Kutafakari kuhusu Dan 12: 1-3; Waeb 10: 11-14; Mk 13: 24-32
Tuanze tafakari hii tukijiuliza swali moja: “Je, Wakristo wanapaswa kuwa na
tabia gani wakati wa mazingira magumu na mbele ya kosa la uhakika lililo tabia
ya wakati huu wetu? Sisi tu watu wa tumaini kwa sababu maisha ya mtu anayemfuata
Yesu yamejaa maana. Basi, ujumbe wa liturgia hii ni msukumo kwetu tulioalikwa kutoa
maana za tumaini letu kupitia imani yetu katika Kristo. Uhakika wa ukaribu wake
ndiyo nguvu yetu. Tukikumbuka kwamba leo ndiyo Siku ya Maskini Duniani, tujaribu
kuwa kidugu na wenye mshikamano, tukiwafikiria wengine kuliko sisi wenyewe.
Kulingana na Papa Francis, "umaskini si tunda la hatima bali ni matokeo ya
ubinafsi". Hivyo, hakuna mtu anayeweza kusema: "Hali hii haina
uhusiano wowote nami”.
Somo la nabii Danieli ni mojawapo kati ya maandiko ya Agano la Kale yanayoongelea
imani katika ufufuko (angalia pia 2 Mac 7, 9). Watu wa Israeli walitumwa na Wagiriki
na kuteseka sana. Wengi miongoni mwao walishindwa kumwamini Mungu, lakini
wengine ambao waliendelea kumwamini walihitaji ujumbe wa tumaini na kutia moyo
ili kuendelea safari yao kwa uvumilivu. Mungu ndipo daima kati ya watu wake na
kuwasaidia mbele ya mazingira magumu ambayo wanakabiliana. Ufufuo ulioahidiwa ulitimizwa
kwa ufufuo wa Mwana wake kutoka kwa wafu, kama wa kwanza ya wengi wa ndugu na
dada.
Kulingana na somo la pili toleo la Kristo lilishinda dhabihu zote za
makuhani wa Agano la Kale. Dhabihu zao zilitendeka mara nyingi bila nguvu ya
kuondoa dhambi za watu, yaani zilikosa ufanisi. Kwa upande wa Kristo, hali ni
tofauti. Toleo lake lilitendeka mara moja tu nayo ilitosha kwa kuwatakasa watu
wote katika nyakati zote kwa sababu alijitolea mwenyewe. Katika kila misa
takatifu tunasherehekea fumbo la toleo hili. Ndiye Kristo mwenyewe ambaye
anatuhusisha katika mwendo huu kwa ajili ya wokovu wetu na wa wengine.
Mwanzoni
mwa sura ya kumi na tatu ya injili hii ya Marko Yesu aliongelea uharibifu wa
Yerusalemu. Ufunuo huu uliwaimarisha wanafunzi wake wamwulize kuhusu ishara
gani na siku na saa gani ya uharibifu huu. Kisha, Yesu alitumia nafasi hii ili kuongelea
mambo mengi yatakayotokea kuhusu historia na kuhusu utume wa jumuyia ya
wanafunzi iliwekwa naye. Yeye Atarudi tena mara ya pili kwa ajili ya ukamilifu
wa uumbaji na kuwakusanya mataifa yote karibu naye. Hivyo, “mpago wa Mungu unatimiza:
kufanya Kristo awe moyo wa ulimwengu”.
Mbele ya
udhihirisho mtukufu wa Kristo “nguvu za mbingu zitatikiswa”. Hali hii
inamaanisha kwamba miungu ya uongo, yaani jua, mwezi, itapoteza mwanga wao.
Hata wale waliojiona watu wa kimungu (nyota za angani) ambao wanawatesesha watu
wa mataifa hasa walio maskini, hao (miungo ya uongo) wataanguka na mtazamo wa
wote utamwelekezea Mwana wa Mtu akija amejaa nguvu na utukufu kama mshindi. Hakuna
mtu anayejua wakati kamili ambao mambo yote yatatokea ila Baba peke yake. Kwa
hivyo ni lazima kumwamini yeye.
Ingawa
uharibifu wa mji wa Yerusalemu ulitokea katika mwaka wa 70 B.K., nia ya Yesu
haikuwa kuwajulisha kuhusu tukio hili, bali kuhusu matokeo ya tukio hili
maishani mwa wafuasi wake. Ni lazima kutafakari injili hii kulingana na mazingira
ambayo jumuiya ya Marko ilikuwa inaishi, yaani wanafunzi wa Yesu waliishi
kipindi cha machafuko na kujaribiwa kukata tamaa kuhusu utambulisho wao wa wafuasi
wa Yesu kwa sababu ya majaribio na mateso mengi. Kweli ulionekana mwisho wa
dunia. Wale ambao walidumu kwa imani walijiuliza: “hayo yatokeayo yamaanisha
nini?”. Kumbukumbu ya mafundisho ya Yesu ilikuwa muhimu sana kwa kuchukua tena
lile ambalo liliwapa maana kwa maisha yao. Walikuwa na uhakika kwamba ikiwa ni
Yesu kipimo cha kila jambo na lengo la historia, hivyo maisha na historia haziongozwi
kwenye mwisho fulani bali kwenye lengo kamili: Yesu Kristo mwenyewe.
Yesu ni
mshindi juu ya dhambi na kifo na atawafanya wote wanaomfuata wawe washindi.
Wakati wa kuja kwake katika mwisho wa nyakati (utimizaji wa nyakati) anataka kutukuta
sisi "wavumilivu na macho", waaminifu kwa mafundisho yake ili tushiriki
naye furaha yake mwenyewe. Neno lake linatuambia kwamba majaribu na magumu ni
sehemu ya hali yetu kama Wakristo, lakini pia linatuhakikishia ukaribu wa
Bwana: "Tambueni ya kuwa Yeye yu karibu, yu karibu milangoni! (Mk 13, 29)."
Anataka tu kutambuliwa na kukaribishwa. Kwa kuwa sikuzote hatuwezi kuelewa
matukio yanayotuzunguka, ni lazima tuwe na imani katika Baba, tukitambua kwamba
“tuko mikononi mwake na kwa hiyo, tuko mikononi mwema. Hakuna kinachofikiwa na
macho yake. Kila jambo linalotokea linaelekezwa kulingana na mpango wake
mwenyewe wa hekima na wema” (Mt. Yohane Calabria).
Basi kwa
upande wetu tumwaminie Yule ambaye anaiongoza historia.Sisi tulioalikwa kuendelea
utume wa Mwana wake Yesu, tunapaswa kuwa macho kwa ishara za uwepo wake ambazo
zimetokea kati yetu. Ili hali mpya ikatokee maishani mwetu, miungu mingi ya uongo
yapaswa kuanguka na kupoteza thamani yao. Kwa maneno mengine, tunapaswa kuacha
picha za uongo za Mungu, mawazo na tabia ambayo inayapinga mafundisho ya injili.
Tuishi wito wetu kwa shauku na furaha kwa sababu kuna tumaini kwa wakati ujao
wetu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário