Tafakari kutoka Is 7: 10-14; Rm 1: 1-7; Mt 1: 18-24
Katika
safari yetu kuelekea Krismasi, ni muhimu sana kutafakari kuhusu Mtakatifu
Yosefu aliyekuwa mtu mkimya bali alikuwa na ushiriki mkubwa katika kuhakikisha
usalama na ulinzi kwa Mwana wa Mungu aliyekuja ulimwenguni, dhaifu na mhitaji.
Ingawa Mungu angeweza kuwaokoa wanadamu peke yake, alitaka kuchagua washirika kwa
kutekeleza mpango wake kama alivyosema Mtakatifu Augustino, “Mungu alituumba
bila sisi lakini hakutaka kutuokoa bila sisi”.
Katika
somo la kwanza nabii Isaya halikukataa uamuzi wa mfalme wa Yuda, yaani Ahazi ambaye
akihisi kutishwa na uvamizi unaowezekana na uliokuwa karibu, aliamua kufanya
mapatano ya kisiasa na kijeshi pamoja na Ashuru badala ya kumwomba Bwana ishara
kama maonyesho ya imani katika uwepo na ulinzi wake. Lakini Mungu, hata
akikataliwa, hajiachi kuzuiwa kuhusu mpango wake wa kuwaokoa watu wake na kwa
sababu hiyo anatoa kuzaliwa kwa mtoto ambaye ataufanya ufalme huu kuwa imara,
na kutoa mustakabali wa tumaini kwa watu wote. Tunaona katika mtoto huyo sura
ya Yesu, ambaye anatuletea wokovu, akihakikishia kwamba uthabiti wa kweli
hautokani na ulinzi wa kibinadamu bali kwa kumtumaini Mungu.
Katika
somo la pili, Paulo anahutubia Wakristo wa Rumi kwa kujijulisha mwenywe si kwa kutumia
data yake binafsi ya masjala bali kutokana na utambulisho wake mpya uliozaliwa
kutokana na mkutano na Yesu Kristo aliyemfanya kuwa mtume wa Mataifa.
Utambulisho wake huu hautokani na sifa zake bali ni uchaguzi unaofanywa kwa upendo,
zawadi ya neema ya Mungu. Ufahamu huu wa Mtume Paolo unatuimarisha katika
safari yetu na kutufanya tuelewe kwamba sisi pia tunapendwa na Mungu nasi tu
watakatifu kwa wito kwa ajili ya kuwa washirika wake katika kazi ya wokovu kama
mashahidi wa upendo wake na uhuru wake.
Injili
inatujulisha mfano wa Yusufu ambaye anaitwa mtu mwenye haki, yaani, “aliyekuwa
na sheria yote ya Bwana moyoni mwake”. Kwa sababu ya pendekezo la Mungu lenye changamoto
kwa Mariamu, anaongozwa kufanya uchaguzi wa ajabu. Maria anapomweleza kuhusu
hali aliyokuwa akikabili, anamhakikishia kwamba ilikuwa ni uingiliaji wa
kimungu. Kisha, Yosefu alikuwa mbele yake si tu sheria ya Mambo ya Walawi,
ambayo iliamuru kushutumu wanawake kama kwahali hii ya Mariamu, bali pia upendo
aliokuwa nao kwa msichana huyo na uaminifu wa maneno yake, akikubali kuweka
maisha yake hatarini ili mpango wa Mungu ukatimize kwa ajili ya wokovu wa watu
wake.
‘Ndiyo’
ya Maria aliye huru na mkarimu ilikuwa imesubiriwa na Mungu ambaye alimtaka awe
mtumishi wake na alikuwa amemwandaa kwa hili, lakini tunapaswa kukubali kwamba
ili aishi ndiyo hii yake, zaidi ya neema ya Mungu, Mariamu pia alisaidiwa na ndiyo
ya Yusufu. Kwa busara na ukimya wake, anafanya ndoto ya wanandoa itimie kwa
wakati zaidi na kumpa Mungu nafasi sahihi ya kutenda. Kwa hakika, pamoja na
Yusufu Mungu hatoi Mariamu tu bali pia malaika wa kumsaidia “kuifuata njia ya
upendo na kuiacha ile ya Sheria”. Hivyo toleo la Maria kuhusu ukweli wa lililotokea
limethibitishwa. Wote wawili wameongozwa katika njia ifaayo ili kazi hii
iliyozaliwa na mpango wa kimungu isishindwe kwa sababu ya magumu ya kibinadamu.
Watu
hawa wawili wanaotembelewa na Mungu, katika unyenyekevu na udogo wao hufanya
maisha yao ya kila siku kuwa yenye kuzaa matunda, wanakuwa vyombo vya heshima
vilivyotumiwa na Mungu kwa hiari katika kazi kuu ya wokovu. Ushuhuda wao unatusaidia kuelewa ni nini njia ya Mungu
na ni nini hasa kinachompendeza. Hata kama
hawakuelewa kazi yao ingekuwaje hapo mwanzo, hawakuweka vikwazo katika njia ya
mipango ya Mungu.Vivyo hivyo lazima iwe mwitikio wetu wa kila siku kwa wito wa
Mungu. Hatuhitaji kuelewa mara moja kazi yetu inapaswa kuwa nini. Tunahitaji
kupatikana na kuwa tayari kwa kila kitu, tukimwaminia Mungu kama Mariamu,
Yusufu na wengine wengi walivyofanya.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário