Tafakari kutoka Nm 11, 25-29; Yak 5, 1-6; Mk 9, 38-43. 45. 47-48
Mungu
habagui mtu yeyote kwa sababu anapenda na katika upendo hakuna ubaguzi. Katika
andiko la kwanza la tafakari yetu, Yeye anatarajia kwamba watu wake wote wawe
manabii, kwa kulikisikia Neno lake na kuongea kwa jina lake. Zawadi za Roho
wake hutusukuma kutenda mema kwa kila mtu, kwa kuthibitisha kuwa upendo wake
hauna mipaka. Hakuna mtu anayepaswa kutumia zawadi alizopokea kwa ajili yake mwenyewe
ama kufikiria kuwa yeye ndiye aliye na upendeleo wa Mungu. Mbele yake hakuna
mtu aliye na hadhi zaidi ya wengine.
Katika
andiko la pili, Mtakatifu Yakobo anakosoa vikali wale wanaotajirika kwa njia ya
udhalimu, kuwanyima wafanyikazi mishahara yao. Waathiriwa wa hali hii
hawasahauliwi na Mungu ambaye analaani aina zote za ukosefu wa haki na usawa
kati ya watu. Ukosoaji huu unatumika pia kwa wale wote wanaotegemea zaidi vitu
walivyo navyo kuliko Mungu. Mtu anapokufa hawezi kuchukua chochote naye. Kwa
hivyo, tabia ya kujilimbikiza ni upumbavu.
Katika
injili wanafunzi wanamzuia mtu kutoa pepo kwa jina la Yesu kwa sababu hakuwa wa
kikundi teule cha wale Tenashara. Mwanamume, ambaye alimkomboa mwingine kutoka
kwa uovu na kumtoa maisha mapya, amezuiliwa na wafuasi wa Yesu. Hao waliweka
taasisi hiyo kwanza kuliko binadamu, wazo lao kuliko mtu aliye na shida:
wagonjwa wanaweza kusubiri, furaha inaweza kusubiri. Tunaona kwamba bado
wanakosa utambuzi, uwazi na kufungwa.
Yesu anapinga wazo hili kwa kusema kwamba mtu
yeyote ambaye husaidia ulimwengu kujikomboa na kufanikiwa ni wetu. Mtu yeyote
anayepanda upendo ni wetu, na hivyo ni wa Kristo. Tufikirie ni wangapi
wanafuata Injili halisi, bila hata kujua, kwa sababu wanafuata upendo. Mtu
anaweza kuwa wa Kristo bila kuwa mwana wa kundi la Tenashara. Mtu anaweza kuwa
wanaume na wanawake wa Kristo, bila kuwa wanaume na wanawake wa kanisa, kwa
sababu ufalme wa Mungu ni mkubwa kuliko kanisa, hailingani na kikundi chochote.
Kisha tujifunze kufurahia na kushukuru kwa mema yaliyofanywa na yeyote.
Wakati
tunapobaki kutafiti ni nani aliye wetu au la, tunakosa nafasi ya kusaidiwa kutenda
mema kwa ufanisi. Tufikirie juu ya yale mema tunashindwa kutenda kwa sababu ya
ugumu wetu wa kutenda pamoja na wengine. Tujiulize ikiwa tunataka kukuza ufalme
wa Mungu au sisi wenyewe? Kashfa kubwa ni kuwa kikwazo kwa wale wanaotaka
kumwamini Yesu. Kufungwa kwa wale walio tofauti nasi ni kizuizi kinachotuzuia
kuzaa matunda. Kwa upande mwingine, Yesu ndiye mtu asiye na vizuizi, bila
mipaka, ambaye mpango wake ni mmoja tu: ninyi nyote ni ndugu na dada. Alitaka
kujenga udugu wa ulimwengu wote, akiwafanya watu wote wawe watu mmoja, yaani Watu
wa Mungu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário