kutafakari juu ya Lk 19, 28-40; Is 50,4-7; Waf
2,6-11; Lc 22, 14-23, 56
Tunaingia katika wiki muhimu sana kwa Jumuiya
za Kikristo. Hii ni wiki inayojumuisha matukio makuu ya imani yetu, ikieleza
kwa ishara nyingi na kwa kina vipindi vya mwisho vya maisha ya Yesu kama
binadamu hapa duniani na kutualika kwa shukrani na kutafakari. Hii ni pia nafasi
ya kufanya upya ahadi yetu kama wafuasi wa Yesu na kujiruhusu kuimarisha kwa mifano
yake ya uaminifu na uamuzi.
Tunaalikwa kumfuata Yesu anayeingia kama mshindi
katika Yerusalemu ili kukamilisha kazi yake ya upendo. Kwa kweli, hakuja juu ya
farasi kwa kiburi na kwa jeshi yenye nguvu kama walivyofanya majenerali wakiingia
mijini, lakini amepanda punda, na kuja kwa wema na rehema kama imetokea wakati
wa maisha yake yote. Yesu anajua sana nini itatokea nawe, hata hivyo hakukata
tamaa. Kinyume, anaonyesha uhuru wa Mwana mpendwa aliyepelekwa kuwaokoa
wanadamu. Pamoja na kukumbuka kuingia kwake katika “Mji wa amani”, tunakumbuka pia
mateso na kifo chake katika mji huu ulio na mazoea ya kutenda kwa ukatili dhidi
ya wajumbe wa Mungu. Hivyo, kifo chake sio hatima, bali matokeo ya kazi ya kinabii
aliyeishi kwa uaminifu hadi upeo.
Kama tunavyojua, nabii Isaya anatoa nyimbo nne
ili kuongea juu ya utambulisho na kazi ya Watu wa Mungu, wanaoitwa pia
“Mtumishi wa Mungu.” Nyimbo hizi ziliandikwa wakati wa utumwa wa Babeli nasi
tunaweza kuzipata katika sehemu ya pili ya Kitabu cha Isaya. Andiko tunalotumia
hapo unafahamika kama ‘wimbo wa tatu’ na kulingana na wimbo huu, mtumishi
anaishi wito wake kama zawadi inayotoka kwa Mungu kwa ajili ya kutoa maisha
mapya kwa ndugu zake. Kwa sababu ya uaminifu wake, aliaibishwa, alikataliwa na kuteseka
sana, lakini hakukata tamaa kwa sababu aliona ukaribu na utunzaji wa Mungu. Mtumishi
huyo ni mfano wa Yesu ambaye kwa utambulisho wake na hali ya binadamu, alijinyenyekeza,
akaaibishwa, akateseka na kuuawa maana ya uaminifu wake kwa Mungu. Amini yake ya
mwana katika Mungu ndiyo maana ya uaminifu wake. Kwa njia ya kujifanya upole aliupata
utukufu. Njia ya unyenyekevu, ya ishara ndogo na ya kuchagua kinachoonekana
bila maana kwa jamii ndizo tabia za wale wanaoendelea kazi yake.
Yesu aliachwa na marafiki zake, lakini yeye
hakuwako peke yake msalabani wala wakati wa kazi yake. Maneno yake mwenyewe yanashuhudia
kuhusu hayo, yaani “Yule aliyenituma yuko pamoja nami, hakuniacha peke yangu,
kwa maana mimi nafanya yanayompenda yeye (Yoh 8.29).” Hivyo “kilio” ambacho
Mathayo anaweka mdomoni mwa Yesu kinapaswa kufahamika kwa uhusiano na
kujisalimisha kwake mikononi mwa Baba, kulingana na toleo la Luka, iliyo tabia
yake daima, yaani “Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu (Lk 23,46).”
Vinginevyo, tungekuwa kukana sio tu kazi yake kwa ushirika na Baba bali pia uaminifu
wa Baba huyo.
Fumbo la mateso na kifo cha Yesu halionyeshi
uchungu kama jambo la kwanza kwa kutafakari bali upendo wake mkubwa hadi upeo. Kwanza
ya kuwa mateso ya uchungu ni mateso ya upendo. Kwa sababu hiyo mwinjilisti Luka
aliweka tukio la Ekaristi kama utangulizi wa simulizi yake. Kifo hakikuwa kulazimishwa
kwa Yesu, bali jambo ambalo yeye alikubali kwa hiari. Yesu alijua kwamba
alikuwa akifanya jambo sahihi na hivyo mateso yake ni mwanzo wa ushindi wake
juu ya mauti, akifufua matumaini yote ya maskini na ya wanadamu wakosefu.
Mateso ya Mwana wa Mungu yanatualika kutafakari
kuhusu hali ngumu ya mateso ya binadamu. Kama Mungu alijibu kwa ufufuko mbele
ya kifo cha Mwanawe, tunaweza kuhitimisha kwamba Mungu hataki mateso wala mauti
ya watu. Yeye hawaachi wale wanaoteseka wala hanyamazi mbele ya mateso yao.
Kristo alichukua kwa nafsi yake uchungu wa watu wote wa nyakati zote. Yeye
anaendelea kuteseka wakati sisi tunahisi maumivu na majaribio katika safari
yetu. Mfano wake unatuimarisha tuwe na kuwepo ufanisi maishani mwa watu wanaoteseka
zaidi kuliko sisi. Misalaba ya mshikamano na huruma tunayoitwa kuchukua kila
siku kama yeye alivyo inafanya kwamba kujitolea kwetu kuwe ishara ya upendo pia
kama ushiriki katika mateso yake kwa ajili ya wokovu wa watu wote.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário