akamjibu akisema: “Najaribu kuweka maji yale yote ndani ya shimo
hii”. Ameshangaa sana, Agustino akasema: “Hutapata kufanya hivyo kamwe!” Kisha,
mtoto mdogo akamwambia akisema: “ni rahisi kwangu kuyaweka maji yale yote
shimoni kuliko wewe upate kufahamu fumbo la Utatu Mtakatifu kwa akili yako.
Mwishowe, mtoto mdogo alitoweka na Mtakatifu Agustino akajiambia: “Labda mtoto
huyo angeweza kuwa ni malaika!”
Ujumbe wa masomo
ya siku ya leo unatusaidia kujifungua kwa fumbo hili. Kwa mfano, somo la kwanza
linaongelea Mungu aliye karibu, ambaye anajifunua katika hali yetu ya kawaida
kwa ishara ndizo halisi sana. Kuwa naye uhusiano wa mwana na imani ndiyo njia
kamili ya kupata furaha na maisha mengi. Somo la pili linachukua tena hali
ambayo tulitafakari wiki iliyopita, yaani tumepokea Roho ambaye anatufanya kuwa
wana. Tendo la Roho ndani yetu anathibitisha kwamba sisi tu wana wa Mungu, na
Yesu “hana aibu ya kuwafikiria kama ndugu wale ambao aliwatakasa”. Utakaso huu
unamaanisha kuhusishwa katika ushirika mmoja ambao yeye anaishi pamoja na Baba,
ushirika wa Mungu ambaye hajui kufanya jambo lingine isipokuwa kupenda.
Wanafunzi
waliitwa na Yesu kuenda pamoja kwenye mahali fulani huko Galilaya. Kutoka
mahali huko walitumwa pamoja tena
kuinjilisha kwa sababu ushahidi wa kwanza wa jumuiya ya wanafunzi wa Yesu ni
umoja utakaohakikishwa na Roho yake. Kila mtu anaitwa kuweka juhudi kwa ajili
ya kuusaidia umoja huu kama maana ya utambulisho. Tumezipokea zawadi kutoka kwa
Mungu ili tuwe zawadi sisi kwa sisi na kuendeleza kuujenga mwili mmoja, ambao
ni takatifu na hai kwa sababu ni Roho mmoja anayetenda ndani yake. Hivyo, uwepo
wa Yesu ni muhimu sana kwa ajili ya nguvu na ufanisi wa wanafunzi wake, kwa maana
mwili bila kichwa unakufa. Siku moja alisema, “Bila mimi hamuwezi kufanya
chochote”.
Ndiye Yesu peke
yake na mamlaka aliyopokea kutoka kwa Baba ya kudhihirisha mpango wake wa wokovu.
Alishiriki mamlaka haya na wanafunzi wake kwa ajili ya kufanya wanafunzi wapya
miongoni mwa watu. Wanafunzi walitumwa
kama wajumbe wa habari njema kwa wanadamu wote kwa sababu injili haina mipaka.
Yesu aliwaahidi kuandamana nao mpaka upeo. Ingawa uwepo wake wa mwili hauonekani
tena, Roho wake anahakikisha ukaribu wake katika safari yao kwa sababu kama
Yesu alitenda pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, vivyo hivyo Roho huyo anatenda
pamoja na Yesu na Baba. Ikiwa wanafunzi wanaruhusu kuongozwa na Roho huyo wanaweza
kuwashirikisha wengi katika mpango wa Yesu ulio mpango wa Utatu Mtakatifu. Kuwa
mwanafunzi wa Yesu ni kuwa makao ya Utatu Mtakatifu.
Ujumbe wa
uhusiano wa Utatu Mtakatifu ni msaada mkubwa ambao Ukristu unatoa kwa jamii
yetu ambayo inaongozwa kwa njia ya ubinafsi na mashindano. Yesu alitukabidhi
ujumbe wa upendo kama maana ya mambo yote. Tunaweza kuonyesha ukweli wa ujumbe
huu ikiwa tunaishi kuungana naye (na
Utatu). Siku moja alisema “wote wawe na umoja; kama wewe Baba, ulivyo
ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu ili ulimwengu upate
kusadiki.” Tunapoishi kwa uhusiano wa ndani na Yesu vivyo hivyo tunahisi ndani
yetu tendo la Baba na Roho wake. Uzoefu wetu wa Yesu katika Ekaristi ni tena
uzoefu wa Utatu Mtakatifu. Kulingana na fumbo hili, Mungu anatumikia, yeye yupo
kati yetu na tena ndani yetu. Ndiye yeye mwenyewe anayetuunganisha naye na
miongoni mwetu. Anafanya hivyo kwa sababu anataka tuwe washiriki katika uhai
wake mwenyewe. Kwa hivyo, tuombe “Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mt...
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário