kutafakari juu ya Mt 21,1-11; Is 50,4-7; Waf 2,6-11; Mc 14,1-15,47
Tunaingia katika wiki muhimu sana kwa Jumuiya
za Kikristo. Hii ni wiki inayojumuisha matukio makuu ya imani yetu, ikieleza
kwa ishara nyingi na kwa kina vipindi vya mwisho vya maisha ya Yesu ya kibinadamu
hapa duniani na kutualika kwa kimya na kutafakari. Hii ni pia nafasi ya kufanya
upya ahadi yetu kama wafuasi wa Yesu na kujiruhusu kuimarishwa na mfano wake wa
uaminifu na uamuzi.
Tunaalikwa kumfuata Yesu anayeingia kama mshindi
katika Yerusalemu ili kukamilisha kazi yake ya upendo. Kweli, hakuja juu ya
farasi kwa kiburi na kwa jeshi yenye nguvu kama walivyofanya majenerali wakiingia
mijini, lakini amepanda punda, na kuja kwa wema na rehema kama imetokea wakati
wa maisha yake yote. Yesu anajua sana nini itatokea nawe, hata hivyo hakukata
tamaa. Kinyume, anaonyesha uhuru wa Mwana mpendwa aliyetumwa kuwaokoa wanadamu.
Pamoja na kukumbuka kuingia kwake katika “Mji wa amani”, tunakumbuka pia mateso
na kifo chake katika mji huu ulio na mazoea ya kutenda kwa ukatili dhidi ya
wajumbe wa Mungu. Hivyo, kifo chake sio hatima, bali ndicho matokeo ya kazi ya kinabii
aliyeishi kwa uaminifu hadi upeo.
Kama tunavyojua, nabii Isaya anatoa nyimbo nne
ili kuongea juu ya utambulisho na kazi ya Watu wa Mungu, wanaoitwa pia
“Mtumishi wa Mungu.” Nyimbo hizi ziliandikwa wakati wa utumwa wa Babeli nasi
tunaweza kuzipata katika sehemu ya pili ya Kitabu cha Isaya. Andiko tunalotumia
hapo unafahamika kama ‘wimbo wa tatu’ na kulingana na wimbo huu, mtumishi
anaishi wito wake kama zawadi inayotoka kwa Mungu kwa ajili ya kutoa maisha
mapya kwa ndugu zake. Kwa sababu ya uaminifu wake, aliaibishwa, alikataliwa na kuteseka
sana, lakini hakukata tamaa kwa sababu aliona ukaribu na utunzaji wa Mungu
kuyahusu maisha yake.
Kulingana na Jumuiya za Kikristu Mtumishi huyo
ni mfano wa Yesu. Mtakatifu Paulo asema kwamba kwa ajili ya kujiambulisha
mwenyewe na hali ya binadamu, Yesu Kristo alijinyenyekeza, akaaibishwa, akateseka
na kuuawa maana ya uaminifu wake kwa Mungu. Amini yake ya mwana katika Mungu ndiyo
maana ya uaminifu wake. Kwa njia ya kujifanya upole aliupata utukufu. Njia ya
unyenyekevu, ya ishara ndogo na ya kuchagua kinachoonekana bila maana kwa jamii
ndizo tabia za wale wanaoendelea kazi yake.
Kulingana na masimulizi ya Marko, Yesu anafikiria
kuwa kukamatwa kwake, mateso yake na kifo chake kitakuwa kashfa kwa wanafunzi
wake, maana bado walikuwa na mawazo ya Masihi mwenye nguvu na umaarufu. Hata
hivyo, aliendelea akisema kuhusu ufufuko wake na baadaye mkutano nao kwenye mahali
ambapo yote yalianza, yaani kutoka Galilaya. Kwa Yesu hakuna maonyesho ya
upendo kubwa kuliko kutoa maisha yake kwa ajili ya marafiki zake, hata wakati
wao wametoroka (isipokuwa wanawake na mwanafunzi mpendwa, kulingana na injili
ya Yohane).
Katika kilio chake, yaani “Mungu wangu, Mungu
wangu, kwa nini umeniacha?”, yeye alionyesha uchungu aliohisi kweli kama
mwanadamu, yaani, uchungu wa kuachwa, uchungu wa vitendo viovu, uchungu wa
dhambi za binadamu, n.k. Ghafla, wakati yote yalionekana yamefanyika bila mafanikio,
tuko na tangazo kubwa la imani kutoka kwa watu wasiotarajiwa, yaani yule akida
pamoja na walioandamana naye: “Kweli mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
Yesu aliachwa na marafiki zake, lakini yeye
hakuwako peke yake msalabani wala wakati wa kazi yake. Maneno yake mwenyewe yanashuhudia
kuhusu hayo, yaani “Yule aliyenituma yuko pamoja nami, hakuniacha peke yangu,
kwa maana mimi nafanya yanayompenda yeye (Yoh 8.29).” Hivyo “kilio” ambacho
Mathayo anaweka mdomoni mwa Yesu kinapaswa kufahamika kwa uhusiano na
kujisalimisha kwake mikononi mwa Baba, kulingana na toleo la Luka, iliyo tabia
yake daima, yaani “Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu (Lk 23,46).”
Vinginevyo, tungekuwa kukana sio tu ushirika wake na Baba bali pia uaminifu wa
Baba huyo.
Fumbo la mateso na kifo cha Yesu halionyeshi
uchungu kama jambo la kwanza kwa kutafakari bali upendo wake mkubwa hadi upeo.
Kifo hakikuwa kulazimishwa kwa Yesu, bali jambo ambalo yeye alikubali kwa hiari.
Yesu alijua kwamba alikuwa akifanya jambo sahihi na hivyo mateso yake ni mwanzo
wa ushindi wake juu ya mauti na ya dhambi, akifufua matumaini yote ya maskini
na ya wanadamu wote.
Mateso ya Mwana wa Mungu yanatualika kutafakari
kuhusu hali ngumu ya mateso ya binadamu. Kama Mungu alijibu kwa ufufuko mbele
ya kifo cha Mwanawe, tunaweza kuhitimisha kwamba Mungu hataki mateso na uchungu
wa watu. Yeye hawaachi wale wanaoteseka wala hanyamazi mbele ya mateso yao.
Kristo alichukua kwa nafsi yake uchungu wa watu wote wa nyakati zote. Yeye
anaendelea kuteseka wakati sisi tunahisi maumivu na majaribio katika safari
yetu. Mfano wake unatuimarisha tuwe na kuwepo ufanisi maishani mwa watu wanaoteseka
zaidi kuliko sisi. Misalaba ya mshikamano na huruma tunayoitwa kuchukua kila
siku kama yeye alivyo inafanya kwamba kujitolea kwetu kuwe ishara ya upendo pia
kama ushiriki katika mateso yake kwa ajili ya wokovu wa watu wote.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário