Kutafakari
kutoka Mdo 15,1-2.22-29; Ufu 21, 10-14.22-23; Yoh 14, 23-29
Ujumbe
muhimu wa maandiko haya ni kuhusu uwepo na makao ya Mungu ulimwenguni na ndani
ya kila mtu kupitia upendo. Hali hii inatualika kufanya upya ahadi zetu za
waliobatizwa na kuboresha uhusiano wa kweli na yule ambaye anapendezwa kukaa
ndani yetu.
Hali
ya somo la kwanza inaongea kwamba mwanzoni mwa kuinjilisha wanafunzi wa Yesu
walihitaji utambuzi sana watangaze habari njema ya Yesu bila kipimo na masharti.
Baadhi ya desturi za binadamu ni kama mzigo katika uhusiano wa watu na Mungu. Mazungumzo
ya Paulo na Barnaba pamoja na mitume wengine wameongozwa na Roho Mtakatifu ni
mfano wazi kuhusu njia ya Kanisa ya kutenda ili liweze kutatua shida na magumu miongoni
mwa wana wake kwa sababu ya tofauti ya tamaduni, ya mawazo na kadhalika. Matokeo
ya mwendo huu ni kutia moyo kupitia waraka wa mwongozo kwa ajili ya jumuiya na ya
kujenga mwili mzima. Kulingana na mtazamo wa Yohana, Mungu alifanya makao
duniani na kupitia Yesu, aliye hekalu la kipekee tunaloweza kukutana na Mungu
kwa kweli. Lengo la safari yetu kama Watu wa Mungu ni kushiriki katika utukufu
wake na kutia nuru kupitia Mwana wake aliye mwanga wa ulimwengu.
Katika
injili tuko na hotuba ya kuaga ya Yesu anayewashauri wafuasi wake walishike
neno lake kama alama ya upendo wao kwake. Wanafunzi wana maana nzuri ya kufanya
hivyo kwa maana hiyo ni njia maalum ya kuwa makao pa Mungu. Uhusiano wa
ushirika kati ya Mwana na Baba na Roho Mtakatifu sio kufungwa bali ni mwaliko
wa ushiriki wa wale watakaoendelea kazi ya Yesu ulimwenguni. Kipimo cha mwendo
huu ni neno lake linalo asili katika Baba na linapatikana kwa wote kupitia tendo la Roho Mtakatifu. Roho
huyo ni Msaidizi anayeweza kubadilisha maisha ya yeyote anayejifungua kwa neno la Yesu. Wanafunzi
wanaalikwa kuishi hatua mpya katika safari yao na maneno haya ya Yesu ni faraja
inayotoa ujasiri ili wapate kushinda kila hofu.
Yesu
hakuwaacha kama walio yatima. Yeye atatoweka kwa kimwili lakini ataendelea kuwepo
miongoni mwao kupitia upendo. Mahali ambapo Yesu yupo vivyo hivyo Baba na Roho
Mtakatifu wapo. Ikiwa mara iliyopita (Yoh 13, 31-35) tulitafakari kuhusu haja
ya kupendana kama Yesu alivyopenda, sasa muhimu ndio upendo wao kwa Yesu aliye
njia ya kweli ya kumkutana na Mungu. Yeye, pamoja na Baba na Roho Mtakatifu wanakuja
daima kwetu na kutarajia kukaribishwa vizuri. Ujio wao maishani mwetu ni
ufanisi sana, kulingana na Baba wa Kanisa Gregori, yaani, “wanakuja kwetu
twende kwao; wanakuja kusaidia wakati wa dhiki; tunakwenda kwao kwa kutii;
wanakuja kwa kutuelimisha, tunawaendea kwa kutafakari; wanakuja kwa kutujaza,
tunawaendea kwa kushikilia; ufunuo wao si wa nje bali wa ndani; makao yao kwetu
si ya muda bali ya milele. Imesemwa tutakuja kwake na kufanya makao kwake.”
Yesu
anaongea kuhusu Baba kwa hamu na kutambua sana msaada wa Roho Mtakatifu katika
kazi yake. Huu ni mwaliko wa tuishi uhusiano mpya miongoni mwetu hata tufikirie
wengine muhimu kuliko sisi wenyewe na tena kutambua kazi yao muhimu kuliko
zetu. Ufunuo wa Yesu unaleta changamoto kwetu tulioalikwa kuendeleza kazi yake.
Anataka kwamba kupitia maneno na matendo yetu dunia ikamjue. Bila shaka kwamba tunapaswa
kuwa waaminifu na mwendo huu ni matokeo ya kulisikia na kulishika neno lake. Tendo
hili ni kipimo cha upendo wetu kwake. Tunaweza kufanya hili kwa sababu alikuwa
yeye aliyetupenda kwanza na kuja kwetu. Wakati tunalishika neno lake Yesu tunaruhusu
kuingia kwa Utatu Mtakatifu ndani yetu. Tunajua kwamba hali hii ni kweli tangu
ubatizo wetu, lakini sio daima tumeishi kulingana na uwepo huu. Tuchukue nafasi
hii ili kufanya mpya urafiki wetu na uwepo huu maalum ndani yetu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário