Kutafakari kutoka Is 40, 1-5, 9-11; 2Pt 3, 8-14, Mk 1, 1-8
Maandiko haya yanatualika kuandaa
njia ya Bwana kupitia safari
ya kutubu, kwa kukubali mapendekezo ya Neno la Mungu na kutangaza habari njema kutoka uzoefu wa Neno
hili. Wale ambao waliongea kwa jina la Mungu walikuwa watu waliobadilishwa na Neno
hili kwa njia ya ndani na kwa hivyo, walikuwa mashahidi
wa kweli. Mtu yeyote ambaye anaongea kwa jina la Bwana, anaweza kusaidia wengine watembee
katika njia ya Bwana.
Nabii Isaya alitabiri kuhusu wakati mpya kwa watu waliokuwa wakiteseka uhamishoni mwa Babeli na kuutarajia ukombozi. Mungu hakuwasahau watu wake na kutaka waonje hali
mpya. Hata hivyo ni lazima kuandaa njia ya
Bwana, yaani, maisha yao wenyewe. Kama kosa la uaminifu kwa Mungu lilisababisha
uhamisho, hakuna njia nyingine ya kuona maisha mapya ila uzoefu
wa huruma ya Mungu kwa kupitia kutubu. Mungu anaonyesha enzi yake hasa
anapoonea huruma. Hivyo, utukufu wake unadhihirishwa zaidi wakati
tabia yetu yabadilika kwa sababu ya mkutano na huruma hii. Hii ndiyo
habari nzuri ambayo yapaswa kutangazika. Katika somo la pili, maneno ya Petro ndiyo ushauri ili watu wasubiri ujio wa Bwana wakiwa macho na kujitolea kwa manufaa ya jumuiya. Kulingana
na Petro, Mungu ni mvumilivu na mwenye huruma. Hivyo, yeye hataki kuwaadhibu watu,
bali atarajia waweze kutubu na kuokolewe.
Miongoni
mwa wainjilisti ndiye Marko peke yake ambaye
anaingiza injili yake kwa kutumia maneno
Habari njema wakati anapoongea kuhusu
Yesu. Maneno haya habari njema
yalijulikana wakati wa Yesu, lakini hayakutumia katika maana ya kidini; yalitumia
ili kutangaza habari ya furaha, mfano, kuzaliwa kwa mfalme ama kutembelea kwa
mfalme katika sehemu fulani ya ufalme wake. Tangazo la habari hii lilileta
matarajio ya mabadiliko ya hali, lakini baadaye mambo yote yakaendelea kama
kawaida. Nia ya Marko ndiyo kujibu swali kuhusu utambulisho wa Yesu, yaani,
Yesu ni nani? Kweli katika mwanzo na mwisho wa injili hii tunakuta maneno ‘Mwana
wa Mungu’ kumhusu Yesu na mambo yote ambayo Yesu anatenda katika injili hii
yaonyesha kwamba Yesu anatoka kwa Mungu kweli. Basi, kulingana na Marko, habari
inayoleta furaha ya kweli kwa dunia hii ndiye Yesu aliye Mwana wa Mungu.
Habari njema ya Yesu inaanza kupitia kazi ya Yohana Mbatizaji, ndiye nabii mkuu, kulingana na Yesu mwenyewe. Yohana
anajulishwa kama mfano kwa wote kwa sababu alitumia nguvu zake zote ili kuwaandaa watu wakaribishe Mwana wa Mungu, ndiye Yesu Kristo.
Yohana aliishi katika upweke wa jangwa na kufunguliwa
kabisa kwa msukumo wa Mungu.
Katika mahali hapo alijifunza kutokana na Neno la Mungu, jinsi ya kushuhudia
habari njema za wokovu. Ndilo jambo la ajabu tabia yake
ya unyenyekevu hasa kuhusu mavazi na chakula. Ukuu wa Yohana ulionyeshwa katika uwezo wake wa kutambua ukuu wa Bwana, akijifikiria mwenyewe kama sauti tu
ambaye huandaa njia
ya yule atakayekuja. Katika
ujumbe wake, Yohana alitangaza huruma
ya Mungu akisema: “Mmrudie Bwana! Mungu atawasamehe dhambi zenu.” Pamoja
na maneno haya, Yohana aliwabatiza watu kama ishara
halisi ya kutubu na makaribisho ya huruma ya Mungu.
Sababu ya uaminifu wa ujumbe
wa Yohana ilikuwa sio maneno yake
tu, bali pia unyenyekevu wake na njia ya kweli ya kuishi. Hata bila maneno, maisha yake
yalikuwa tangazo la kweli la hali mpya ambayo Yesu alikuja kuleta duniani. Maisha
ya Yohane yatuambia kwamba tunaweza kufanya tofauti maishani mwa watu, lakini
ahadi haiwezekani bila uzoefu wa jangwa, yaani, uzoefu wa ndani wa Mungu na wa
Neno lake. Ndio kutoka jangwa kwamba pendekezo la mabadiliko linakuja kwetu.
Tukiishi uzoefu wa mabadiliko tunaweza kuwa mashahidi wa habari
njema kwa uaminifu kwa sababu ushuhuda wa maisha ndio
ufanisi kuliko maneno. Uvumilivu na huruma ya Mungu ndiyo nafasi tunayohitaji
ili tuweze kumrudia yeye.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário