Kutafakari kuhusu Luka 2, 1-14
Tangazo
la kuzaliwa kwake Yesu ndio ujumbe wa furaha kubwa
kwa wote, kwa sababu Mwokozi
amezaliwa kwa wote. Tufurahi kwa sababu Mungu anatupenda, yeye yupo kati yetu na kuleta
wokovu kwetu. Mungu
aliweza kufanya mambo yote peke yake lakini alipendelea kuuomba msaada wa
Bikira Maria, wa Yusufu na wengine wengi. Katika mpango
wake wa wokovu watu wanaalikwa kufania kitu kulingana na uwezo kibinafsi wa
kila mtu. Katika tukio la kuzaliwa kwa Yesu, Mungu alionyesha
njia yake mwenyewe ya kutenda, yaani, tukio rahisi na mahali padogo na watu wanyenyekevu.
Hali hii inathibitisha msemo wa Afrika ambao husema, “watu wanyenyekevu,
wakifanya vitu rahisi na katika mahali padogo wanaweza kubadilisha ulimwengu.” Mabadiliko makubwa ambayo
jamii yetu inahitaji yapaswa kutokea
ndani ya binadamu. Jamii mpya itatokea wakati kila mtu atambue haja ya kujibadilisha mwenyewe badala ya kujaribu
kuwabadilisha wengine. Kulingana
na Baba Mtakatifu Francisco, “Dunia itabadilika
ikiwa tuanze kuyabadilisha matendo yetu kupitia tabia zetu na chaguzi zetu.”
Katika Yesu,
Mungu amekuwa mmoja wetu, akichukua hali
yetu ya kibinadamu na kulitoa pendekezo mpya la maisha. Kwa hivyo haitoshi kumkiri
Yesu kama wokovu wa Mungu; ndiyo muhimu turuhusu kuongozwa na ujumbe wake wa amani na upendo. Kwa kuzaliwa kwake, Yesu aliwafanya binadamu wote
kuwa ni familia moja na kujaza mioyo ya
watu kwa furaha na matumaini. Kweli,
Mungu anajifunua kama jirani, maskini na
anayekataliwa, kutualika kutambua thamani ya ishara ndogo na miradi midogo. Katika
ufalme, wake wadogo na waliokataliwa wanakuwa ni wakuu.
Wachungaji pia
wanatufundisha sana. Hao walikuwa watu
waangalifu ambao walichunga wanyama
wao karibu na Bethlehemu wakati wa
usiku. Walikuwa kweli waangalifu kwa sababu ndani yao hamu ya Mungu
na uhakika wa ukaribu wake ulikuwa
hai sana. Hivyo, hao walikuwa watu wa kwanza wa kuipokea habari
ya kuzaliwa kwa Yesu kwa sababu mioyo
yao ilikuwa macho. Mtu aliye na moyo makini anaweza kuamini katika habari
njema na kutarajia hali nzuri
katika kila “alfajiri mpya”. Mtu aliye na moyo makini ana ujasiri wa kuanza safari kwenye mkutano na Mungu katika
mahali pasipotarajiwa, yaani katika hali ya mtoto mdogo na mahali
maskini sana.
Mungu Mwenyezi alikubali kuwa ni mtoto mdogo, akiutegemea utunzaji na upendo wa binadamu. Akifanya hivyo, anatufundisha tuwe na unyenyekevu
na kukubali udhaifu wetu wa kibinadamu ulio muhimu katika uhusiano wetu nawe. Imani
inatuongoza kumtambua mtoto huyu mdogo wa Bethlehemu katika
kila mtoto ambaye hukutana na sisi katika
safari yetu ya kila siku. Kila mtoto anaomba upendo
wetu. Tufikiri leo, kwa njia maalum, kuhusu baadhi ya watoto ambao
hawana uzoefu wa upendo wa wazazi
wao wala hawana mahali pa kuishi; kuhusu watoto ambao wanatumika kama askari, wanaobadilishwa katika vyombo vya vurugu, badala
ya kuwa vyombo ya upatanisho
na amani; tena kuhusu watoto walio
waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia, na kuhusu watoto maskini waliolazimishwa kuziacha
ndoto zao kwa sababu ya hali yao mbaya ya kiuchumi. Mwanga wa Bethlehemu uguse
mioyo yetu ili tuwe na utunzaji na upendo kwa walio na
mahitaji mengi.
Ingawa sisi
huishi katika jamii ya ulaji ambayo
inatuzuia kushughulika kwa thamani muhimu
sana, tunapaswa kuwa macho. Krismasi
si ulaji. Ni sikukuu
ya ufunuo wa Fumbo la upendo wa Mungu unaoweza kubadilisha moyo wa kibinadamu.
Upendo wa Mungu kwetu haitegemei astahili yetu bali wema na ukarimu wa Mungu
mwenyewe. Uzoefu huu unatuimarisha tufanye vivyo
hivyo ili kushinda hali ya vurugu na chuki katika hali yetu. Hivyo, Krismasi itakuwa sio kipindi
kimoja kwa mwaka bali kila wakati. Itakuwa Krismasi daima
ikiwa tujifunze kupenda kwa njia ya kweli
na kuweka juhudi zaidi ili kujenga
jamii ya undugu na haki kwa wema wa wote.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário