Kutafakari kuhusu Yon 3, 1-5.10; Mk 1,14-20
Tukiendelea
tafakari yetu iliyopita, tena jambo letu ndilo la wito. Tofauti kati yao ni
kwamba katika mara iliyopita tulialikwa kutembelea/kushiriki katika hali ya kawaida
ya Mwalimu Yesu; mara hii ndiye yeye ambaye anakuja katika hali yetu ya kila
siku kwa njia ya unyenyekevu na mvuto na kutoa pendekezo lake kwetu, hata ni
ngumu kulikataa. Labda hatupati kumfuata ‘mara’ kama yeye anataka, lakini
anakubali tuanze kuchukua mwendo wa kutubu kwa umakini ambao unafananisha
maisha yetu pole pole kulingana na njia yake ya kuwa na kuishi.
Andiko la kwanza
linaongea kuhusu wito wa Yona na kutubu kwa watu wa Ninive, mji mkuu wa Asiria.
Yona ndiye nabii aliye na tabia siyo za kawaida. Mungu alimpa kazi, kama
alivyofanya kwa ajili ya manabii wengine, lakini badala ya kuchukua kazi, Yona
aliamua kuenda zake mbali sana na Mungu. Baada ya muda fulani katika tumbo la
nyangumi, alichukua kazi lakini kwa upinzani ya kibinafsi dhidi ya njia ya Mungu
ya kutenda. Nabii Yona ndiye Myahudi ambaye aliitwa kufanya kazi kati ya maadui
wa Wayahudi. Basi, wakati Mungu alipomwomba kutangaza kutubu, Yona alitangaza
kuharibu. Kwa bahati nzuri, watu walimwamini Mungu na kubadilisha tabia zao.
Mungu anatarajia tabia hii tu kutoka kwa watoto wake bila kufikiria taifa gani
mtu anapokuja.
Hii ndiyo nia ya
Yesu wakati alipoanza maisha yake ya umma. Wakati Yohana Mbatizaji alifungwa
gerezani, yaani wakati ambao utabiri wa Neno la Mungu haukutangazwa tena, Yesu
alitambua kwamba nafasi yake ilifika. Basi, yeye aliacha Uyahudi ambapo
alifanya uzoefu wa ubatizo na jangwa na kwenda Galilaya akitangaza habari njema
ya Mungu. Kiini ya ujumbe wake ni
ukaribu wa Ufalme wa Mungu na hivyo, mwaliko wa kutubu kama tabia muhimu
ya kuukaribisha ufalme huu. Alisema: “Wakati umetimia na ufalme wa Mungu
umekaribia. Tubuni na kuiamini injili!” Kupitia Kristo, wakati unapata
ukamilifu wake. Wakati ambao tunaongea hapa sio kronos kama kiasi ya wakati, bali ndiyo kairos, yaani wakati mwafaka ya kukutana na Mungu na wokovu wake.
Katika nafsi ya
Kristo, ufalme unakuwa hali halisi. Kuuamini na kuukubali ufalme huu
kunamaanisha kukubali kumfuata Kristo ambaye analeta pendekezo la jamii mpya
kabisa na kubadilisha maisha ya walioalikwa. Hivyo, Yesu anapita na kuwaona
ndugu wawili, yaani aliiangalia familia ambayo kwa kupitia mahusiano na kazi
yake ya kila siku inazaa maisha na kujenga historia. Yesu anajitoa kama kipimo,
akiwaita ndugu hawa kutoa maana kwa maisha yao ya kawaida. Alisema: “Mnifuateni
nami nitawafanya nyinyi kuwa wavuvi wa watu.” Yesu ndiye wazi sana na pendekezo
lake lina mvuto na kunasababisha uamuzi. Kutoka kwa ndugu hawa Yesu anataka
kujenga dunia ya kindugu. Pendekezo lake linaalika kuacha kila kitu mara, yaani
kwa upatikanaji kabisa: kuanza kwa nyavu na baadaye familia… ama mawazo ya
uongo kuihusu familia...
Kulingana na
andiko hili, mwaliko wa kutubu unauhusu mwaliko wa kumfuata Yesu. Mwaliko wa
msingi ulioelekezwa kwa kila mtu ndio ule wa kutembea nyuma ya Kristo na pamoja
naye ili kuitoa maana ya kweli kwa maisha ya mtu mwenyewe, kama wanafunzi wa
kwanza ambao waliendelea kama wavuvi lakini kwa njia tofauti. Ikiwa mimi niko
na kazi ama nimefunga ndoa ama niko na wito fulani wa utumishi wa kikanisa ama
tena ninautafuta wito wangu, baada ya kukutana na injili ya Kristo siwezi
kubaki nilivyo kabla ya mkutano huu, yaani ninapaswa kuamua na kuishi wito na
kutafuta kwangu kwa njia tofauti. Hali ya kawaida na hali ya jumuiya zilikuwa
muhimu sana katika maisha ya Yesu na ya wanafunzi wa kwanza. Kwa upande wetu
hali hizi ndipo mahali ambapo Mungu anatutembelea daima na kupendekeza kwetu
mwendo wa metanoia, yaani mabadiliko
ya mawazo, ya njia ya kutenda, ya kufikiri na kuishi.
Kwa kuishi vizuri
wito wetu ni lazima kuacha kitu fulani ama vitu vingi. “Hata hivyo ni muhimu
kukumbuka pia kwamba mwanafunzi sio mtu ambaye anaacha kitu bali ndiye yeyote
ambaye alimkuta Mtu. Ikiwa tunaacha kitu tunazawadiwa mno na Yule ambaye
tunamkuta”. Ndivyo hivyo tukio letu na Kristo; hatujui litamalizika wapi,
lakini yeye anajua. Ni lazima ujasiri kwa kumwamini yeye ambaye alipendezwa kuukabidhi
ufalme wake kwa sisi. Basi, tunaalikwa kuyaungana maisha yetu na yake ili
kuitoa maana ya kweli kwa maisha yetu. Kama wanafunzi wa kwanza ambao waliacha
kila kitu na kwa utayari walimjibu Bwana ambaye aliwaalika, tujikabidhi katika
Yesu, kwa kuacha usalama wetu wa uongo na kila kitu ambacho kinatuzuia kuishi
wito wetu kwa upatikanaji kabisa kwa ajili ya ufalme wake.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário