Kutafakari
kuhusu Am 6, 1a. 4-7;
1Tm 6, 11-16; Lk 16,
19-31
Mungu analaumu kila kutojali na unafiki kati ya watu wake. Kama anatamani
wawe na furaha kamili na maisha mengi, yeye anapendekeza njia kamili ya kuishi.
Kulingana na somo la kwanza, nabii Amosi anatusaidia kufahamu kwamba hali
mbaya ya utumwa katika safari ya Waisraeli haikuwa adhabu ya Mungu bali matokeo
ya uamuzi ya kuishi mbali sana naye. Nabii huyo anashutumu njia ya kianasa ya
wakubwa ambayo inajaa udhalimu na kosa la undugu kati ya watu. Hali hii mbaya ya
kuishi ilivutia utumwa kwa maisha yao. Wakati mwafaka Mungu ataonyesha upendo
wake hasa kwa ajili ya wadogo na ya maskini. Maisha ya kianasa na ya wingi mtu
anayoishi yaweza kuwa kikwazo ili awe na macho mbele ya hali ya walio na shida.
Kipimo cha uhusiano mwema na Mungu na kupata furaha kamili ni hisia ya kindugu.
Somo la pili linaonyesha shauri ya Mtakatifu Paulo kwa Timotheo na kwa kila
Mkristo. Andiko linaanzwa hivyo: “Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo
hayo”. Ni kuhusu mambo gani? Ndiyo mambo ya kila namna ya kupenda fedha ambayo
anaharibu imani na kuvutia kila namna ya maovu.
Haitoshi kuwa na jina la Kikristo ili kuwa mwanafunzi wa kweli wa Yesu.
Mtakatifu Paulo anatualika kufuata njia ya haki, utauwa, imani, upendo,
uvumilivu na upole.
Yesu anasimulia mfano wa mtu tajiri na Lazaro maskini anawaonya
wasikilizaji wake kuhusu hali ijayo iliyo matokeo ya chaguzi za watu katika
wakati huu. Kwanza kabisa ni lazima tufahamu kwamba kuzimu iko bali kuna pia
peponi. Sio wote wa matajiri wataenda kuzimuni na sio wote wa maskini wataenda
peponi. Mwelekeo wa maisha ya mtu utakuwa kulingana na njia ambayo alichagua
kuishi na tabia mbele ya vitu vya dunia. Yesu anafundisha tabia kamili.
Basi, palikuwa na mtu mmoja tajiri na Lazaro maskini. Mtu wa kwanza ni
ishara ya walio na mazoea ya kuitumainia mali bila kuguswa na hisia kuhusu kile
kinachotokea kandokando yao. Hao walichagua kwa nafsi yao njia ambayo itawaongozea
mauti. Lazaro ni ishara ya walio maskini ambao wameachwa bila ulinzi na utunzaji;
wanapiga kelele ili wapate nafasi ya kuishi kwa heshima. Tena Lazaro ni pendekezo
la kuishi tofauti, kuyalenga maisha katika thamani za kweli. Huyo ni ishara ya
uvumilivu, ya mapigano na mwaliko wa kumtumainia Mungu ambaye katika riziki
yake hawaachi wale ambao wanamwamini.
Kupitia mfano huu
Yesu anatukumbusha kuhusu hali mbaya ambayo ipo katika jamii yetu, yaani kosa la
usawa kati ya watu. Katika mafundisho yake, Kanisa limeshutumu hali hii mara
nyingi kwa kusema, “Hali mbaya ya kijeuri imezaa matajiri mno daima na tena kwa
upande mwingine imezaa maskini mno daima.” Hali hii ni dhidi ya mipango ya
Mungu anayefanya mvua inyeshe kwa wenye haki na wasio na haki, tena kwa walio wema
na kwa wabaya ili vitu vyote alivyoumba kwa wote tena vipatikane kwa wote.
Mfano mzuri kuhusu
hayo tunapata katika Wimbo wa Bikira Maria ambao unaishuhudia njia ya ajabu ya
Mungu ya kutenda, yaani yeye huwashusha wakuu na kuwapandisha wadogo ili waweze
kuishi pamoja kama ndugu na kwa usawa wa haki na wa heshima. Mungu
anajitambulisha na hali ngumu ya wasio na nguvu na ya maskini. Udhalimu wote
unaofanyika kwao unamgusa Mungu ambaye anasimama katika upande wao.
Katika wakati ujao, baada ya hali ya dunia, hali itakuwa tofauti kabisa,
yaani waliopokea mambo mema katika maisha yao bila ahadi na hisia kuhusu hali
ya walio na shida hawatakuwa na hali nzuri kwa maisha yao. Kwa upande wa wale
waliopata mabaya kama Lazaro alivyo, watafarijiwa. Yeyote ambaye anatumia mali
yake ili kuwadharau wengine anatupa maisha yake takatakani kwa sababu maisha ya
kweli hayamaanishi kuwa na mali mengi bali kuwa na uwezo wa kutenda mema. Mtakatifu
Yohane Calabria asema: “Maskini wako ili matajiri waokolewe”.
Hali ya maskini inatuhusu sote, kwa sababu “dhambi ya kijamii ni matokeo
ya kiasi cha dhambi za kibinafsi”. Basi, ni lazima mabadiliko sio tu kuhusu dhambi
za kibinafsi, bali pia kuhusu dhambi ya kijamii. Mwendo huu unaweza kwanza
kupitia tabia ya kuacha njia ya ukusanyaji ambayo kwa kawaida inatuongoza kuwa
na kutojali kuhusu hali ya wengine. Vitu tulivyo navyo ni zawadi za Mungu. Tunaalikwa
kuchukua njia ya unyenyekevu kwa kuepuka matumizi ya vitu vya bure na kuwa na
hisia kuhusu wale wasio navyo. Mungu anatuokoa maana ya upendo wake, lakini
anathamini sana juhudi zetu kama alivyosema Baba Mtakatifu Benedito wa kumi na
sita: “kwa kweli, wokovu ni zawadi iliyo neema ya Mungu, lakini ili uwe ufanisi
katika maisha yangu unadai ridhaa yangu, ambayo inaonyeshwa kupitia matendo,
yaani kupitia utayari wa kuishi kama Yesu alivyo kwa kuufuata mfano wake.”
Fr Ndega