Kutafakari kutoka Kumbukumbu la Sheria
18: 15-20; 1Wak 7: 32-35; Marko 1: 21-28
Masomo haya ni mwaliko ili tukaribishe mafundisho ya
Neno la Mungu ambalo lina uwezo wa kubadilisha maisha ya watu kwa
kuwapa uwezo ili wawe wajumbe wa wakati mpya. Andiko la
linataja mfano wa nabii atakayechukua nafasi ya Musa na kuzungumza na watu kwa
jina la Mungu. Nabii ndiye mtu anayechukuliwa na hali ya watu ili kuongea nao yale ambayo Mungu
anamwuliza kusema tu. Msukumo wa Mungu,
pamoja na upatikanaji wa nabii, ulifanya tofauti kubwa maishani mwa Waisraeli,
ukiwaongoza kuyaona maisha mapya. Mt. Paulo
anaonyesha tamani yako ili watu wa jumuiya ya Kikristo waweze kuishi bila
wasiwasi kwa sababu tabia hii ndiyo matokeo ya hofu nayo inazuia ushuhuda wa
kweli. Jumuiya inaalikwa kufanya upya ahadi yake ya imani katika Bwana Yesu
Kristo, ndiye mfano yetu ya kujisalimisha mikononi mwa Mungu.
Baada ya ubatizo na
uzoefu jangwani, Yesu alianza kazi yake
akitangaza Ufalme wa Mungu na kuwaalika watu watubu. Yeye hupenda kutembelea na kufundisha
katika masinagogi kwa sababu katika mahali hapo kwa kawaida watu hukusanya wasikilize Neno
la Mungu na kuyakubali mapenzi
yake. Mamlaka aliyopokea Yesu
kutoka kwa Baba yanaonyesha kwamba
mafundisho yake ni vizuri kuliko waandishi.
Kidogo kidogo watu walielewa kwamba mtu huyo Yesu, ambaye
alizungumza kwa upendo na ukweli,
alikuwa mjumbe wa Mungu. Maneno yake yana
uhai kabisa na kuongoza kwa mabadiliko ya maisha. Wale ambao wana kazi
ya kuwaongoza watu, wanapaswa kuisikiliza sauti yake.
Hata pepo
wachafu wanautambua utambulisho na
mamlaka ya Yesu, lakini hawashiriki hisia zake na ahadi yake kwa ajili ya watu.
Kwa hivyo, Yesu hazungumzi
nao; yeye anawaamuru wanyamaze tu.
Pepo wachafu hawa ni ishara ya upinzani dhidi ya mpango wa Mungu, kuwadhoofisha watu na kuwazuia
kuishi uwezo wao kikamilifu. Mbele
ya nguvu hizi, Yesu anaweka mamlaka na kutenda
kama Mkombozi.
Uwepo wa Yesu kati ya binadamu unaanzisha
wakati mpya, yaani wakati wa wokovu wa
Mungu. Kupitia matendo ya Yesu,
Mungu anaonyesha upendo na utunzaji kuhusu maisha ya watu wake. Yale ambayo
Yesu anatenda ndiyo kulingana na maneno anayosema. Kwa hivyo mafundisho yake yanafikiriwa mapya sana. Yeye ni Masiya wa
Mungu anayetabiriwa na manabi wengi na kutarajiwa kwa muda mrefu sana. Lakini haitoshi
kuutambua utambulisho wa Yesu kama
Masihi wa Mungu, kwa sababu hata pepo wachafu walivyo. Mtakatifu Agustino alisema: “Usijiridhishe kwa kumwamini
Mungu; hata pepo wachafu walivyo.” Ni muhimu kukubali pendekezo la Yesu la toba na
kuweka juhudi kwa kufanya uhusiano mwema
na Mungu na wengine. Upinzani dhidi ya Yesu ni upinzani kwa mafanikio wa Ufalme wa Mungu. Yesu wakati alipotangaza habari njema ya Ufalme, akawaomba watu ushiriki kwa hiari. Jibu ambalo anatarajia kutoka
kwetu ndilo kutafuta kwa Ufalme huu
kama kipaumbele, kwa sababu hii ni maana ya maisha na kazi zetu.
Ujumbe wa injili hii ni pendekezo
la uanafunzi upya. Ni mwaliko kwetu ya kujisalimisha kwa ajili
ya Yule ambaye ametuita na kutaka tuwe
wajumbe wake. Yeye hujitambulisha
na wale waliomfuata. Yesu anaendelea kutenda dhidi ya nguvu zote au mawazo ambayo
yanayaogopesha maisha ya watu. Kwa
maneno mengine, kupitia matendo
yetu, ishara za ukombozi wa Kristo bado zinatokea katika maisha ya watu wengi. Kutoka kwake tunaupokea uwezo ili tuwe
mashahidi wa kweli kwa kutangaza ukweli wa ufalme wake kupitia
tabia zaidi kuliko maneno. Hakika Yesu anaandamana nasi katika safari yetu, kutuhamasisha kupigana dhidi ya maovu
na dhambi ambayo inatuzuia
kumtumikia Mungu kwa ukarimu na hiari. Neno lake ni pendekezo ambalo tunataka kuchukua kama sheria
ya maisha. Neema yake itusaidie kuchukua ahadi hii.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário