Kutafakari kuhusu Lk 13, 22-30
Wakati wa safari ya
kwenda Yerusalemu, Yesu alitumia nafasi ya kuwafundisha wanafunzi wake hasa
kuhusu masharti ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwanza kabisa haitoshi
kuwa wanafunzi wake ili kupata wokovu. Hivyo, aliwapendekezea mlango mwembamba
kama changamoto. Ikiwa Yesu anajulisha mlango mwembamba ni kwa sababu pia kuna
mlango mpana. Wakati Mt. Yohane Paulo wa II alipoongea na vijana katika mwaka
wa 1993, alitofautisha vizuri njia hizi mbili, akisema: “kataeni barabara
rahisi: barabara ya anasa, uhalifu, kudharau mazuri, na kukwepa wajibu. Ulevi
na matumizi ya madawa ya kulevya na uasherati visiwe na nafasi katika maisha
yenu. Pitieni mlango mwembamba. Chagua barabara ielekeayo kwenye uzima wa milele
na furaha pamoja na Mungu.” Katika kifungu kingine Yesu alisema kwamba mlango
mwembamba ni njia ambayo inaongoza kwenye uzima na wachache tu wanaoweza
kuigundua njia hiyo. “Huu ni mlango wa uvumilivu, busara, kujitoa, ukarimu,
wema, shukrani na kazi”. Kuhusu mlango mpana, hii ni njia rahisi inayoongoza
kwenye maangamizi na waendao njia hiyo ni wengi. Basi, ili wanafunzi wa Yesu
waweze kupata mafanikio katika safari yao wapaswa kupitia mlango mwembamba.
Katika mazingira
yetu mlango mwembamba ni ishara ya juhudi yetu ya kushinda mwelekeo mbaya wa
maisha yetu na kuwatendea watu mema. Katika mwendo huu ndio sisi wa kwanza wa
kupata mafanikio ama bahati mbaya, kwa sababu lile tunalofanya kwa ajili ya
wengine linasababisha hali nzuri ama mbaya kwetu pia. Hadithi fulani
inatusaidia kuelewa vizuri hali hii. “Siku moja mwandishi wa habari alimhoji
mwenye shamba ambaye ameshinda mara ya tano mashindano kuhusu mahindi mazuri
zaidi katika eneo hilo. Mwandishi alimwuliza swali akisema, “unapataje kuzaa
mahindi bora kuliko wengine?” Mwenye shamba alijibu, mwendo huu ni rahisi sana;
nina mazoea ya kushiriki mbegu zangu nzuri na majirani wangu.” Mwandishi
aliendelea kwa swali akisema, “Kwa nini unashiriki mbegu zako nzuri na majirani
wako ikiwa hao wanashindana pia katika mashindano haya pamoja?” “kwa sababu ni
upepo ambao unasambaza poleni ya mahindi na tena ni upepo ambao unaweka poleni
mashambani na unafanya mbegu zikue. Ikiwa majirani wangu watakuwa na mahindi
mabaya, upepo utasambaza poleni mbaya shambani kwangu nayo mahindi yangu
yatakua mbaya. Basi ili mahindi yangu yawe mazuri ninapaswa kuwasaidia majirani
wangu wote ili wawe na mbegu nzuri.”
Basi, lile zuri ambalo
tunatarajia kwa maisha yetu tunapaswa kusaidia kwa ajili ya wengine. Katika
mwendo huu hatuwezi kuitafuta furaha kwa njia ya ubinafsi. Ikiwa tunataka kuwa
wenye furaha, tunapaswa kuisaidia hali hii nzuri kwa wale wanaoishi karibu nasi
nao wako na shida sawa nasi. Tunapaswa kushinda mwelekeo wa jamii wa kufikiria
wengine kama washindani nasi. Wengine sio washindani, bali ndugu. Kujaribu
kupata upendeleo tukiwavuruga wengine ni udhalimu na kutuacha mbali sana na
matarajio ya Yesu. Ikiwa tuko mbali na matarajio ya Yesu, matokeo yatakuwa
mbali sana na yale tuliyotarajia kwa maisha yetu. Tunaweza kuongea vizuri sana
kuhusu Yesu ili kuonyesha kwamba tunamjua Yeye na Biblia pia. Tunaweza hata
kufikiri kwamba kuongea bora kuliko wengine kunawezekana kuwa faida ili tupokee
baadhi ya tuzo kutoka kwa Mungu. Lakini, kulingana na andiko hili, maneno hayatoshi kuingia katika ufalme
wa Mungu. Wokovu si astahili yetu, lakini hii ni zawadi ya ukarimu wa Mungu.
Je,
inawezekanaje tuseme kwamba tunamjua Yesu naye aseme kwamba hatujui sisi?” Hii
ni kwa sababu katika biblia kitenzi kujua kinamaanisha uhusiano wa ndani,
uzoefu wa kina ambao ni muhimu sana katika safari yetu ya wanafunzi wa Yesu.
Ikiwa anasema kwamba hatujui sisi ni kwa sababu sisi hatumjui yeye. Katika
mwendo huu hakuna ahadi/makubaliano kuhusu pendekezo lake, hakuna utambulisho.
Hatuwezi kuwa wanafunzi wa Yeu kupitia maneno peke yake. Ushuhuda wa maisha unathamini
zaidi kuliko maneno. Tukijifikiria bora kuliko wengine haituhakikishia wokovu.
Kila kitu tunachofanya kinasababisha matokeo makubwa kwetu na katika hali iliyo
kandokando yetu. Kwa maneno mengine, kufikia mafanikio ama bahati mbaya kwa
maisha yetu kunatutegemea sisi wenyewe; huu ni uamuzi wetu. Neema ya Mungu
ituongoze ili tuweze kufanya mapenzi yake na kupata uhai.
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Serah
Nenhum comentário:
Postar um comentário