Kutafakari kuhusu Is 11: 1-10; Rm 15: 4-9; Mt 3: 1-12
Paulo akiwaandikia Waroma anathibitisha kwamba Kristo
alitimia ahadi zilizowafanyiwa mababu kama mtumishi mwaminifu wa Mungu. Uwepo
wake duniani umekuwa maonyesho ya huruma ya Mungu kwa wote hata kwa Wapagani
ambao walichukuliwa kama wasio na nafasi ya wokovu. Yeyote anayejitambulisha na
Kristo kama mfuasi wake anapaswa kuwa na hisia sawasawa na yeye. Hivyo imani na
ushirika wa Waroma na Wakristo wote wakuwa uenezi wa habari njema kwa kuzaa
mazao mazuri kwa utukufu wa Mungu. Huu ndio ukweli wa utambulisho wetu.
Injili inaongelea Yohane Mbatizaji anayeonekana jangwani
kwa kutangaza Neno la Mungu. Uwezo wa Yohane unatokana na uzoefu wa Neno hili
kwa maana hakuna mtu hata mmoja aweze kutoa ushahidi wa jambo fulani bila
kupata nafasi ya kufanya uzoefu wa jambo hili. Yohane anaanza kazi yake
jangwani. Katika biblia jangwa ni mahali maalum pa uzoefu wa Neno la Mungu.
Katika mahali huko viongozi wengi waliishi uzoefu wa ndani wa Mungu ili kujiandaa
kwa kazi ya kuwaongoza Watu wa Mungu kulingana na mwongozo wake na tena kwa
matakwa wake. Yohane Mbatizaji ndiye nabii wa mwisho na kufikiriwa kama mkuu wa
manabii wote.
Kuja kwake
Yohane Mbatizaji kunaufuata mpango wa Mungu ambaye ana wakati kamili kwa kila
kitu. Kama Yohane ni kiungo kati ya Agano la kale na la Jipya, kazi yake
inatangaza kwamba nyakati za Masiya zimeanza. Yeye ni sauti tu ambayo
inatayarisha njia za Bwana. Kwanza kabisa aliwatangazia watu watubu ili kuukaribisha
ufalme wa Mungu ulio karibu nasi. Ufalme huu unamaanisha uwepo wa Mungu
miongoni mwa watu wake kupitia nafsi ya Yesu na makaribisho kwa ufalme huu yatokea
tunapotoa ruhusa kwa tendo la Mungu maishani mwetu.
Zaidi ya
maneno, tena Yohane aliwatayarisha watu kumpokea Masiya kwa ubatizo. Kupitia
ishara hii alitangaza huruma ya Mungu iliyopatikana kwa kila mtu kwa sababu ni
mpango wa Mungu kwamba wokovu wake ufikie wote. Ubatizo wa Yohane haukuweza
kuziondoa dhambi za watu naye Yohane alitambua hilo vizuri. Basi, je ikiwa ubatizo
huu haukuwa na uwezo wa kuziondoa dhambi, kwa nini Yohane aliitumia ishara hii?
Ni kwa sababu alitaka kuwasaidia watu kukiri dhambi zao na kufungua moyo kwa huruma
ya Mungu. Ubatizo huu ulikuwa maandalizi kwa ubatizo mpya na kamili atakaotumia
Masiya kama ishara inayoonekana mapito kutoka dhambi kwenye neema na kutoka mauti
kwenye maisha mapya.
Ubatizo wa Yohane
ni tofauti na ubatizo wa Yesu, lakini yote mbili ni nafasi ya kuishi maisha
mapya. Kwa upande wetu maisha mapya ni zawadi ya Kristo na matokeo ya utume
wake. Ubatizo wa Kikristo, pamoja na maondoleo ya dhambi, unadhamini ushiriki
katika uzima wa Mungu mwenyewe. Ubatizo ni wa kwanza kati ya sakramenti tatu za
mwanzo ukifuatiwa na Kipaimara na Ekaristi kwa uzoefu wa mwanzo katika safari ya
kikristo. Ubatizo wetu ni ishara ya nje ya kufa kwa maisha ya dhambi, na ya kufufuka
kwa maisha mapya katika Kristo aliye mshindi dhidi ya dhambi na mauti. Yeye ni mwanga
wa kweli unaomfafanua kila mtu. Kupitia mwendo huu tumekuwa wana wa nuru ili
tutembee katika nuru ya Mungu kila siku ya maisha yetu.
Kipindi cha
Majilio kinatusaidia kujiandaa kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu. Maisha ya
unyenyekevu ya Yohane ni mwaliko tutende kama yeye alivyo ili maisha yetu
yaweze kumpendeza Mungu. Mambo Yohana aliyowaambia mafarisayo na masadukayo ni
muhimu pia kwetu: kuhusu kutubu hayatoshi maneno; tunapaswa kuzionyesha ishara
halisi za mabadiliko yetu, vinginevyo hatutapata kujitayarisha ipasavyo kwa kumkaribisha
yesu. Kuna vikwazo vingi vya kuondoa katika maisha yetu kwa msaada wa huruma ya
Mungu. Basi, tuchukue nafasi hii nzuri kuadhimisha sacramenti ya Upatanisho (na
kitubio) na kuishi kwa njia mpya uhusiano wetu na Mungu na wengine.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário