sábado, 27 de janeiro de 2018

HAJA YA MAFUNDISHO MAPYA


Kutafakari kutoka Kumbukumbu la Sheria 18: 15-20; 1Wak 7: 32-35; Marko 1: 21-28



Masomo haya ni mwaliko ili tukaribishe mafundisho ya Neno la Mungu ambalo lina uwezo wa kubadilisha maisha ya watu kwa kuwapa uwezo ili wawe wajumbe wa wakati mpya. Andiko la linataja mfano wa nabii atakayechukua nafasi ya Musa na kuzungumza na watu kwa jina la Mungu. Nabii ndiye mtu anayechukuliwa na hali ya watu ili kuongea nao yale ambayo Mungu anamwuliza kusema tu. Msukumo wa Mungu, pamoja na upatikanaji wa nabii, ulifanya tofauti kubwa maishani mwa Waisraeli, ukiwaongoza kuyaona maisha mapya. Mt. Paulo anaonyesha tamani yako ili watu wa jumuiya ya Kikristo waweze kuishi bila wasiwasi kwa sababu tabia hii ndiyo matokeo ya hofu nayo inazuia ushuhuda wa kweli. Jumuiya inaalikwa kufanya upya ahadi yake ya imani katika Bwana Yesu Kristo, ndiye mfano yetu ya kujisalimisha mikononi mwa Mungu.

Baada ya ubatizo na uzoefu jangwani, Yesu alianza kazi yake akitangaza Ufalme wa Mungu na kuwaalika watu watubu. Yeye hupenda kutembelea na kufundisha katika masinagogi kwa sababu katika mahali hapo kwa kawaida watu hukusanya wasikilize Neno la Mungu na kuyakubali mapenzi yake. Mamlaka aliyopokea Yesu kutoka kwa Baba yanaonyesha kwamba mafundisho yake ni vizuri kuliko waandishi. Kidogo kidogo watu walielewa kwamba mtu huyo Yesu, ambaye alizungumza kwa upendo na ukweli, alikuwa mjumbe wa Mungu. Maneno yake yana uhai kabisa na kuongoza kwa mabadiliko ya maisha. Wale ambao wana kazi ya kuwaongoza watu, wanapaswa kuisikiliza sauti yake.

Hata pepo wachafu wanautambua utambulisho na mamlaka ya Yesu, lakini hawashiriki hisia zake na ahadi yake kwa ajili ya watu. Kwa hivyo, Yesu hazungumzi nao; yeye anawaamuru wanyamaze tu. Pepo wachafu hawa ni ishara ya upinzani dhidi ya mpango wa Mungu, kuwadhoofisha watu na kuwazuia kuishi uwezo wao kikamilifu. Mbele ya nguvu hizi, Yesu anaweka mamlaka na kutenda kama Mkombozi.

Uwepo wa Yesu kati ya binadamu unaanzisha wakati mpya, yaani wakati wa wokovu wa Mungu. Kupitia matendo ya Yesu, Mungu anaonyesha upendo na utunzaji kuhusu maisha ya watu wake. Yale ambayo Yesu anatenda ndiyo kulingana na maneno anayosema. Kwa hivyo mafundisho yake yanafikiriwa mapya sana. Yeye ni Masiya wa Mungu anayetabiriwa na manabi wengi na kutarajiwa kwa muda mrefu sana. Lakini haitoshi kuutambua utambulisho wa Yesu kama Masihi wa Mungu, kwa sababu hata pepo wachafu walivyo. Mtakatifu Agustino alisema: “Usijiridhishe kwa kumwamini Mungu; hata pepo wachafu walivyo.” Ni muhimu kukubali pendekezo la Yesu la toba na kuweka juhudi kwa kufanya uhusiano mwema na Mungu na wengine. Upinzani dhidi ya Yesu ni upinzani kwa mafanikio wa Ufalme wa Mungu. Yesu wakati alipotangaza habari njema ya Ufalme, akawaomba watu ushiriki kwa hiari. Jibu ambalo anatarajia kutoka kwetu ndilo kutafuta kwa Ufalme huu kama kipaumbele, kwa sababu hii ni maana ya maisha na kazi zetu.


Ujumbe wa injili hii ni pendekezo la uanafunzi upya. Ni mwaliko kwetu ya kujisalimisha kwa ajili ya Yule ambaye ametuita na kutaka tuwe wajumbe wake. Yeye hujitambulisha na wale waliomfuata. Yesu anaendelea kutenda dhidi ya nguvu zote au mawazo ambayo yanayaogopesha maisha ya watu. Kwa maneno mengine, kupitia matendo yetu, ishara za ukombozi wa Kristo bado zinatokea katika maisha ya watu wengi. Kutoka kwake tunaupokea uwezo ili tuwe mashahidi wa kweli kwa kutangaza ukweli wa ufalme wake kupitia tabia zaidi kuliko maneno. Hakika Yesu anaandamana nasi katika safari yetu, kutuhamasisha kupigana dhidi ya maovu na dhambi ambayo inatuzuia kumtumikia Mungu kwa ukarimu na hiari. Neno lake ni pendekezo ambalo tunataka kuchukua kama sheria ya maisha. Neema yake itusaidie kuchukua ahadi hii. 

Fr Ndega

segunda-feira, 22 de janeiro de 2018

ESPERIENZA CHE PORTA IL SENSO VERO ALLA NOSTRA VITA


Riflessione su Sam 3: 3-10.19; 1Cor 6: 13-15.17-20; Gv 1,35-42

La nostra vocazione è una storia d’amore perché la sua origine è Dio che dona se stesso quando chiama qualcuno perché sia suo/sua servo/a. Per questo ogni vocazione porta con sé una verità profonda, vale a dire: se esiste Dio, egli ama; e se ama, egli chiama. Se esiste libertà, la sua origine è Dio; se esiste essere umano, esiste come essere libero perché viene da Dio. E se esiste vita, è perché sia donata come il proprio Dio fa. In ogni vocazione è Dio stesso che prende l’iniziativa realizzando un rapporto d’amore con la persona chiamata per il suo servizio.
La vocazione di Samuele, raccontata nel primo testo, è un modello per tutte le vocazioni. Dio gli viene incontro in una occasione veramente speciale, lo chiama per nome dimostrando che lo conosce. Fin da ragazzo Samuele è stato offerto dalla sua mamma per servire Dio ed è stato cresciuto nel tempio. Dio ha accettato l’offerta e decide di rivelare a Samuele la sua volontà. E’ chiaro che Samuele ha avuto bisogno di un processo di discernimento per capire l’intenzione di Dio per la sua vita. Il sacerdote Eli è stato la mediazione di Dio per aiutare Samuele a discernere la voce che gli parlava a partire dal suo intimo e rispondere con prontezza. Dio chiamò Samuele per tre volte. Vuol dire che l'invito di Dio a Samuele è stato espresso più volte. Dio non si stanca mai di chiamare le persone perché questo è il suo modo di dimostrare amore per ognuno. È necessario stare attenti e cercare aiuto per discernere la voce di Dio tra le molte voci che si fanno sentire e rispondere alla sua chiamata con generosità e prontezza.
Secondo San Paolo, siamo tempio di Dio e la nostra vocazione è essere membra del corpo di Cristo. Attraverso il nostro battesimo Dio ci ha fatto sua dimora: “Non sapete che voi siete tempio di Dio e che il suo Spirito dimora in voi?” Quindi come membra del corpo di Cristo, la nostra identità è essere con gli altri. Non siamo stati creati per vivere da soli o per noi stessi ma per la comunione. Noi viviamo la nostra vocazione insieme agli altri e aiutati dagli altri. Dio ha voluto usare la realtà del nostro corpo per mostrare la sua divinità. Quando permettiamo che il suo Spirito ci conduca, siamo in grado di rivelare il Dio che dimora in noi. Anche senza conoscenza siamo aiutati a compiere la nostra vocazione perché apparteniamo a Dio.
Il vangelo parla della vocazione dei primi discepoli di Gesù, secondo la versione di Giovanni. Tutto comincia con l’esperienza. Giovanni Battista certamente ha avuto l’opportunità di conoscere Gesù e proprio per questo è stato in grado di indicarlo come “Agnello di Dio che toglie i peccati del mondo”. La sua testimonianza è stata fondamentale perché i suoi discepoli potessero seguire il vero Maestro. Quando Gesù li vide ha posto loro la domanda fondamentale della loro esistenza, vale a dire: “Che cosa cercate?” Più avanti, nell’ultima parte del vangelo di Giovanni la domanda non sarà più “che cosa cercate” ma “chi cercate?” perché veramente i discepoli non cercano qualcosa ma qualcuno. I due discepoli rispondono a Gesù con un’altra domanda: “Maestro, dove dimori?” questa domanda rivela che davvero volevano conoscere il maestro e rimanere con lui. Questa esperienza ha portato nel loro cuore la passione per Gesù e la passione per annunciarlo perché gli altri potessero avere la stessa opportunità di sperimentare una nuova vita come è accaduto a loro. Così Andrea trovando suo fratello Simone gli ha detto: “Abbiamo trovato il Messia”, cioè abbiamo trovato colui che ha portato il senso vero alla nostra vita.
Ci sono delle esperienze che preferiamo lasciar perdere e ce ne sono altre che sono fondanti perché marcano profondamente la nostra vita e senza di esse nulla ha senso per noi. Questo tipo di esperienza richiede un perdersi per trovarsi veramente. È a questo che ci invita Gesù quando propone “venite e vedrete” – Vedrai che bello! Questa è l’esperienza che il nostro cuore desidera in modo molto profondo. Non possiamo conoscere Gesù in fretta soltanto per sentito dire. Trattasi di un processo che richiede lungo tempo ed esperienza costante della sua presenza. Lui stesso vuole rivelarsi a noi, ma la sua rivelazione si scopre passo dopo passo; è ciò che accade in questo testo in cui Gesù è chiamato prima “Agnello di Dio, poi “Maestro” e più tardi Andrea lo chiamerà  “Messia”.
Se vogliamo conoscere Gesù davvero dobbiamo accettare l’invito di partecipare alla sua quotidianità e rimanere con lui permettendo che la nostra vita sia coinvolta nella sua e trovi in essa la sua vera identità e senso. In questo processo le mediazioni che Dio ci invia sono veramente importanti, per esempio, la sua Parola, la realtà della comunità, i nostri fratelli bisognosi, l’accompagnamento spirituale, ect. Senza un processo di discernimento tramite realtà come queste, diventa difficile scoprire la chiamata di Dio e discernere la sua voce che ci chiama. Permettiamo di essere condotti dalla sua Parola e siamo aperti alla realtà attorno a noi perché possiamo vivere la nostra vocazione con impegno e fedeltà secondo la volontà di colui che ci ha chiamato.

Fr Ndega
Revisione dell'italiano: Giusi

sábado, 20 de janeiro de 2018

WITO KAMA MWALIKO KWA MABADILIKO YA MAWAZO


Kutafakari kuhusu Yon 3, 1-5.10; Mk 1,14-20


          Tukiendelea tafakari yetu iliyopita, tena jambo letu ndilo la wito. Tofauti kati yao ni kwamba katika mara iliyopita tulialikwa kutembelea/kushiriki katika hali ya kawaida ya Mwalimu Yesu; mara hii ndiye yeye ambaye anakuja katika hali yetu ya kila siku kwa njia ya unyenyekevu na mvuto na kutoa pendekezo lake kwetu, hata ni ngumu kulikataa. Labda hatupati kumfuata ‘mara’ kama yeye anataka, lakini anakubali tuanze kuchukua mwendo wa kutubu kwa umakini ambao unafananisha maisha yetu pole pole kulingana na njia yake ya kuwa na kuishi. 
            Andiko la kwanza linaongea kuhusu wito wa Yona na kutubu kwa watu wa Ninive, mji mkuu wa Asiria. Yona ndiye nabii aliye na tabia siyo za kawaida. Mungu alimpa kazi, kama alivyofanya kwa ajili ya manabii wengine, lakini badala ya kuchukua kazi, Yona aliamua kuenda zake mbali sana na Mungu. Baada ya muda fulani katika tumbo la nyangumi, alichukua kazi lakini kwa upinzani ya kibinafsi dhidi ya njia ya Mungu ya kutenda. Nabii Yona ndiye Myahudi ambaye aliitwa kufanya kazi kati ya maadui wa Wayahudi. Basi, wakati Mungu alipomwomba kutangaza kutubu, Yona alitangaza kuharibu. Kwa bahati nzuri, watu walimwamini Mungu na kubadilisha tabia zao. Mungu anatarajia tabia hii tu kutoka kwa watoto wake bila kufikiria taifa gani mtu anapokuja.
        Hii ndiyo nia ya Yesu wakati alipoanza maisha yake ya umma. Wakati Yohana Mbatizaji alifungwa gerezani, yaani wakati ambao utabiri wa Neno la Mungu haukutangazwa tena, Yesu alitambua kwamba nafasi yake ilifika. Basi, yeye aliacha Uyahudi ambapo alifanya uzoefu wa ubatizo na jangwa na kwenda Galilaya akitangaza habari njema ya Mungu. Kiini ya ujumbe wake ni  ukaribu wa Ufalme wa Mungu na hivyo, mwaliko wa kutubu kama tabia muhimu ya kuukaribisha ufalme huu. Alisema: “Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini injili!” Kupitia Kristo, wakati unapata ukamilifu wake. Wakati ambao tunaongea hapa sio kronos kama kiasi ya wakati, bali ndiyo kairos, yaani wakati mwafaka ya kukutana na Mungu na wokovu wake.
            Katika nafsi ya Kristo, ufalme unakuwa hali halisi. Kuuamini na kuukubali ufalme huu kunamaanisha kukubali kumfuata Kristo ambaye analeta pendekezo la jamii mpya kabisa na kubadilisha maisha ya walioalikwa. Hivyo, Yesu anapita na kuwaona ndugu wawili, yaani aliiangalia familia ambayo kwa kupitia mahusiano na kazi yake ya kila siku inazaa maisha na kujenga historia. Yesu anajitoa kama kipimo, akiwaita ndugu hawa kutoa maana kwa maisha yao ya kawaida. Alisema: “Mnifuateni nami nitawafanya nyinyi kuwa wavuvi wa watu.” Yesu ndiye wazi sana na pendekezo lake lina mvuto na kunasababisha uamuzi. Kutoka kwa ndugu hawa Yesu anataka kujenga dunia ya kindugu. Pendekezo lake linaalika kuacha kila kitu mara, yaani kwa upatikanaji kabisa: kuanza kwa nyavu na baadaye familia… ama mawazo ya uongo kuihusu familia...
           Kulingana na andiko hili, mwaliko wa kutubu unauhusu mwaliko wa kumfuata Yesu. Mwaliko wa msingi ulioelekezwa kwa kila mtu ndio ule wa kutembea nyuma ya Kristo na pamoja naye ili kuitoa maana ya kweli kwa maisha ya mtu mwenyewe, kama wanafunzi wa kwanza ambao waliendelea kama wavuvi lakini kwa njia tofauti. Ikiwa mimi niko na kazi ama nimefunga ndoa ama niko na wito fulani wa utumishi wa kikanisa ama tena ninautafuta wito wangu, baada ya kukutana na injili ya Kristo siwezi kubaki nilivyo kabla ya mkutano huu, yaani ninapaswa kuamua na kuishi wito na kutafuta kwangu kwa njia tofauti. Hali ya kawaida na hali ya jumuiya zilikuwa muhimu sana katika maisha ya Yesu na ya wanafunzi wa kwanza. Kwa upande wetu hali hizi ndipo mahali ambapo Mungu anatutembelea daima na kupendekeza kwetu mwendo wa metanoia, yaani mabadiliko ya mawazo, ya njia ya kutenda, ya kufikiri na kuishi.
         Kwa kuishi vizuri wito wetu ni lazima kuacha kitu fulani ama vitu vingi. “Hata hivyo ni muhimu kukumbuka pia kwamba mwanafunzi sio mtu ambaye anaacha kitu bali ndiye yeyote ambaye alimkuta Mtu. Ikiwa tunaacha kitu tunazawadiwa mno na Yule ambaye tunamkuta”. Ndivyo hivyo tukio letu na Kristo; hatujui litamalizika wapi, lakini yeye anajua. Ni lazima ujasiri kwa kumwamini yeye ambaye alipendezwa kuukabidhi ufalme wake kwa sisi. Basi, tunaalikwa kuyaungana maisha yetu na yake ili kuitoa maana ya kweli kwa maisha yetu. Kama wanafunzi wa kwanza ambao waliacha kila kitu na kwa utayari walimjibu Bwana ambaye aliwaalika, tujikabidhi katika Yesu, kwa kuacha usalama wetu wa uongo na kila kitu ambacho kinatuzuia kuishi wito wetu kwa upatikanaji kabisa kwa ajili ya ufalme wake.


Fr Ndega

LA VOCAZIONE COME UN INVITO ALLA CONVERSIONE


Riflessione su Giona 3, 1-5.10; Mc 1,14-20


     In continuità alla riflessione scorsa, anche questa volta il nostro argomento è vocazionale. La differenza è che la volta scorsa siamo stati invitati a visitare/partecipare alla quotidianità del Maestro Gesù; questa volta è lui stesso che viene nella nostra quotidianità in modo molto semplice e affascinante e ci fa la sua proposta coinvolgente, difficile da rifiutare. Forse non riusciamo a seguirlo subito come Lui vuole, ma egli accetta che prendiamo sul serio un processo di conversione che ci faccia conformare pian piano la nostra vita al suo stile di essere e di vivere.
        Il primo testo parla della missione del profeta Giona e la conversione della gente di Ninive, capitale assira. Giona è un profeta un po’ particolare. Dio gli ha dato una missione, come ha fatto con gli altri profeti, ma anziché assumerla, ha preso la decisione di allontanarsi dalla presenza di Dio. Dopo un periodo nel grembo della balena ha ripreso la sua missione, però con alcune resistenze personali perché non andava d’accordo con il modo d’agire di Dio. Giona è un ebreo che è chiamato a una missione in mezzo a un popolo nemico degli ebrei. Allora, mentre Dio manda ad annunciare la conversione, il profeta annuncia la distruzione. Per fortuna la gente ha creduto in Dio e ha cambiato i suoi atteggiamenti. È soltanto questo che Dio aspetta da ciascuno dei suoi figli, vale a dire un atteggiamento sincero di conversione a lui, non importa la nazione a cui appartenga.
        Questa è l’intenzione di Gesù quando inizia la sua vita pubblica. Quando Giovanni è stato arrestato, quando cioè la profezia della Parola di Dio non era più proclamata, Gesù ha capito che era arrivato il suo turno. Allora egli lascia la Giudea dove ha fatto l’esperienza del battesimo e del deserto e va in Galilea proclamando il vangelo di Dio. Il centro del suo messaggio è la vicinanza del Regno di Dio e quindi, l’invito alla conversione come atteggiamento fondamentale per accogliere questo Regno. Diceva: “Il tempo è compiuto e il regno di Dio è vicino: convertitevi e credete nel Vangelo”. Con Gesù il tempo raggiunge la sua pienezza. Il tempo di cui parla qui non è Kronos come quantità del tempo, ma kairòs, cioè l’occasione opportuna di trovare Dio e la sua salvezza. Con Gesù è ormai tempo di sentire Dio che ci è veramente vicino.
        Nella persona di Gesù il Regno diventa una realtà concreta. Credere e accettare questo regno vuol dire accettare di seguire Gesù che porta la proposta di una società totalmente nuova che cambia totalmente la vita di chi è coinvolto. Così Gesù passa e vede due fratelli, cioè fissa lo sguardo sulla famiglia che nei suoi rapporti e nel lavoro di ogni giorno va generando vita e costruendo la storia. Gesù si offre come punto di riferimento, chiamando questi fratelli a dare un senso vero alla loro quotidianità: “venite con me e vi farò pescatori di uomini”. Gesù è molto chiaro e la sua proposta è coinvolgente e affascinante. Da questi fratelli egli vuol costruire un mondo di fratelli. Questa proposta invita a lasciare tutto subito, cioè con totale disponibilità: primo le reti, poi la famiglia…    
       Secondo questo testo, l’invito alla conversione coincide con la chiamata a seguire Gesù. La chiamata fondamentale fatta ad ogni uomo è quella di andare dietro Cristo e con Cristo per dare un senso vero alla propria vita, come i primi discepoli che continuarono ad essere pescatori ma in modo diverso. Se ho una professione o se sono sposato o se ho una delle vocazioni di servizio ecclesiale o se sono ancora in ricerca, dopo il confronto con la parola di Gesù, non posso continuare lo stesso, devo prendere posizione, vivendo la mia vocazione o ricerca diversamente.  La quotidianità e la realtà della comunità sono stati molto importanti nella vita di Gesù e dei suoi primi discepoli. Questi sono per noi i luoghi dove Dio ci visita continuamente e ci propone una metanoia, cioè un cambiamento di mentalità, di modo d’agire, di ragionare, di vivere.
      Per vivere bene la vocazione bisogna lasciare qualcosa o molte cose. “Però è importante ricordare anche che discepolo non è chi lascia qualcosa, ma chi ha incontrato qualcuno. Quello che si perde è compensato abbondantemente con quello che si trova”. È proprio così la nostra avventura con Gesù; non sappiamo dove va finire, ma lui sa. Bisogna avere il coraggio di fidarsi di lui che ha avuto il piacere di affidarci il suo Regno. Quindi siamo chiamati a unire la nostra vita alla sua per dare un senso nuovo alla nostra vita. Come i primi discepoli che hanno lasciato tutto e con prontezza hanno risposto al Signore che li chiamava, affidiamoci a Gesù, lasciando le nostre “sicurezze” e tutto ciò che ci impedisce di vivere la nostra vocazione con totale disponibilità al servizio del Regno.\

Fr Ndega
Revisione dell'italiano: Giusi

sábado, 13 de janeiro de 2018

UZOEFU AMBAO UNALETA MAANA YA KWELI KWA MAISHA YETU


Kutafakari kutoka Sam 3: 3-10.19; 1Wak 6: 13-15.17-20; Yoh 1,35-42

Wito wetu ndio historia ya upendo kwa sababu asili yake ndiye Mungu ambaye anajitoa mwenyewe anapomwita yeyote ili awe mtumishe wake. Kwa hivyo kila wito unaleta ukweli mkubwa, yaani: Ikiwa Mungu yuko, yeye anapenda; ikiwa anapenda, yeye anaita. ikiwa uhuru uko, asili yake ni Mungu; ikiwa binadamu yuko ndiye mwenye uhuru maana anatoka kwa Mungu; ikiwa maisha yako, yakatolewe kama Mungu mwenyewe anafanya. Katika kila wito ndiye Mungu anayechukua nafasi ya uhusiano wa upendo na mtu kwa kumwita kwa utumishi wa watu wake.
Wito wa Samueli, unaosimuliwa katika somo la kwanza, ni mfano wa wito wote. Mungu alikutana naye katika nafasi maalum na kumwita kwa jina lake akionyesha kwamba alimjua Samueli. Mtoto huyo alitolewa na mamaye kwa ajili ya Mungu na kukua hekaluni. Mungu alichukua nafasi hii kumwita Samweli ili awe mtumishi wake. Bila shaka Samueli alihitaji mwendo wa utambuzi ili kufahamu nia ya Mungu kwa maisha yake. Kuhani mkuu Eli alikuwa mpatanishi wa Mungu kumsaidia Samueli kuitambua sauti ambayo ilimwita kutoka ndani yake na kujibu kwa utayari. Mungu alimwita Samueli kwa mara tatu. Inamaanisha kwamba mwaliko wa Mungu kwa Samueli ulikuwa daima. Hivyo, Mungu hachoki kuwaita watu kwa sababu hii ni njia yake ya kuonyesha upendo kwao. Ni lazima kuwa macho na kuutafuta msaada ili kutambua sauti ya Mungu kati ya sauti nyingi zilizosikika na kujibu kwa mwaliko wake kwa ukarimu na utayari.
Kulingana na Mtakatifu Paulo, wito wetu ni kuwa sehemu ya mwili wa Kristo kama hekalu hai la Mungu. Kwa njia ya ubatizo Mungu ametufanya makao yake: Ninyi ni hekalu la Mungu na Roho wake anakaa ndani yenu.” Basi, kama sehemu za mwili wa Kristo, utambulisho wetu ni kuwa pamoja na wengine. Hatujaumbwa kwa upweke ama kwa ubinafsi bali kwa ushirikiano. Tunaishi wito wetu pamoja na wengine na kusaidiwa nao. Mungu alitaka kutumia hali yetu ya kimwili ili kuonyesha hali yake ya kimungu. Wakati tunaporuhusu kuongozwa na Roho wake tunaweza kumdhihirisha Mungu anayekaa ndani yetu. Hii ndiyo hali ya kwa mahekalu matakatifu ya Mungu. Hata bila kujua sisi tunasaidiwa ili kutimiza wito wetu kwa sababu sisi ndio wa Mungu.  
Injili inaongea kuhusu safari ya wito wa wafuasi wa kwanza wa Yesu. Mambo yote yaanza kwa uzoefu. Yohana Mbatizaji alikuwa na nafasi ya kukutana na Kristo na kumjua na kwa hivyo alikuwa na uwezo wa kumwonyesha kama “Mwana-kondoo wa Mungu, aondoaye dhambi za dunia”. Ushuhuda wake ulikuwa msaada mkubwa ili wafuasi wake waweze kumfuata Yesu. Wakati Yesu alipowaona aliwauliza swali la msingi wa safari yao, yaani, “mnatafuta nini”? Kweli katika sehemu ya mwisho wa injili ya Yohane swali hili litabadilishwa kuwa “mnatafuta nani”? kwa sababu kutafuta kwa wanafunzi sio kuhusu kitu bali kuhusu Mtu. Wafuasi wawili walijibu kwa kutumia swali lingine: “Mwalimu, unakaa wapi”? Swali hili linaonyesha kwamba walitaka kujua mwalimu kwa kweli na kukaa pamoja naye. Uzoefu huu ulibadilisha maisha yao na kusababisha moyoni mwao hamu ya kumtangaza Yesu ili wengine waweze kuwa na nafasi ya kuonja maisha mapya kama ilivyotokea kwao. Hivyo, Andrea alimjia nduguye Simoni na kusema “Tumemwona Masihi”, yaani tumemwona yule ambaye alileta maana ya kweli kwa maisha yetu.

Uzoefu wa “Njoni nanyi mtaona” uliopendekezwa na Yesu ndio changamoto kwetu. Hatuwezi Kumjua Yesu kwa haraka kwa kuisikiliza habari yake peke yake. Mwendo huu unachukua muda mrefu sana na kuhitaji uzoefu wa uwepo wake daima. Yeye mwenyewe anataka kujifunua kwetu. Lakini ufunuo wake ni pole pole na hatua kwa hatua kama ilivyotokea katika kifungu hiki cha injili ambapo Yesu aliitwa kwanzaMwana-kondoo wa Mungu” na baadaye “Mwalimu” na tena Andrea alisema “Masihi”. Hivyo, pendekezo ni kukubali mwendo wa kubaki pamoja na Yesu katika hali yake na kuruhusu kwamba hali yake pole pole na kidogo kidogo yachukuliwe na maisha yetu. Katika mwendo huu upatanishi ambao Mungu anatutumia ni muhimu sana mfano, Neno lake, hali ya jumuiya zetu, ndugu zetu walio na shida, shauri ya mtu mwenye busara na kadhalika. Bila mwendo wa utambuzi kupitia hali hizi ni ngumu kugundua mwaliko wa Mungu na kutambua sauti yake iliyotuita. Kama Samueli, tunahitaji kuwa macho kwa mwaliko wa Bwana na kujibu kwa mwaliko wake kwa utayari. Kama Eli, tunaalikwa kupatikana ili kuwasaidia wengine kugundua mapenzi ya Mungu kwa maisha wao. Turuhusu kongozwa na Neno la Mungu na kufunguliwa kwa hali kandokando yetu ili tuweze kuishi wito wetu kwa ahadi na uaminifu.

Fr Ndega