Kutafakari
kuhusu Hek 18, 6-9; Wab 11, 1-2. 8-19; Lk 12, 32-48
Liturgia
ya siku ya leo ni mwaliko wa kumwamini Mungu kwa kweli. Kwa kufanya hivyo, tuna
Ibrahimu kama mfano na mwaliko wa Yesu ili
wanafunzi wake wakeshe na kujiweka tayari kwa ujio wake. Somo la kwanza linaongea
kuhusu usiku ule maarufu ambao Waisraeli waliutazamia wokovu wa wenye haki na
uharibifu wa adui. Uhakika kuhusu uwepo na tendo la ajabu la Mungu katika
safari yao
uliwaimarisha watu kukesha na kungoja ukombozi wao kutoka utumwani Misri. Huu
ni mwaliko wa tuwe tayari kumtambua Bwana Yesu miongoni mwetu na kumkaribisha
katika nyakati zote. Kulingana na somo
la pili, katika imani sisi tu warithi wa ahadi za Mungu kwa Ibrahimu; nasi,
pamoja naye, tu wasafiri na wageni juu ya nchi. Kupitia imani tunatamani nchi
iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Ndiye Mungu mwenyewe aliyetutengenezea mji kwa sababu
hana haya ya kuitwa Mungu wetu. Pamoja na Ibrahimu na wenye haki wengine
tunaalikwa kuziamini ahadi za Mungu kwa sababu ni mwaminifu yule aliyeahidi.
Katika njili Yesu aliwaita wanafunzi wake kama kundi dogo
ambalo lilikuwa limepewa ufalme kutokana na ukarimu wa Mungu Baba. Katika
mazingira yale, watu walioacha kila kitu na kumfuata Yesu, walikuwa wachache na
hawakuwa matajiri au watu wenye uwezo. Hata hivyo, Yesu aliwaalika kuuza mali
yao na kutoa sadaka kwa ajili ya walio na mahitaji zaidi. Katika njia hii
wanaweza kujitajirisha wenyewe kwa Mungu kupitia uhuru wa moyo kama vile
mwalimu wao alivyo. Mali yao haina maana tena kwa sababu Kristo ndiye hazina
yao. Kristo mwenyewe anataka kuwatumikia kwa kushiriki nao furaha sawa anayoona
katika ushirika wake na Baba. Yeye anaweka wazi kwamba kumtumainia Mungu na
wala siyo mali, ni wajibu wa kila mfuasi wake wa kundi dogo, ambalo mwishowe
wanaunda Kanisa lake. Mwinjili
Luka alipoiandika Injili yake, Kanisa lilikuwa bado dogo, la wanyonge wasiokuwa
na uwezo na hawakujulikana.
Mwaliko
wa Yesu kwa kundi lake, lililo sisi sote, ni kufanya tofauti na tabia ya
kutafuta usalama katika mali
nyingi ama ulinzi katika wenye nguvu. “Ni hatari kwa Kanisa na viongozi wake
kutafuta umaarufu na nguvu, kama vile kuwa na
uwezo wa kisiasa na kuweka vitega uchumi. Wakati wote katika historia, ambapo
Wakristo walitegemea serikali, wanasiasa, na faida kubwa katika biashara,
Kanisa lilikuwa dhaifu na kuporomoka.” Basi, Yesu anatuangalisha tena kuhusu
hatari ya mali
na anatushauri tuwafadhili fukara. Tumepewa ufalme na Baba kwa sababu sisi tu
kweli wake, katika Yesu. Kutokana na hii zawadi ya Mungu, tunakuta hazina yetu
ya kweli na kwa hivyo ni halali kumtegemea Mungu katika mambo yote; hayo ni
matarajio yake. Wakati Mungu anakuwa hazina ya kweli katika maisha yetu, na
mioyo yetu ikamtukuza yeye, uhusiano mpya utaanza na kukua. Moyo wetu uko wapi?
Mungu alitukabidhi ufalme wake nasi tunaalikwa kujikabidhi mikononi mwake. Huu
ni ukabidhi wa makubaliano. Hii ni hali inayotupasa kuwa na imani, yaani, ile
imani ya Ibrahimu na wenye haki wengine wa Biblia.
kulingana
na uzoefu wa Ibrahimu, haitoshi kuamini; ni lazima kutii, kumwachia Mungu na
kuruhusu kuongozwa naye hadi palipompendeza. Kuhusu uzoefu huu wa Ibrahimu,
waraka wa Waebrania unatuletea ushuhuda mzuri sana ,
yaani, “Kwa njia ya imani Ibrahimu alitii alipoitwa ahamie nchi ambayo angepewa
kuwa mali
yake. Alihama bila kujua anakokwenda” (Waebrania 11:8). Kumwachia
Mungu ni kuwa na imani ya Ibrahimu. Ni imani ya kumwacha Mungu aitwe Mungu aliye Baba na Mtoaji. “Matatizo yote
yapaswa kufikiriwa na kusomeka kwa maelewano na ubaba wake” (Mt. Yohane
Calabria). Haya ni matarajio ya Yesu kwa maisha ya sisi sote tulio wanafunzi
wake wapya na warithi wa utume wake. Yeye anakuja daima kukutana nasi na
kutarajia kukaribishwa vizuri kupitia uaminifu na utayari wetu. Kama anavyoona
furaha kwa kushiriki nasi ufalme wa Baba yake vile vile ataona furaha kubwa
zaidi atakapokutana na wale ambao watakuwa tayari kwa ujio wake. Tukumbuke
kwamba “furaha ya Bwana ni nguvu yetu.”
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Serah
Nenhum comentário:
Postar um comentário