sábado, 31 de março de 2018

UPENDO UNAPASWA KUWA WA KWANZA KATIKA MAMBO YOTE



Kutafakari kuhusu At 10,34a.37-43; Col 3,1-4; Yoh 20,1-9


Tufurahi sote, kwa sababu hii ni siku aliyotufanyia Mungu! Tangazo la ufufuko wa Yesu ni mwaliko wa furaha, yaani furaha ya maisha ambayo yanayashinda mauti, furaha ya upendo ambao unaushinda uchungu na kuwepo katika hali yetu ya kawaida akiyaimarisha matumaini yetu. Wanafunzi wa kwanza walipotangaza tukio hilo, walianza kutokana na maisha ya Yesu ya kibinadamu, aliyetiwa na Mungu kwa kazi ya wokovu wa binadamu. Kama alama ya wema wa Mungu, maana ya maisha ya Yesu ilikuwa kuwatendea watu mema. Matendo yake yote mengi yaliwezekana tu kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye. Kwao Wanafunzi wa kwanza uzoefu walioishi pamoja na Yesu ulikuwa umejaa maana. Kutokana na uzoefu huu waliweza kuwa mashahidi. Basi, tangazo lao halikuwa maneno peke yake bali uzoefu wa maisha pia, yaani maisha yao yalibadilika.
Ikiwa Kristo hakuwa amefufuka, je, mahubiri ya wanafunzi wake yangekuwa na maana gani? Hakika yangekuwa tupu, yaani, pasipo maana. Mbele ya kifo kisicho na haki cha mwalimu wao walikufa moyo sana, lakini ushindi wa uhai unawapa maana mpya ya kuishi. Basi, ujumbe wa wanafunzi unatafsiri pia ushindi dhidi ya hali ya hofu ambayo waliishi baada ya kifo cha Mwalimu, yaani kikundi chao kilivunjika. Kwa wanafunzi ilikuwa vigumu sana kuendelea kwa safari baada ya kukatishwa tamaa kwao kuhusu mwalimu Yesu ambaye walitarajia mengi, hasa awe mfalme mwenye nguvu. Lakini maisha yao yalibadilishwa kabisa baada ya kuona ushahidi wazi wa ufufuko wa Mwalimu, yaani kaburi tupu, vitambaa alivyolalia, na baadaye Yeye mwenyewe akajionyesha kwao; kisha waliacha hofu, wakiitoa nafasi kwa imani na kuchukua maisha ya mashahidi.     
Lakini tunapaswa kutambua kwamba safari hii ya imani ya wanaume iliimarishwa na ushuhuda wa mwanamke mmoja anayeitwa Maria Magdalena ambaye alikuwa wa kwanza kuenda kaburini akutane na Yesu na kupokea habari kwa ajili ya Mitume. Walialikwa kukaribisha njia mpya ya Yesu ya kuishi kati yao na kuyaamini Maandiko yasemayo kwamba alipaswa kufufuka kutoka wafu. “Magdalena ni yule ambaye Yesu aliponya kwa kufukuza mashetani saba ndani yake. Katika Biblia namba saba inamaanisha ukamilifu. Basi, Maria Magdalena alikuwa ameponywa na Yesu kikamilifu.” Katika uhusiano na Kristo Maria alikuta upendo wa kweli ambao alikuwa ameutafuta sana kwa muda mrefu. Mwanamke huyo alijifunza jinsi ya kuwa mwanafunzi wa kweli, akimfuata Yesu wakati wa mahubiri, tangu Galilaya hadi msalabani. Kwa hivyo anastahili cheo cha “Mtume wa Mitume wa Yesu.” 
Baada ya kupokea habari kuhusu udidimizi wa mwili wa Kristo, wanafunzi wawili wakaenda mbio kuelekea kwenye kaburi, yaani Petro na mwanafunzi aliyependwa na Yesu (Yohane). Walikimbia pamoja, lakini huyo mwanafunzi alifika kwanza. Hivi, ndio upendo ambao unapaswa kufika kwanza katika mambo yote. Yule anayependa anapata kuwa wa kwanza katika maonyesho ya upendo na imani. Anaweza kutambua mabadiliko kandokando yake, kwa sababu yeye mwenyewe ana moyo ambao umebadilishwa na uzoefu wa kujiona kupendwa. Anaweza kushuhudia kuwa bila uzoefu wa upendo wa kweli imani yetu ni haba na bila maana.
Uzoefu wa ufufuko ni uzoefu wa upendo wa hiari na mwaminifu wa Mungu ambaye anaendelea kufanya upya mambo yote na kutuchagua ili tuwe mashahidi wa hali hii mpya. Tena ni uzoefu wa imani ambayo inakuta msingi wake katika Maandiko Matakatifu yanayoshuhudia kwa Yesu Mfufuka. Huu ni pia uzoefu wa ahadi ambao unatuimarisha kama wafuasi sio wa Mungu aliye mfu bali Mungu aliye mzima.  Upendo wake unazaa uzima katika sisi pia na kutufanya tuushinde vikwazo, hofu na mashaka yote. Kama ilivyotokea kwa wafuasi wa kwanza, sisi pia tunajaribiwa kufa moyo katika safari yetu, lakini Mungu anatutumia daima yeyote ambaye kama Maria Magdalena anatuletea habari inayofanya tofauti katika maisha yetu na kuonyesha njia tofauti ya kufikiri na kuishi imani mahusiano yetu. Ushuhuda wetu kama mashahidi wa Bwana Mfufuka uwe kama ilivyotokea na wanafunzi wa kwanza, yaani umejaa furaha na shauku.

Fr Ndega

L’AMORE ARRIVA PRIMA IN TUTTO



Riflessione su At 10,34a.37-43; Col 3,1-4; Gv 20,1-9


         Rallegriamoci, perché questo è il giorno che Dio ha fatto per noi! L’annuncio della risurrezione di Gesù è un invito alla gioia, alla gioia della vita che vince la morte, alla gioia dell’amore che vince il dolore e si fa presente nel nostro quotidiano, ravvivando le nostre speranze. I primi discepoli hanno annunciato l’evento della risurrezione, iniziando dalla vita storica di Gesù di Nàzaret, che è stato consacrato da Dio e mandato per salvarci dal peccato e dalla potenza del male. Come espressione della bontà di Dio, il significato della vita di Gesù è stato quello di fare del bene alle persone. Tutte le sue azioni sono state possibili perché Dio era con lui. L’esperienza dei discepoli con Gesù è stata piena di significato e da questa esperienza essi sono diventati testimoni. Nel loro annuncio non ci sono solo parole, ma anche esperienza di vita, di vite che si sono cambiate.
       Se Cristo non fosse risorto, che significato avrebbe il messaggio degli apostoli? Certamente nessuno. Davanti alla morte senza colpa del loro maestro si sono scoraggiati, ma la vittoria della vita ha dato un nuovo significato alle loro vite; vittoria contro lo stato di paura in cui vivevano dopo la morte del Maestro, perché ormai il loro gruppo si era sfaldato. Per i discepoli è stato molto difficile continuare il cammino dopo la loro delusione per il maestro Gesù, verso il quale aspettavano molto, soprattutto che fosse un potente re. Ma le loro vite sono state cambiate per sempre dopo aver visto i segni evidenti della sua resurrezione, vale a dire, la tomba vuota, i tessuti piegati, e poi lui stesso che appare loro. Hanno vinto la paura, le incertezze e hanno dato una nuova opportunità alla vita di fede e di testimonianza.
        Ma dobbiamo renderci conto che questo cammino di fede degli uomini fu motivato anche dalla testimonianza di una donna di nome Maria Maddalena che è stata la prima ad andare alla tomba, ad incontrare Gesù e ricevere informazioni per gli apostoli (Gv 20,16). Saranno invitati ad accogliere il nuovo modo di Gesù di vivere in mezzo a loro, credendo nella Scrittura che afferma che egli doveva risorgere dai morti. “Maria Magdalena è quella che Gesù ha guarito scacciando da lei sette demoni. Nella Bibbia il numero sette significa perfezione. Quindi, vuol dire che questa è stata una perfetta e completa guarigione”. Nell’incontro con Cristo, Maria ha trovato il vero amore che aveva cercato per tanto tempo. Ha imparato come essere una vera discepola, seguendolo dall’inizio della sua attività nella Galilea fino alla croce. Così è degna del titolo di “Apostola degli Apostoli di Gesù”.
           Dopo aver ricevuto le informazioni relative alla sparizione del corpo di Gesù, due dei suoi discepoli corsero verso la tomba, vale a dire, Pietro e il discepolo che Gesù amava. Correvano insieme, ma questo discepolo è arrivato prima. Così è l’amore, che arriva prima in tutto. La persona che ama veramente si anticipa sempre nella dimostrazione di affetto e di fede. È capace di identificare senza difficoltà i cambiamenti intorno a sé, perché egli stesso ha un cuore che è stato cambiato dall’esperienza di sentirsi amato. Egli può testimoniare che senza l’esperienza di un vero amore a Gesù non è possibile avere una fede autentica in lui.
         L'esperienza della risurrezione è un’esperienza dell’amore libero e fedele di Dio, che continua a fare nuove tutte le cose rendendoci testimoni di questa novità. Questa è anche un’esperienza di fede che incontra il suo fondamento nelle Scritture che testimoniano che Gesù è Risorto. Questa è anche l’esperienza dell’impegno che ci motiva come seguaci non di un Dio morto, ma del Dio vivente, presente e attivo nella nostra storia. Il suo amore produce vita anche in noi per farci superare ogni ostacolo, ogni paura e ogni dubbio nel nostro cammino. Come è successo ai primi discepoli, anche noi siamo tentati dalla disperazione, ma Dio si serve sempre di persone come Maria Maddalena chi ci porta la notizia che fa la differenza nella nostra vita, mostrando un modo diverso di pensare e di vivere la fede e i nostri rapporti. La nostra esperienza di preghiera insieme rafforzi in noi la certezza della presenza del Gesù vivente in mezzo a noi e come i primi discepoli, possiamo anche noi essere testimoni gioiosi di questo grande avvenimento che ha cambiato tutta la nostra esistenza.

Fr Ndega

sábado, 24 de março de 2018

“YULE ALIYENITUMA YUKO PAMOJA NAMI, HAKUNIACHA PEKE YANGU”



kutafakari juu ya Mt 21,1-11; Is 50,4-7; Waf 2,6-11; Mc 14,1-15,47


         Tunaingia katika wiki muhimu sana kwa Jumuiya za Kikristo. Hii ni wiki inayojumuisha matukio makuu ya imani yetu, ikieleza kwa ishara nyingi na kwa kina vipindi vya mwisho vya maisha ya Yesu kama binadamu hapa duniani na kutualika kwa shukrani na kutafakari. Hii ni pia nafasi ya kufanya upya ahadi yetu kama wafuasi wa Yesu na kujiruhusu kuimarisha kwa mifano yake ya uaminifu na uamuzi.

         Tunaalikwa kumfuata Yesu anayeingia kama mshindi katika Yerusalemu ili kukamilisha kazi yake ya upendo. Kwa kweli, hakuja juu ya farasi kwa kiburi na kwa jeshi yenye nguvu kama walivyofanya majenerali wakiingia mijini, lakini amepanda punda, na kuja kwa wema na rehema kama imetokea wakati wa maisha yake yote. Yesu anajua sana nini itatokea nawe, hata hivyo hakukata tamaa. Kinyume, anaonyesha uhuru wa Mwana mpendwa aliyepelekwa kuwaokoa wanadamu. Pamoja na kukumbuka kuingia kwake katika “Mji wa amani”, tunakumbuka pia mateso na kifo chake katika mji huu ulio na mazoea ya kutenda kwa ukatili dhidi ya wajumbe wa Mungu. Hivyo, kifo chake sio hatima, bali matokeo ya kazi ya kinabii aliyeishi kwa uaminifu hadi upeo.

            Kama tunavyojua, nabii Isaya anatoa nyimbo nne ili kuongea juu ya utambulisho na kazi ya Watu wa Mungu, wanaoitwa pia “Mtumishi wa Mungu.” Nyimbo hizi ziliandikwa wakati wa utumwa wa Babeli nasi tunaweza kuzipata katika sehemu ya pili ya Kitabu cha Isaya. Andiko tunalotumia hapo unafahamika kama ‘wimbo wa tatu’ na kulingana na wimbo huu, mtumishi anaishi wito wake kama zawadi inayotoka kwa Mungu kwa ajili ya kutoa maisha mapya kwa ndugu zake. Kwa sababu ya uaminifu wake, aliaibishwa, alikataliwa na kuteseka sana, lakini hakukata tamaa kwa sababu aliona ukaribu na utunzaji wa Mungu. Mtumishi huyo ni mfano wa Yesu ambaye kwa utambulisho wake na hali ya binadamu, alijinyenyekeza, akaaibishwa, akateseka na kuuawa maana ya uaminifu wake kwa Mungu. Amini yake ya mwana katika Mungu ndiyo maana ya uaminifu wake. Kwa njia ya kujifanya upole aliupata utukufu. Njia ya unyenyekevu, ya ishara ndogo na ya kuchagua kinachoonekana bila maana kwa jamii ndizo tabia za wale wanaoendelea kazi yake.

        Kulingana na masimulizi haya ya Marko, Yesu anafikiria kuwa kukamatwa kwake, mateso na kifo chake kitakuwa kashfa kwa wanafunzi wake, maana bado walikuwa na mawazo ya Masihi mwenye nguvu na umaarufu. Hata hivyo, aliendelea akisema kuhusu ufufuko wake na baadaye atafanya upya ahadi nao kutoka mahali ambapo yote yalianza, yaani kutoka Galilaya. Kwa Yesu hakuna maonyesho ya upendo kubwa kuliko kutoa maisha yake kwa ajili ya marafiki zake, hata wakati wao wametoroka (isipokuwa wanawake na mwanafunzi mpendwa, kulingana na injili ya Yohane). Katika kilio chake, yaani “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?”, yeye alionyesha uchungu aliohisi kweli kama mwanadamu, yaani, uchungu wa kuachwa, uchungu wa vitendo viovu, uchungu wa dhambi za binadamu, n.k. Ghafla, wakati yote yalionekana yamefanyika bila mafanikio, tuko na tangazo kubwa la imani: “Kweli mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”

       Yesu aliachwa na marafiki zake, lakini yeye hakuwako peke yake msalabani wala wakati wa kazi yake. Maneno yake mwenyewe yanashuhudia kuhusu hayo, yaani “Yule aliyenituma yuko pamoja nami, hakuniacha peke yangu, kwa maana mimi nafanya yanayompenda yeye (Yoh 8.29).” Hivyo “kilio” ambacho Mathayo anaweka mdomoni mwa Yesu kinapaswa kufahamika kwa uhusiano na kujisalimisha kwake mikononi mwa Baba, kulingana na toleo la Luka, iliyo tabia yake daima, yaani “Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu (Lk 23,46).” Vinginevyo, tungekuwa kukana sio tu kazi yake kwa ushirika na Baba bali pia uaminifu wa Baba huyo.

        Fumbo la mateso na kifo cha Yesu halionyeshi uchungu kama jambo la kwanza kwa kutafakari bali upendo wake mkubwa hadi upeo. Kifo hakikuwa kulazimishwa kwa Yesu, bali jambo ambalo yeye alikubali kwa hiari. Yesu alijua kwamba alikuwa akifanya jambo sahihi na hivyo mateso yake ni mwanzo wa ushindi wake juu ya mauti, akifufua matumaini yote ya maskini na ya wanadamu wakosefu.

         Mateso ya Mwana wa Mungu yanatualika kutafakari kuhusu hali ngumu ya mateso ya binadamu. Kama Mungu alijibu kwa ufufuko mbele ya kifo cha Mwanawe, tunaweza kuhitimisha kwamba Mungu hataki mateso wala mauti ya watu. Yeye hawaachi wale wanaoteseka wala hanyamazi mbele ya mateso yao. Kristo alichukua kwa nafsi yake uchungu wa watu wote wa nyakati zote. Yeye anaendelea kuteseka wakati sisi tunahisi maumivu na majaribio katika safari yetu. Mfano wake unatuimarisha tuwe na kuwepo ufanisi maishani mwa watu wanaoteseka zaidi kuliko sisi. Misalaba ya mshikamano na huruma tunayoitwa kuchukua kila siku kama yeye alivyo inafanya kwamba kujitolea kwetu kuwe ishara ya upendo pia kama ushiriki katika mateso yake kwa ajili ya wokovu wa watu wote.

Fr Ndega

COLUI CHE MI HA MANDATO NON MI HA LASCIATO SOLO



Riflessione su Is 50,4-7; Fil 2,6-11; Mc 14,1-15,47


Stiamo iniziando la settimana più importante per le Comunità cristiane. Questa è la settimana che mette insieme gli avvenimenti centrali della nostra fede, narrando con molto simbolismo e profondità gli ultimi momenti di Gesù nella sua esistenza terrena e invitando alla contemplazione e al ringraziamento a causa di tanto amore. Questa è anche un’opportunità per riprendere il nostro cammino di impegno con il Signore e lasciarci motivare dal suo esempio di fedeltà e decisione.
Noi siamo invitati ad accompagnare Gesù che entra trionfante in Gerusalemme per concludere la sua opera d’amore. Infatti, egli non viene su un cavallo con arroganza e con un esercito potente come facevano i generali quando entravano nelle città, ma viene su un asino, pieno di bontà e misericordia come è stata tutta la sua vita. Gesù è consapevole di ciò che gli accadrà ma non si lascia abbattere. Al contrario, dimostra libertà di Figlio molto amato e mandato per salvare l’umanità. Mentre ricordiamo la sua entrata solenne nella città della pace, ricordiamo anche la sua passione e morte in questa città che ha la fama d’agire in forma violenta contro le persone mandate da Dio. Gesù muore non perché gli uccidono ma perché egli si consegna in totale libertà. Quindi, la sua morte non è una fatalità ma il risultato di una missione profetica vissuta con fedeltà fino in fondo.  
Come sappiamo, il profeta Isaia presenta quattro cantici per parlare della missione e identità del Popolo di Dio, che è anche chiamato “Servo del Signore”. Questi cantici sono stati composti durante l’esilio a Babilonia e li possiamo trovare nella seconda parte del libro di Isaia. Il testo che stiamo usando è il “terzo cantico”, e secondo questo, il Servo vive la sua vocazione come un dono di Dio per dare nuova vita ai suoi fratelli / sorelle. A causa della sua fedeltà, deve affrontare molte umiliazioni, rifiuti e sofferenze, ma non si scoraggia, perché si sente accompagnato e aiutato da Dio. Questo Servo è figura di Gesù che nella sua identificazione con la condizione umana, si umilia, accetta di essere maltrattato e ucciso a causa della sua fedeltà a Dio. La sua fiducia filiale in Dio è la ragione per la sua fedeltà. Per l’umiliazione ha trovato la via per la sua glorificazione. Il cammino di umiltà, dei piccoli gesti e l’opzione per ciò che è più insignificante nella società saranno i segni autentici che identificheranno coloro che continueranno la sua opera.    
La narrazione della passione secondo Marco porta all’inizio il gesto profetico della donna che spende un profumo di grande valore sul capo di Gesù. Egli chiedi che questo suo gesto sia sempre ricordato nel percorso evangelizzatore. Questa donna ci insegna a offrire al Signore della gloria ciò che è più prezioso, nella nostra vita. Più avanti nel contesto eucaristico, mentre esprime la sua fedeltà e il suo amore per i suoi, Gesù preannuncia anche il tradimento di un discepolo e la negazione dell’altro. La sua passione e la sua morte saranno uno scandalo per i suoi discepoli, perché loro avevano ancora la mentalità di un messia trionfalista. Tuttavia, continua il discorso parlando della risurrezione e dopo riprenderà con loro da dove tutto è cominciato, cioè, dalla Galilea.
Per Gesù non c’è più grande espressione di amore che quella di dare la vita per i suoi amici, anche se sono fuggiti (eccetto le donne e il discepolo prediletto, secondo il vangelo di Giovanni). Nel suo grido: “Dio mio, Dio mio, perché mi hai abbandonato”, ha espresso il dolore che davvero ha sentito come un essere umano, vale a dire, il dolore dell’abbandono, il dolore degli oltraggi, il dolore dei peccati dell’umanità, etc. E nel momento in cui tutto sembrava essere stato fatto invano, abbiamo la grande professione di fede: “Davvero quest’uomo era Figlio di Dio”.
Gesù è stato abbandonato dai suoi amici, ma lui non era solo sulla croce e mai è stato da solo nella sua missione. Viene dalle sue proprie parole questa testimonianza: “Colui che mi ha mandato è con me, non mi ha lasciato solo, perché io faccio tutto ciò che gli piace” (Gv 8,30). Così il “grido” che Matteo mette in bocca a Gesù deve essere riflettuto sempre in connessione con la sua fiducia filiale espresso nella versione di Luca, perché così è successo durante tutta la sua vita, vale a dire: “Padre, nelle tue mani consegno il mio spirito” (Lc 23,46). In caso contrario, sarebbe negata non solo la sua opera in intima comunione con il Padre ma anche la fedeltà di questo Padre.
Il mistero della passione e morte di Gesù non ha come primo riferimento il dolore e la sofferenza che egli ha vissuto, ma il suo grande amore fino alla fine. La morte non fu un’imposizione, ma un’accettazione volontaria, cioè libera. Gesù era consapevole che stava facendo la cosa giusta, e così la sua passione è l’inizio della sua vittoria sulla morte, facendo rivivere tutte le speranze dei poveri e di tutta l’umanità peccatrice.
La sofferenza del Figlio di Dio ci invita a riflettere sulla dura realtà della sofferenza umana. Come Dio ha risposto con la risurrezione alla morte del Figlio, possiamo concludere che Dio non vuole la sofferenza e neanche la morte delle persone. Egli non abbandona coloro che soffrono e non tace di fronte alla loro sofferenza. Cristo ha fatto suoi i dolori di tutte le persone di tutti i tempi. Egli continua a soffrire in noi quando sperimentiamo il dolore e le prove nel nostro cammino. Il suo esempio ci spinge ad essere presenza consolatrice nella vita di coloro che soffrono di più di noi. Le Croci di solidarietà e di compassione che siamo chiamati a portare ogni giorno come egli ha fatto, rende anche il nostro sacrificio un atto d'amore, come partecipazione nella sua passione per la salvezza di tutta l’umanità.

Fr Ndega

sábado, 17 de março de 2018

"TUNATAKA KUMWONA YESU"



Kutafakari kutoka Yeremia 31:31-34; Waebrania 5:7-9; Yoh 12:20-33

Kutoka maandiko haya tunaanza kutafakari kuhusu fumbo la “Saa” ya Yesu, ambayo inajumuisha mateso, kifo na ufufuko wake. Kwa kupitia Saa hii yeye atamtukuza Baba na atamaliza kazi yake. Kazi ya Mwana Yesu ndio wokovu wa ulimwengu ambao ingawa ulikwisha tendeka kwa wote lakini kila wakati unaomba kukubali kwa hiari kutoka kila mtu. Upendo wa Mungu uliofunuliwa na Yesu ndilo Agano Jipya ambalo liliandikwa moyoni mwetu na kutupa utambulisho wa Watu wa Mungu. Tunataka kumuona Yesu kwa njia yake ya kujifunua mwenyewe na kujifunza kutoka kwake kuishi kama chembe ya ngano ambayo inakufa ili kutoa mazao mengi.   

Somo la kwanza linaongea kuhusu Agano jipya ambalo Mungu ataanzisha na Watu wake. Litakuwa tofauti sana na Agano la kwanza lililoandikwa katika mawe nao watu walikosa kwa uaminifu. Tabia kamili kwa agano hili jipya ni uhusiano wa ndani kati ya Mungu na watu wanaoalikwa kuishi kulingana na Neno lililoandikwa na Mungu moyoni mwao. Basi, Mungu anaongea na watu wake kutoka moyo kwa moyo ili wajione kutibiwa kwa upendo na huruma. Bila msamaha hakuna maridhiano, tena hakuna furaha. Uaminifu na hisia ya kuwa watu wa Mungu itakuwa utambulisho mpya wa watu hawa: “Nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu”.

Kulingana na mwandishi wa Waraka wa Waebrania, kupitia utii kwa mapenzi ya Mungu, Yesu alianzisha Agano Jipya na kukubali kuteseka ili kutoa maana mpya kwa mateso ya binadamu. Uzoefu huu ulikuwa nafasi ya kujifunza zaidi maana ya utambulisho wake wa kibinadamu. Mfano wake wa kujisalimisha kwa upendo ni njia kuishi kama pendekezo kwa wote.

Injili inaongea kuhusu mkutano muhimu ambao ulianza kwa ombi: “tunataka kumwona Yesu”. mazingira ya tukio hili yalikuwa sherehe ya Pasaka ambayo Wagiriki na watu wengine walikuja Yerusalemu ili kushiriki pamoja na Wayahudi. Wagiriki walimkaribia Yesu kupitia Andrea na Filipi walio wanafunzi wake. Tamani ya Wagiriki ya kumwona Yesu ilikuwa zaidi ya udadisi wa kumwona mtu maarufu. Kitenzi “kuona” hapa kunamaanisha kujua kwa njia ya ndani kuhusu utambulisho wa Yesu. Basi, yeye alichukua nafasi ya kuwafundisha wanafunzi wake tena jinsi anavyotaka kutangazwa, yaani kama Masihi mtumishi ambaye alijisalimisha kwa upendo.

Tukio hili inatukumbusha ile la mwanzo wa injili ambalo wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walitaka kumjua mwalimu Yesu naye aliwaalika watembelee mazingira yake, yaani “mjoni nanyi mtaona”. Ni mwaliko wa kufanya uzoefu. Hakuna njia nyingine ya kumjua Yesu. Msingi wa injili hii ni ‘ ‘Saa’ ya Yesu. Neno hili ndilo muhimu katika injili hii ya Yohana. Tunaweza kukuta vifungu vingi ambavyo vinaongea kuhusu jambo hili. Yesu alijaribu kuelea akiutumia mfano wa Chembe ya ngano ambayo inakufa ili kuzaa mazao mengi. Hivyo, muhimu ya tafakari yetu sio kifo bali maisha mengi. Saa yake Yesu inajumuisha mateso, kifo na kufufuka. Ndio upendo ulimwimarisha Yesu kutenda hivyo.  Hivyo, mkutano wa kweli na Yesu ni kushiriki katika fumbo la kujisalimisha kwake.  

Kumwona Yesu ni hamu ya moyo wa binadamu, kwa sababu Yeye ndiye wa kipekee anayeweza kumdhihirisha Baba. Maisha yake ya kibinadamu yalikuwa bila utukufu daima (Kenosis, neno la kigiriki), akichukua njia ya mtumishi, kwa sababu alikuja kutumikia sio kutumikiwa. Hivyo, kila mtu anayetaka kumfuata anapaswa kufanya vivyo hivyo. Watu ambao wanatukaribia kumtafuta Yesu, hawataki tuongelee Yesu fulani kulingana na maneno yetu, bali Yule aliyejisalimisha kabisa kwa ajili yetu akikubali msalaba kama ishara kubwa ya upendo. Hivyo, hakuna njia nyingine ya kuwa wanafunzi wake wa kweli ila tukubali kuwa wa mwisho ili kuwa wa kwanza; kuyatoa maisha ili kuyapokea baadaye; kufa ili kuishi milele. Tunaweza kushiriki katika ushirikiano ambao Mwana anaishi na Baba ikiwa tuko na uwezo wa kuyatoa maisha kama Yesu. Mashahidi wengi wa historia ya Kikristo walikuwa na uhakika huu. Watu wengi wanaendelea wakifa ili wengine wengi waweze kuishi sio kwa njia yoyote bali kwa heshima. Kwa upande wetu, hakuna njia nyingine ya kuwa waaminifu kama wanafunzi wa Yesu ila kuyatoa maisha kama yeye alivyo. Kwa hivyo, "tunataka kumwona Yesu".

Fr Ndega

domingo, 11 de março de 2018

MUNGU ALIUPENDA ULIMWENGU HATA AKAMTOA MWANAWE WA PEKEE



Kutafakari kuhusu Yoh 3, 14-22


            Baada ya tukio ambalo Yesu aliwafukuza watu nje ya hekalu, mkuu mmoja wa Mafarisayo aliyeitwa Nikodemo alimtafuta Yesu wakati wa usiku ili kukutana nawe. kukutana na Yesu ni hamu ya moyo wa binadamu. Lakini ni lazima kutambua ikiwa yeyote anamtafuta Yesu ni kwa sababu Yesu alimtafuta kwanza. Kukutana na Yesu ni kukutana na Mungu, kwa sababu Yesu mwenyewe alisema, “yeyote anayeniona mimi anamwona Baba,” na “mtu anayenikaribisha mimi anamkaribisha Yule aliyenituma.” Nikodemo alishangaa kwa sababu ya tabia ya Yesu ya kinabii, lakini alipendelea kubaki amefichwa kwa sababu ya hofu ya wenzake Mafarisayo.

Tunakuta vifungu vingine viwili ambavyo Nikodemo alionyesha upatikanaji fulani kwa ajili ya Yesu. kifungu kimoja ndicho wakati alipowakumbusha wenzake wa Baraza kuu wa Wayahudi kwamba Sheria hairuhusu kumlaani mtu bila kumhukumu. Katika kifungu kingine alionekana pamoja na Yosefu wa Arimathaya ambaye alimwendea Pilato na kumwomba apewe mwili wa Yesu. Kulingana na toleo la Mathayo Yosefu alikuwa mwanafunzi wa Yesu. Ingawa Nikodemo alikuwa kiongozi wa Mafarisayo na Yusefu wa Arimathaya alikuwa mmoja wa Baraza kuu wa Wayahudi, wote wawili ni mfano ya kumtafuta Yesu.

Ishara ya Yesu hekaluni iligusa ndani ya Nikodemo. Ile ilikuwa nafasi kwa kuitafuta nuru kwa sababu labda aliona kwamba maisha yake alikuwa kama usiku na giza. Katika sehemu ya mwisho ya kifungu hiki cha injili jambo hili la usiku/giza linatumika kama ishara ya upinzani dhidi ya pendekezo la Yesu aliye nuru ya dunia na kumwita kila mtu aje kwenye nuru ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu. Ni tabia ya mwinjilisti Yohane mwenyewe kusisitiza kuhusu tofauti kati ya baadhi ya maneno kama haya, mfano, giza na mwanga ama usiku na asubuhi/mapambazuko ama mbingu na dunia, akionyesha haja hali ya Mungu katika hali yetu.

Yesu alijali tukio la nyoka ambaye Musa alimwinua jangwani kama mfano ya kuinua kwake kwa njia ya msalaba ili kila mtu awe na uzima wa milele. Kazi ya wokovu wa ulimwengu ni kazi ya upendo mno wa Mungu ambaye “aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee”. Hii ni sehemu ya msingi wa andiko hili. Ndio upendo maana ya ishara ya Baba akimtoa Mwana wake kwa ajili ya wokovu wetu. Basi, hatuwezi kutafakari jambo la msalaba peke yake bali kama maonyesho na matokeo ya maisha mazima yalitolewa kwa upendo. Tena kwa sababu ya upendo baada ya msalaba tuko na ushindi wa uzima juu ya mauti. Imani katika Yesu inatufanya kuonja uzima wa milele kwa kutarajia wakati tuko bado duniani. Kwa hivyo misalaba sio aibu kama Wayahudi walivyofikiri wala wazimu kama walivyofikiri Wapagani bali ni kutukuzwa kwa Kristo na wokovu wetu.

Mwendo wa kutukuzwa kwa Kristo unaifuata njia ya kuwa tupu na kujinyenyekeza. Tunaweza kukuta maoni hayo katika waraka wa Mtakatifu Paulo kwa Wafilipi (Fil 2, 5-9a): “Yeye ingawa alikuwa sawa na Mungu, hakuona kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya si kitu, akajifanya sawa na mtumwa, akazaliwa katika umbo la mwanadamu. Naye akiwa na umbo la mwanadamu,  alijinyenyekeza hata mauti, naam, mauti ya msalaba! Kwa hiyo, Mungu alimtukuza sana”. Kwa hivyo tuko na tumaini. Mateso na mauti hayana neno la mwisho wala hayawezi kuyatawala maisha yetu. Hivyo, hatuwezi kutafakari msalaba bila ufufuko. Ndio upendo ambao unaimarisha Yesu kwa kujisalimisha kwake. Ni kwa sababu ya upendo wanafunzi wake wataendelea kazi yake na kujitolea kama vile yeye. Ni kwa sababu ya upendo sisi sote kama Wakristo tunaweza kuishi maisha mapya na kutangaza kwa furaha ukaribu wa Mungu na mambo makuu ambayo yeye anaendelea kutenda kwa ajili ya wokovu wetu. Tuwe macho kwa ishara ya upendo wa Mungu katika hali yetu na kupatikana kama Nikodemo kwa kukutana nawe na kubadilisha mawazo yetu na njia yetu ya kuishi.

Fr Ndega

sábado, 3 de março de 2018

UHUSIANO MPYA KATI YA MUNGU NA WATU WAKE



Kutafakari kuhusu Kut 20: 1-17; 1Wak 1, 22-25; Yoh 2, 13-25

Maandiko Matakatifu yaongea kuhusu uhusiano maalum kati ya Mungu na watu wa Israeli. Yeye alianzisha agano na watu hawa akiwapa miongozo ili watembee salama na kufanya mapenzi ya Mungu. Katika hali halisi hii, amri kumi zilizaliwa. Kuishi Amri ilikuwa jambo muhimu katika safari ya Watu wa Israeli ambao wanafikiria Sheria kama Neno la Mungu na Neno la Mungu kama Sheria. Basi kuna uhusiano wa ndani kati ya Sheria na Neno la Mungu. Kupitia Sheria au Amri, Mungu anaonyesha utunzaji kwa watu wake na kuonyesha njia ya ukombozi.

Wakati watu wanafuata miongozo hii wanaweza kuona Baraka za Mungu, lakini wakati wanachagua ukosefu wa uaminifu matokeo ni kifo. Kidogo kidogo muhimu ya Sheria ilikuwa ikisahauliwa na kubadilishwa kuwa ni mawazo ya kibinadamu. Hali hii ilizaa aina ya dini ambayo haikuzaa matunda tena.  Ilipaswa kuchukua tena maana ya kweli ya Sheria kwa ajili ya kuanzisha tena uhusiano mpya na Mungu kupitia Agano mpya na milele. Iliwezekana kupitia Kristo, aliyejulishwa na Mtakatifu Paulo kama nguvu na hekima ya Mungu.

Katika injili tuko na tukio la kutakasa kwa hekalu. Katika wainjilisti wengine tukio hili lilijulishwa katika sehemu ya mwisho ya injili yao wakati alipoingia Yerusalemu ili kuteseka mateso yake. Kwa upande wa mwinjilisti Yohana ni tofauti, yaani anaweka tukio hili mwanzoni mwa injili yake. Kisha, Yesu alienda mpaka Yerusalemu na kuona huko hekaluni watu wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. Alihisi hasira fulani kwa sababu ya hali ile na mara akatengeneza mjeledi wa kamba na kuwafukuza wote nje ya hekalu. Katika mwanzo wa tukio hili hakuna mtu ambaye aliweza kufahamu tabia hii ya Bwana Yesu. Mara nyingi walikuwa na mazoea ya kumwona Yesu akitenda kwa huruma na upendo na unyenyekevu. Hawakutarajia kwamba aweze kutenda hivyo. Basi, tujaribu kufahamu maana ya tabia ya Yesu.

Watu walikuwa wamebadilisha mahali pa sala kuwa hali ya biashara. Alipowatoa wote hekaluni, Yesu alionyesha hamu yake kwa nyumba ya Mungu na hasira fulani kuhusu tabia ya kutoheshimu kwa Hekalu. Bila shaka mambo ambayo yalitendeka hekaluni yalitafsiri aina fulani ya dini iliyoko. Kwa  uwepo wa Yesu duniani aina hii ya dini imeisha na uhusiano wa kibiashara na Mungu imeshindwa. Uwepo wa Yesu unatangaza wakati mpya. Katika nafsi yake tunakuta Hekalu mpya, yaani mahali pazuri mno pa mkutano na Mungu. Katika Yesu mtu anaweza kukutana na Mungu kwa kweli. Mafundisho yake yaliwasaidia watu watafakari vizuri kuhusu lengo la Hekalu na tabia kamili kuhusu mahali huko. Msingi wa mafundisho yake ni kumwabudu Baba kwa Roho na ukweli. Hiyo ndiyo maana ya kuwa mwanafunzi wa Kristo, yaani kuwa hekalu pamoja naye.

Wale wanaokuwa wanafunzi wa Kristo wanaalikwa kuwa naye Hekalu jipya ambapo Mungu anaishi. Kwa njia ya ubatizo tumezaliwa upya kwa njia ya kiroho. Kwa njia hii tunabadilishwa kuwa mahekalu hai, yaani na makao yake Mungu. Kila mmoja wetu ndiye jiwe la ujenzi mkubwa unaoitwa Kanisa ambalo ni mwili wa Kristo na jumuiya ya imani na upendo. Kama mawe hai tunaalikwa kutenda pamoja kupitia ushuhuda wa maisha ili ujenzi huu kutimiza lengo lake. Utunzaji kwa urembo wa nje wa kimwili ni mzuri, lakini hauwezi kutuzuia ya kujali hekalu hai la Mungu ndipo ndani yetu. Hiyo ni kauli ya Mtakatifu Paulo katika waraka wake kwa Wakorintho: “Ninyi ni hekalu la Mungu na Roho wake anakaa ndani yenu”. Kweli kama jumuiya ya Kikristu tunaimarishwa na Roho wa Mungu ili tuweze kuzaa matunda mazuri, kwa kuwa vyombo vya wokovu wake. Imani tunayoishi katika jumuiya inatufanya mashahidi wa kweli. Ushuhuda wetu unatangaza ukaribu wa Mungu na hali mpya ambayo Yesu alileta katika nafsi yake mwenyewe.

Fr Ndega