Hek 2:12.17; Yak 3: 16-4:3; Mk 9,30-37
Katika ulimwengu wa
sasa ambao mbio wa kuchukua nafasi za kwanza, utafutaji wa vyeo na upendeleo,
na mwelekeo wa kutaka kuchukua faida juu ya wengine zinaongezeka kila wakati,
Neno la Mungu linatukumbusha kwamba ni muhimu kutenda kwa busara na kutafuta
maadili ya kweli; hii ni njia ya kipekee ya kupata furaha ya kweli. Mwaliko wa
kubadili mawazo na tabia zetu ili tuweze kumfuata Yesu ni wazi kabisa.
Andiko la kitabu
cha Hekima ya Sulemani linaongea kuhusu ushuhuda muhimu wa mtu mwenye haki na
upinzani wa wale ambao hawaukubali ushuhuda wake na kumtendea vibaya, hata kwa kupanga
kifo chake. Hali hii inatokea kwa sababu ya uaminifu yake kwa Mungu. Mambo yote
ambayo washtaki wanasema dhidi ya mwenye haki yanakuwa uthibitisho wa
utambulisho wa mtu huyo aliye mwana wa Mungu naye Mungu mwenyewe atamtegemeza
na kumtetea dhidi ya adui zake. Huu ndio mfano wa Kristo ambaye aliteseka sana
kwa sababu ya uaminifu wake kwa mpango wa Mungu na kwa kujisalimisha kwake aliupata
wokovu hata kwa wale waliomkandamiza.
Andiko la pili
linasema kuwa hekima ambayo inasababisha kujua kamili inatoka kwa juu kwa
sababu ni Mungu mwenyewe chanzo cha hekima ya kweli. Mtu anayeongozwa na hekima
hii anaweza kuchagua vizuri na kuwa chombo cha amani, cha umoja na cha ushirika
katika jumuiya, tena anaweza kuwa tayari kusikiliza maneno ya wengine na
kutenda mema kwa ajili yao.
Injili ni
mwendelezo wa tangazo la Petro kuhusu utambulisho wa Yesu na mwaliko wa Yesu
mwenyewe ili wafuasi wake wamfuate katika kujisalimisha kwake ili wapate uzima.
Yesu alitambua kwamba walihitaji kujua maana kamili ya utambulisho wake kama
Masihi na kuyafahamu vizuri mapendekezo yake. Kwa hivyo alitumia nafasi maalum katika
mahali pa faragha ili kuwafundisha. Kwa nini hakutaka watu wafahamu alipo
pamoja na wanafunzi wake? Kwa sababu wazo wa Masihi ambao watu walikuwa nao ulikuwa
mbali sana na utambulisho wake na kwa hivyo lilikuwa hatari kwa malezi ya
wanafunzi wa Yesu.
Basi, bila
kusukumwa na uwepo wa watu, Yesu alijiona mwenye heri kabisa ili kuwaongelea wanafunzi
wake kwa uwazi kuhusu mateso, kifo na ufufuko wake, lakini walionekana mbali
sana na mwalimu. Hawakuelewa tena kwa sababu walishughulika kwa mawazo na nia
tofauti. Kwao ilikuwa muhimu kujadiliana juu ya msimamo na upendeleo kuliko
kuandamana na mwalimu wao kwenye kujisalimisha. Hivyo tunaona kwamba hata
wanafunzi waliingia nyumbani pamoja na Yesu, inaonekana wanaendelea nje. Kwa hivyo
Yesu anawaita kwako kama ilivyotokea mara ya kwanza, yaani anawalika ili waweze
kuishi kwa ushirika nawe na hisia yake na mawazo yake na kupata kufahamu maana
ya kujitolea kwake hadi upeo.
Kwa uvumilivu na
kwa kutumia mtoto kama mfano, yeye aliwasaidia kufahamu ufunuo wake na masharti
ya kumfuata. Yule anayeamua kumfuata Yesu anapaswa kuongoza maisha yake
kulingana na njia tofauti na mawazo wa dunia. Ikiwa katika nafasi iliyopita
Yesu aliwaomba kuyatoa maisha ili kuyaokoa, hapo aliwaomba kuwa wa mwisho na
mtumishi ili kuwa wa kwanza.
Yesu
anadhihirisha utambulisho wake kama Mwana wa Adamu (mtu). Katika Agano la Kale
tunakuta maneno haya katika vitabu vya nabii Danieli na Ezekieli. Kulingana na
Danieli maneno haya yaongea kuhusu hali ya utukufu wa yule ambaye atakuja siku
ya mwisho (Dan 7:13). Kulingana na toleo la Ezekieli maneno Mwana wa Mtu
yanatumiwa na Mungu kwa uhusiano na nabii wake na kuonyesha hali ya udhaifu na
kifu cha binadamu (Ezk 2:1, 3:1.25, 17:2). Basi, hii ni maana iliyotumiwa na
Yesu ili kuongea kuhusu utambulisho wake kwa uhusiano na hali ya binadamu na
fumbo la mateso, kifo na ufufuko wake ambalo lilisababisha ubinadamu mpya. Hivyo,
tunafahamu maana ya ufundishaji wa uvumilivu wa Yesu ili kuwasaidia wanafunzi wake walio na
ujinga na udhaifu wa akili.
Watoto wadogo
wana nafasi maalum moyoni mwa Yesu. Alisema kwamba Ufalme ni wao naye mtu anayetaka
kuingia katika Ufalme huu anapaswa kuwa kama watoto. Mfano wa watoto wadogo ni
maalum kwetu kwa sababu hao wanatusaidia kutafuta muhimu zaidi ya maisha, yaani
ukweli, unyenyekevu wa moyo, kuamini, n.k. Kama vile wanafunzi wa kwanza sisi
pia tuko na ugumu wa kufahamu mambo yote kumhusu Yesu na mapendekezo yake,
lakini tukimruhusu, yeye anaweza kufungua akili zetu na kubadilisha moyo wetu ulingane
na matarajio yake. Siku ya leo yeye anatualika kwa uhusiano wa kibinafsi naye.
Kupitia uhusiano huu peke yake tunaweza kuingiza utambulisho wake na kufahamu
maana ya ushiriki wetu katika kazi yake ya ukombozi. Mfano wa watoto wadogo
utusaidie kufahamu nia ya Yesu kuhusu maisha yetu na kukubali mapendekezo yake kwa
kutumia nguvu zetu kwa ajili yake “mpaka kifo, mpaka uzima”.
Nenhum comentário:
Postar um comentário