Kutafakari kuhusu Kut 20: 1-17; 1Wak 1, 22-25; Yoh 2,
13-25
Maandiko Matakatifu yaongea kuhusu
uhusiano maalum kati ya Mungu na watu wa Israeli. Yeye alianzisha agano na watu
hawa akiwapa miongozo ili watembee salama na kufanya mapenzi ya Mungu. Katika
hali halisi hii, amri kumi zilizaliwa. Kuishi Amri ilikuwa jambo muhimu katika
safari ya Watu wa Israeli ambao wanafikiria Sheria kama Neno la Mungu na Neno
la Mungu kama Sheria.
Basi kuna uhusiano wa ndani kati ya Sheria na Neno la Mungu. Kupitia Sheria au
Amri, Mungu anaonyesha utunzaji kwa watu wake na kuonyesha njia ya ukombozi.
Wakati watu wanafuata miongozo hii wanaweza kuona Baraka za
Mungu, lakini wakati wanachagua ukosefu wa uaminifu matokeo ni kifo. Kidogo
kidogo muhimu ya Sheria ilikuwa ikisahauliwa na kubadilishwa kuwa ni mawazo ya
kibinadamu. Hali hii ilizaa aina ya dini ambayo haikuzaa matunda tena. Ilipaswa kuchukua tena maana ya kweli ya
Sheria kwa ajili ya kuanzisha tena uhusiano mpya na Mungu kupitia Agano mpya na
milele. Iliwezekana kupitia Kristo, aliyejulishwa na Mtakatifu Paulo kama nguvu
na hekima ya Mungu.
Katika injili tuko na tukio la kutakasa
kwa hekalu. Katika wainjilisti wengine tukio hili lilijulishwa katika sehemu ya
mwisho ya injili yao wakati alipoingia Yerusalemu ili kuteseka mateso yake. Kwa
upande wa mwinjilisti Yohana ni tofauti, yaani anaweka tukio hili mwanzoni mwa
injili yake. Kisha, Yesu alienda mpaka Yerusalemu na kuona huko hekaluni watu
wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. Alihisi
hasira fulani kwa sababu ya hali ile na mara akatengeneza mjeledi wa kamba na
kuwafukuza wote nje ya hekalu. Katika mwanzo wa tukio hili hakuna mtu ambaye
aliweza kufahamu tabia hii ya Bwana Yesu. Mara nyingi walikuwa na mazoea ya
kumwona Yesu akitenda kwa huruma na upendo na unyenyekevu. Hawakutarajia kwamba
aweze kutenda hivyo. Basi, tujaribu kufahamu maana ya tabia ya Yesu.
Watu walikuwa wamebadilisha
mahali pa sala kuwa hali ya biashara. Alipowatoa
wote hekaluni, Yesu alionyesha
hamu yake kwa nyumba ya Mungu na hasira fulani kuhusu tabia ya kutoheshimu kwa Hekalu. Bila shaka mambo ambayo yalitendeka hekaluni
yalitafsiri aina fulani ya dini iliyoko. Kwa
uwepo wa Yesu duniani aina hii ya dini imeisha na uhusiano wa kibiashara
na Mungu imeshindwa. Uwepo wa Yesu unatangaza wakati mpya. Katika nafsi yake
tunakuta Hekalu mpya, yaani mahali pazuri mno pa mkutano na Mungu. Katika Yesu mtu
anaweza kukutana na Mungu kwa kweli.
Mafundisho yake yaliwasaidia watu watafakari
vizuri kuhusu lengo la Hekalu na tabia kamili
kuhusu mahali huko. Msingi wa mafundisho yake ni kumwabudu
Baba kwa Roho
na ukweli. Hiyo ndiyo maana ya kuwa
mwanafunzi wa Kristo, yaani kuwa hekalu pamoja naye.
Wale wanaokuwa wanafunzi wa
Kristo wanaalikwa kuwa naye Hekalu jipya ambapo Mungu
anaishi. Kwa njia ya ubatizo tumezaliwa upya kwa njia ya
kiroho. Kwa njia hii tunabadilishwa kuwa mahekalu
hai, yaani na makao yake Mungu. Kila
mmoja wetu ndiye jiwe la ujenzi mkubwa unaoitwa Kanisa ambalo
ni mwili wa Kristo na jumuiya ya imani
na upendo. Kama mawe hai tunaalikwa
kutenda pamoja kupitia ushuhuda wa maisha ili ujenzi huu kutimiza lengo lake. Utunzaji kwa urembo wa nje
wa kimwili ni mzuri,
lakini hauwezi kutuzuia ya kujali hekalu
hai la Mungu ndipo ndani yetu.
Hiyo ni kauli ya
Mtakatifu Paulo katika waraka wake kwa Wakorintho: “Ninyi ni hekalu la Mungu na Roho
wake anakaa ndani yenu”. Kweli
kama jumuiya ya Kikristu tunaimarishwa na Roho wa Mungu ili
tuweze kuzaa matunda mazuri,
kwa kuwa vyombo vya wokovu wake. Imani tunayoishi katika jumuiya inatufanya mashahidi
wa kweli. Ushuhuda wetu unatangaza ukaribu wa Mungu na hali
mpya ambayo Yesu alileta katika nafsi yake mwenyewe.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário