Kutafakari
kutoka Luka 1, 26-38
Sisi tuko karibu
sana kwa kusherehekea tukio kuu ambalo linaleta mafanikio ya mpango wa Mungu
kwa dunia, yaani, Kuzaliwa kwa Mwana wake. Ndio wakati maalum wa kufungua moyo
ili kukaribisha na kuinua mikono ili kushukuru, kwa sababu Mungu anaonyesha
upendo wake mkuu kwetu, kwa kufanya makao kati yetu na kuleta wokovu kwetu.
Wokovu ni kazi ya Mungu, lakini yeye hakutaka kuifanya peke yake; alipendelea
kuuomba ushiriki wa binadamu. Bikira Maria ndiye mmoja wetu aliyejibu kwa
mwaliko wa Mungu kwa upatikanaji kabisa. Uamuzi wa Mungu wa kumchagua mwanamke huyo
mdogo unaonyesha kwamba njia yake ya kutenda ni tofauti na yetu.
Katika
andiko la kwanza, tuko na andiko la kitabiri nje ya maandiko ya manabii. Bwana
Mungu anaonyesha hamu yake ya kukaa miongoni mwa watu wake lakini ana njia yake
mwenyewe wa kufanya hivyo. Kupitia ukoo wa Daudi, atamtuma mfalme mpya ambaye ataanzisha
ufalme imara na milele. Utabiri huu ulitimiza katika Kristo ambaye tangu mwanzo
wa maisha yake ya kidunia, alichukua ahadi na historia yetu na kujitambulisha
na hali yetu. Yeye ndiye Mungu pamoja nasi. Paulo anajiona mjumbe mwaminifu wa
injili ya Yesu Kristo ambaye alitabiriwa na manabii wote. Yeye ndiye ufunuo
mkuu wa upendo wa Mungu na kupitia yeye watu wote wanaalikwa kumwamini Mungu na
kukubali mipango yake katika maisha yao.
Andiko la Luka
hili linajulikana kama andiko la “Kupasha habari”. Ndilo tangazo la kuzaliwa
kwa Yesu Kristo aliye utimizaji wa ahadi za Mungu za Agano la Kale. Ndiye
Masihi aliyetarajiwa kwa muda mrefu na alikuwa hali halisi duniani kupitia Bikira
Maria. Makaribisho yako yalikuwa maalum kwa sababu aliishi matarajio ya ujio wa
Masihi kulingana na mapenzi ya Mungu na kabla ya kuzaa Yesu katika tumbo lake,
yeye alimzaa moyoni mwake. Kama mwanamke mwangalifu, alikuwa makini sana kwa
hali ya dunia na mahitaji ya wanadamu. Aliikataa mipango yake ya kibinafsi kama
kijana ili aishi mpango wa wokovu wa Mungu. Mariamu alipata kuishi wito wake
kupitia kusikiliza Neno la Mungu na kutenda
kulingana na neno hili kama tabia yake ya kawaida. Mwinjilisti Luka anaongea
kuhusu tabia hii akisema, “Mama yake aliyaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni
mwake”.
Hivyo, neno la kwanza la malaika ndio mwaliko
wa furaha kwa sababu maisha ya Bikira Maria yalimpendeza Mungu. Mariamu alishangaza
maana ya habari hii kwako kwa sababu ya unyenyekevu wake lakini yeye aliandaliwa na Mungu na kusaidiwa na neema yake kwa ajili
ya kuwa Mama ya Mwokozi. Tangazo la Malaika Gabrieli lilimwomba Mariamu uthibitisho
wa “ndiyo” ambayo yeye alikwisha ishi kama tabia ya kawaida. Hivyo, ingawa Mungu
aliomba jibu la ukarimu na Bikira Maria alijibu kwa njia kamili. Katika udogo
na unyenyekevu wake tunaweza kuona ukuu wake, kulingana na maneno yake
mwenyewe: “Mungu anamwangalia mtumishi wake katika unyenyekevu wake... watu
wote wataniita amebarikiwa (Lk 1,48).” Maisha na chaguzi za Mariamu ni tangazo
kuu la maajabu ya Mungu. Kulingana na maisha yake, mtu ambaye huamini katika
ahadi ya Mungu ni mwenye furaha, kwa sababu Mungu anayeahidi ni mwaminifu.
Maisha ya Bikira
Maria yanashuhudia kwamba Mungu hahitaji matukio makubwa kwa kujifunua
mwenyewe. Anakuja kututembea katika maisha yetu ya kawaida naye ana mpango wa
upendo kwa kila mtu. Anachukua nafasi ya kutualika kama washirika katika kazi
zake na kutupa uwezo kwa kumjibu kwa upatikanaji kabisa kama Bikira Maria. Mungu
ndiye mwaminifu kwetu kama alivyokuwa kwa Bikira Maria. Furaha yetu ilianzishwa na uaminifu wake. Tunamshukuru Mungu
kwa tendo lake katika maisha yetu kwa njia ya Bikira Maria. Ukarimu na
upatikanaji wake kwa mapenzi ya Mungu unatuimarisha katika jibu letu la kila
siku kwa mwaliko wake na kutualika tuwatumikie wengine kwa furaha na shukrani
kama maonyesho halisi ya jibu letu la ukarimu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário