Kutafakari kutoka 1 Waf 17, 10-16; Waeb 9, 24-28; Mk 12: 38-44
Muhimu ya tafakari yetu ni neno ukarimu kama tabia ya kimsingi wa mwamini. Mungu
hajiruhusu kushindwa katika ukarimu. Yeyote anayetenda kwa ukarimu kwake
hupokea kwa ziada. Uzoefu huu upo sana katika maisha yetu ya kila siku nao
unadhihirika sana katika maisha ya wajane wawili wanaowasilishwa na liturujia
ya leo.
Katika
andiko la kwanza, Eliya alitumwa kwa mjane huko Sarepta. Mkutano na mtu huyo wa
Mungu uliyafanya matarajio ya maisha ya mama mjane huyo na mtoto wake yabadilishe
kabisa. Hao walikuwa wanaishi mazingira magumu sana, yaani: “tuweze kula na
kufa”. Jibu lake la ukarimu kwa ombi la nabii linaonyesha tabia ya kuamini katika
riziki ya Mungu ambaye hakuna kisichowezekana. Mwishoni muujiza ulitokea kwa
njia ya ajabu. Sisi twalikwa kuwa na tabia hii ili tendo la neema ya Mungu
maishani mwetu liwe ufanisi.
Kifungu
cha waraka wa Waebrania kinaongea kwamba Kristo alibatilisha dhambi kwa
kujisalimisha mwenyewe msalabani. Hili ndilo fumbo ambalo ametuokoa nasi tunahisi
kwa njia mpya katika kila Ekaristi ambayo tunasherehekea. Hili si tukio la kihistoria
tu bali ndiyo nafasi ya kushiriki katika maisha ya Kristo mwenyewe ambayo inatualika
kuendelea kazi yake kwa kuyatoa maisha yetu kama yeye alivyo.
Sehemu
ya kwanza ya Injili inajulisha upinzani wa Yesu dhidi ya njia ya waalimu wa
sheria ya kuishi. Hao wanapenda sana kujiinua na kupendezwa. Wanasali kwa muda
mrefu lakini bila kusudi kamili. Wanajihisi bora kuliko wengine na kudhulumu
wajane. Yesu ana wasiwasi kuhusu njia hii ya unafiki kwa sababu inalipinga pendekezo
lake kwa wanafunzi wake.
Watu walijua
kwamba kuna tofauti hasa mfarakano kati ya mafundisho ya Yesu na ya waalimu wa
sheria. Yesu aliwafundisha watu kwa mamlaka aliyopokea kutoka kwa Baba. Kuhusu
mamlaka ya walimu wa sheria, yakosa ukweli. Baada ya uhuru kutoka utumwani
Babeli walimu walikuwa viongozi muhimu kwa ajili ya Wayahudi kwa sababu
waliandika Vitabu Vitano via mwanzo wa biblia vinavyojulikana kama Vitabu vya
Musa, yaani Toraa na hao peke yao waliweza kuhukumu na kujulisha sentensi
kulingana na sheria. Hao waliwasisitiza Wayahudi kuzingatia agano kwa kuzishika
sheria za Mungu kama msingi wa taifa lao jipya. Lakini ingawa waliwafundisha
watu waishi sheria, tabia yao ilikuwa mbali sana na mafundisho yao.
Utumiaji
mbaya wa mamlaka ni majaribu daima katika maisha ya walio na jukumu la
kuwaongoza watu katika jumuiya zetu za Kikristu na pia katika jamii. Lakini sio
hao tu ambao wanaguswa na majaribu haya. Hata sisi pia tuko na mwelekeo huu. Majaribu
ya kawaida ni yaani kujiona bora kuliko wengine, kutaka kutumikiwa badala ya
kutumikia, kuwanyonya wengine na kadhalika. Yeyote ambaye anataka kuwaongoza
wengine anapaswa kuiga mfano wa Yesu aliyekuwa na mawazo tofauti na kujua njia kamili
ya kushinda majaribio yote. Hatuwezi kumpendeza Mungu wala kuwa wenye furaha
ikiwa hatuishi majukumu yetu kama utumishi.
Lakini
katika sehemu ya pili ya injili hii tuko na njia kamili ya kuwa mwanafunzi wa
Yesu, yaani mfano wa mama mmoja mjane maskini aliyeenda hekaluni kutoa sadaka
yake. Yesu alikuwa ameketi karibu na sanduku la hazina pamoja na wanafunzi
wake. Alitazama jinsi watu walivyoweka pesa sandukuni. Yeye aliweza kuona moyo
na kusudi kwa kila mmoja alipotoa sadaka. Alipotazama mjane akiweka fedha
sandukuni yeye alitambua kwamba mama huyo alitoa zaidi kuliko wengine kwa
sababu sadaka zao zilikuwa ziada ya matajiri bila kusudi kamili kwa moyo. Sadaka
ya mjane ilimpendeza Mungu kwa sababu alitoa kila alicho nacho cha kuishi,
yaani alitoa maisha yake kama zawadi, kama sadaka.
Mama
mjane maskini hakumjua Yesu, lakini alimpendeza kwa sababu alitenda kulingana
na pendekezo la binadamu mpya. Mtu anakuta
maana ya kweli ya maisha wakati anapoweza kutenda kama Mungu katika ukarimu
wake, yaani zaidi kuliko kutoa kitu, mtu anaweza kujitoa mwenyewe kama sadaka
yote kwa kuonyesha kwamba maisha yake ya kila siku yanamtegemea Mungu. Tuko na
tabia ambayo inadhihirisha ukuu wa moyo wa mtu fulani.
Tunaalikwa
kwa macho kwa ishara halisi ndogo zinazotoka kwa watu unyenyekevu tunaowakutana
kwa kawaida na kujifunza kutoka kwao tabia kamili mbele ya Mungu. Yeye hupendezwa
sio na wingi wa vitu ambavyo tunatoa bali na ukarimu wa moyo wetu. Thamani ya sadaka
yetu hupimwa kulingana na ukarimu wetu. Ukuu wa mtu hautokana na kipimo cha
zawadi ambayo anatoa bali na uzuri wa ishara yake na upendo wake. Kweli, ndizo
ishara ndogo zinazofanya tofauti. Msaada mkubwa ambao ninaweza kumpa wengine
ndimi ninayealikwa nilivyo. Zaidi ya hilo ndio unafiki ambao unanizuia kuwa na
uhusiano mwema na wengine. Tunaweza kushinda hali mbaya hii kwa msaada wa watu
wanyenyekevu ambao wanajenga undugu kandokando yetu na kuwa maonyesho ya
ukarimu wa Mungu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário