Kutafakari kutoka
Yeremia 31:31-34; Waebrania 5:7-9; Yoh 12:20-33
Kutoka maandiko haya tunaanza
kutafakari kuhusu fumbo la “Saa” ya Yesu, ambayo inajumuisha mateso, kifo na
ufufuko wake. Kwa kupitia Saa hii yeye atamtukuza Baba na atamaliza kazi yake.
Kazi ya Mwana Yesu ndio wokovu wa ulimwengu ambao ingawa ulikwisha tendeka kwa
wote lakini kila wakati unaomba kukubali kwa hiari kutoka kila mtu. Upendo wa
Mungu uliofunuliwa na Yesu ndilo Agano Jipya ambalo liliandikwa moyoni mwetu na
kutupa utambulisho wa Watu wa Mungu. Tunataka kumuona Yesu kwa njia yake ya
kujifunua mwenyewe na kujifunza kutoka kwake kuishi kama chembe ya ngano ambayo
inakufa ili kutoa mazao mengi.
Somo la kwanza linaongea kuhusu Agano
jipya ambalo Mungu ataanzisha na Watu wake. Litakuwa tofauti sana na Agano la
kwanza lililoandikwa katika mawe nao watu walikosa kwa uaminifu. Tabia kamili
kwa agano hili jipya ni uhusiano wa ndani kati ya Mungu na watu wanaoalikwa kuishi
kulingana na Neno lililoandikwa na Mungu moyoni mwao. Basi, Mungu anaongea na
watu wake kutoka moyo kwa moyo ili wajione kutibiwa kwa upendo na huruma. Bila
msamaha hakuna maridhiano, tena hakuna furaha. Uaminifu na hisia ya kuwa watu
wa Mungu itakuwa utambulisho mpya wa watu hawa: “Nitakuwa Mungu wao nao
watakuwa watu wangu”.
Kulingana na mwandishi wa Waraka wa
Waebrania, kupitia utii kwa mapenzi ya Mungu, Yesu alianzisha Agano Jipya na kukubali
kuteseka ili kutoa maana mpya kwa mateso ya binadamu. Uzoefu huu ulikuwa nafasi
ya kujifunza zaidi maana ya utambulisho wake wa kibinadamu. Mfano wake wa kujisalimisha
kwa upendo ni njia kuishi kama pendekezo kwa wote.
Injili inaongea kuhusu mkutano muhimu
ambao ulianza kwa ombi: “tunataka kumwona Yesu”. mazingira ya tukio hili yalikuwa
sherehe ya Pasaka ambayo Wagiriki na watu wengine walikuja Yerusalemu ili kushiriki
pamoja na Wayahudi. Wagiriki walimkaribia Yesu kupitia Andrea na Filipi walio wanafunzi
wake. Tamani ya Wagiriki ya kumwona Yesu ilikuwa zaidi ya udadisi wa kumwona mtu
maarufu. Kitenzi “kuona” hapa kunamaanisha kujua kwa njia ya ndani kuhusu
utambulisho wa Yesu. Basi, yeye alichukua nafasi ya kuwafundisha wanafunzi wake
tena jinsi anavyotaka kutangazwa, yaani kama Masihi mtumishi ambaye
alijisalimisha kwa upendo.
Tukio hili inatukumbusha ile la mwanzo
wa injili ambalo wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walitaka kumjua mwalimu Yesu naye
aliwaalika watembelee mazingira yake, yaani “mjoni nanyi mtaona”. Ni mwaliko wa
kufanya uzoefu. Hakuna njia nyingine ya kumjua Yesu. Msingi wa injili hii ni ‘
‘Saa’ ya Yesu. Neno hili ndilo muhimu katika injili hii ya Yohana. Tunaweza
kukuta vifungu vingi ambavyo vinaongea kuhusu jambo hili. Yesu alijaribu kuelea
akiutumia mfano wa Chembe ya ngano ambayo inakufa ili kuzaa mazao mengi. Hivyo,
muhimu ya tafakari yetu sio kifo bali maisha mengi. Saa yake Yesu inajumuisha mateso,
kifo na kufufuka. Ndio upendo ulimwimarisha Yesu kutenda hivyo. Hivyo, mkutano wa kweli na Yesu ni kushiriki katika
fumbo la kujisalimisha kwake.
Kumwona Yesu ni
hamu ya moyo wa binadamu, kwa sababu Yeye ndiye wa kipekee anayeweza kumdhihirisha
Baba. Maisha yake ya kibinadamu yalikuwa bila utukufu daima (Kenosis, neno la kigiriki), akichukua
njia ya mtumishi, kwa sababu alikuja kutumikia sio kutumikiwa. Hivyo, kila mtu
anayetaka kumfuata anapaswa kufanya vivyo hivyo. Watu ambao wanatukaribia
kumtafuta Yesu, hawataki tuongelee Yesu fulani kulingana na maneno yetu, bali Yule
aliyejisalimisha kabisa kwa ajili yetu akikubali msalaba kama ishara kubwa ya
upendo. Hivyo, hakuna njia nyingine ya kuwa wanafunzi wake wa kweli ila
tukubali kuwa wa mwisho ili kuwa wa kwanza; kuyatoa maisha ili kuyapokea
baadaye; kufa ili kuishi milele. Tunaweza kushiriki katika ushirikiano ambao
Mwana anaishi na Baba ikiwa tuko na uwezo wa kuyatoa maisha kama Yesu. Mashahidi wengi wa
historia ya Kikristo walikuwa na uhakika huu. Watu wengi wanaendelea wakifa ili
wengine wengi waweze kuishi sio kwa njia yoyote bali kwa heshima. Kwa upande wetu, hakuna njia nyingine ya kuwa waaminifu
kama wanafunzi wa Yesu ila kuyatoa maisha kama yeye alivyo. Kwa hivyo, "tunataka kumwona Yesu".
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário