Kutafakari kuhusu Lk 9, 28b-36
Tukio la kugeuka sura kwa Yesu kulitokea baada ya siku
nane ya ufunuo kuhusu mateso, kufa na kufufuka kwake na mwaliko wake kwa
wanafunzi wa kumfuata kulingana na njia yake mwenyewe, yaani “Kujikana
mwenyewe, kuuchukua msalaba wake na kumfuata Yesu.” Habari ya kugeuka sura kwa
Yesu tena inafuatwa na tangazo la pili kuhusu kifo na ufufuko wake.
Kwa uzoefu huu Yesu aliwachukua wanafunzi watatu,
Petro, Yakobo na Yohana. Kwa nini wafuasi hawa? Labda kwa sababu aliwapendelea
kuliko wengine. Injili haiongei maana ya habari hii. Yesu aligeuka mbele ya
wafuasi wake na ishara kuu zilikuwa nguo na mwili wake. Yesu aliwaonyesha
kidogo utukufu wake na hali ya wakati ujao kuhusu mwili wa yeyote anayemfuata
kwa uaminifu. Yesu anashiriki utukufu wake na wanafunzi wake kwa maana inampendeza
kufanya hivyo ili wawe na furaha moja ya vile Mwalimu wao alivyo.
Kama illivyotokea kuhusu jangwa, Mlima pia ni mahali muhimu
katika uhusiano wa Watu wa Israeli na Mungu; katika mwendo huu, Musa na Eliya
wana ushiriki maalum. Katika Agano la Kale milima
iliyojulikana sana ni Mlima Sinai na Horebu. Ilikuwa katika Mlima Sinai ambapo
Mungu alikutana na Musa na kuwawekea Waisraeli agano. Ilikuwa katika Mlima
Horebu ambapo Eliya alijiandaa kwa muda mrefu akutane na Mungu. Katika Agano
Jipya Yesu alitumia sana mahali huko mlima kama rejeo la uhusiano wake na Baba
na kama eneo la matukio muhimu katika kazi yake. Kulingana na utamaduni mmoja wa zamani, tukio la injili ya siku ya leo
lilitokea juu ya mlima Tabor.
Uwepo
wa Musa na Elia unaongea kuhusu rejea la ufunuo katika Agano la Kale. Waliongea
na Yesu wakionyesha kwamba hakuna usumbufu kati ya mafundisho yao na mafundisho
ya Yesu, bali uhusiano na mwendelezo. Lakini kulingana na sauti iliyosikika
kutoka kwenye wingu, mwendelezo huu, ambao ni Yesu, lazima kuwa kipaumbele
katika maisha ya wanafunzi kwa sababu ni Yesu peke yake kwa mamlaka aliyoyapokea
kutoka kwa Baba ili kufundisha na kutafsiri kamili lile lililosemwa na mababu wa
zamani.
Kusikiliza
katika Biblia ni kitenzi chenye nguvu sana. Hii ni tabia ya myahudi mbele ya
Neno la Mungu, akiweka vitendoni yale aliyosikia. Kusikiliza kuna uhusiano na
kushika au kutenda. Baba anashuhudia kuhusu Mwana wake, anamweka kama rejeo la
maisha yetu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, msikilizeni”. Huu ni pia mwaliko ili tufananishe
maisha yetu kulingana na Neno la Yesu. Neno la Yesu ni kipimo ili mtu awe pia mwana
mpendwa wa Mungu kama Yeye. Tunashiriki katika kugeuka sura kwa Yesu kupitia
kusikiliza makini kwa Neno lake.
Kuhusu
mambo hayo Mtakatifu Yohana Calabria alisema: sisi ni makini sana kwa maneno ya
binadamu na kuhusu hiyo ni sawa. Lakini tunapaswa kuwa na uangalifu zaidi kwa
Neno la Mungu ambalo huweka wakfu, yaani linalifanya lile linalosema.” Mtakatifu
Yohane Calabria alikuwa anasema hasa kuhusu injili ambayo ni sheria ya Shirika
la Poor Servants of Divine Providence. Katika sehemu nyingine ya maandiko yake Mt.
Calabria alisema: “Ikiwa sisi huamini katika maneno ya Kuweka wakfu –
Consecration - katika misa, yaani “twaeni mle wote, twaeni mnywe wote”,
tunapaswa kuamini pia wakati Yesu asema: “Msiwe na wasiwasi” au “Baba yeno wa
mbinguni anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote” au “mtafuteni kwanza ufalme
wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada.” katika maneno
mengine, kutokana na Maneno ya Yesu tunaalikwa kuwa “Injili hai.” Hiki ni
kipimo ili tuweze kuutambua uso uliogeuka wa Yesu katika nyuso zenye mateso za
ndugu zetu mwetu.
Wanafunzi
walitamani kubaki mlimani, lakini sauti iliyotoka mbinguni ikawaalika
kumsikiliza Yesu na kutoka nje ya uzoefu huu wamepatikana kuandamana naye mpaka
upeo. Mara nyingi Mungu ametualika kufanya uzoefu wa uwepo wake kama
ilivyotokea kwa wale mlimani, mfano, wakati tunaposhiriki katika sherehe fulani
ama siku za maombi, uzoefu wa undugu na kadhalika. Uzoefu kama huu unaiimarisha
imani yetu na hamu yetu kwa ajili ya kazi ya Mungu. Lakini safari yetu yapaswa
kutendeka kati ya “kupanda mlimani” (mfano wa uzoefu wa Mungu wa kibinafsi) na
“kushuka mlimani” (mfano wa changamoto za undugu na kazi). Kila siku tunaalikwa
kufanya uzoefu wa “kugeuka sura” tena na tena kwa kusikiliza Neno la Yesu na
kufanya mazoezi kuhusu Neno hili. Uzoefu huu unatusaidia kutambua uso wa Yesu
katika nyuso za ndugu wengi kandokando yetu na kuona hisia na tabia sawasawa na
zake kwa ajili yao. “Kusikiliza neno lake kunatupatia nguvu ya kumfuata mpaka
mwisho.” Hii ni njia kamili ili tuweze pia kuishi kama “wana wapendwa” wa
Mungu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário