Kutafakari kuhusu Mk 9, 2-10
Nafasi hii injili inajulisha kugeuka sura kwa
Yesu na mwaliko wa kugeuka sura kwetu wenyewe, hasa katika wakati huu wa
Kwaresima. Tunaweza kukuta tukio hili tena katika wainjilisti wengine, yaani
Mathayo e Luka, kwa tofauti fulani, kulingana na mwinjilisti mwenyewe. Kwa
mfano, mara mwanzoni mwa andiko hili la Marco, tunakuta maneno “baada ya siku
sita”. Tena tunakuta maneno haya katika Mathayo lakini katika Luka ni tofauti
kidogo, yaani “takriban baada ya siku ya nane”. Basi, tuanze kutoka tukio
lililotokea siku sita ama ya nane ya injili ya leo, yaani Yesu alitangaza
kujisalimisha kwake na kujulisha mahitaji ya kumfuata. Kisha, Yesu alichukua
wanafunzi wa tatu na kupanda mlima mrefu. Mlima una maana kubwa katika biblia.
Kama jangwa, tuliyotafakari mara iliyopita, mlima ni pia mahali maalum pa
uzoefu wa Mungu. Yesu alipanda mlimani mara nyingi na matendo yake mengi
yalitokea huko.
Kulingana na desturi ya Kikristo, mlima wa
kugeuka sura unaitwa Tabor, wengine watalaam wa Biblia wanasema kwamba huko ni
mlima Hermon. Hata hivyo, ni muhimu kujua kwamba ulikuwa mlima mrefu na huko
Yesu aligeuka sura mbele ya wanafunzi wake. Mwinjilisti Marko anaongea kuhusu
mavazi ya Yesu lakini haongei kuhusu uso wake kama tunavyokuta katika injili ya
Mathayo. Yesu aliwaonyesha kidogo utukufu wake na hali ijayo ya maisha ya wale
wanaomfuata kwa uaminifu. Yesu aliwaalika kwa uzoefu wa juu ili waone vizuri
hali ya kujisalimisha kwake na hali wanayoalikwa kuichukua kama ushiriki katika
kazi ya Mwalimu wao. Basi, sio Yesu peke yake aligeuka sura bali wanafunzi pia
walivyo kwa sababu waliweza kuona tofauti.
Uwepo wa Musa na Elia unaeleza kuhusu rejeo la
ufunuo katika Agano la Kale. Wote wawili waliongea na Yesu wakionyesha kwamba
hakuna kupasuka kati ya mafundisho yao na yale ya Yesu, bali uhusiano na
mwendelezo. Lakini kulingana na sauti iliyosikika kutoka kwenye wingu ndiye
yeye kwa uwezo wa kufundisha na kutafsiri kamili yale yaliyosemwa na mababu wa
zamani. Baba alishuhudia kwa upendo kuhusu Mwana wake, akimweka kama rejeo la
maisha yetu, yaani, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, msikilizeni”. Wote wanaalikwa
kumsikiliza. Kusikiliza katika Biblia ni kitenzi chenye nguvu sana. Hii ni
tabia kamili ya mtu mbele ya Neno la Mungu, akifanya mazoezi kuhusu yale aliyosikia.
Basi, kusikiliza kuna uhusiano wa ndani na kushika/kutenda.
Yesu ni ufunuo wa kipekee wa Mungu. Hakuna
mwingine ambaye aweze kumdhihirisha Mungu kama Yesu alivyo. Kweli Mungu
aliongea wakati wa zamani kwa mababu zetu. Lakini “siku hizi” mambo yote Mungu
anayoendelea kudhihirisha kwa watu anafanya kwa njia ya Mwanawe Yesu. Hata wale
ambao hawamjui Yesu wanapokea ufunuo wa Mungu kwa njia yake. Katika kila ndugu
wanayemsaidia wanaweza kukutana na Kristo ambaye alijitambulisha na walio na
mahitaji mengi (cf. Mt 25,31-46). Kipimo ni upendo/huruma. Matendo yao ya
huruma yanaongelea Kristo.
Wanafunzi walitamani kubaki mlimani, lakini
sauti iliyotoka mbinguni ikawaalika kumsikiliza Yesu na kutoka nje ya uzoefu
huu wamepatikana kuandamana naye mpaka upeo. Mara nyingi Mungu ametualika
kufanya uzoefu wa uwepo wake kama ilivyotokea kwa wale mlimani, mfano, wakati
tunaposhiriki katika sherehe fulani ama siku za maombi, uzoefu wa undugu na
kadhalika. Uzoefu kama huu unaiimarisha imani yetu na hamu yetu kwa ajili ya
kazi ya Mungu. Lakini safari yetu yapaswa kutendeka kati ya “kupanda mlimani”
(mfano wa uzoefu wa Mungu wa kibinafsi) na “kushuka mlimani” (mfano wa
changamoto za undugu na kazi). Kila siku tunaalikwa kufanya uzoefu wa “kugeuka
sura” kupya kwa kusikiliza Neno la Yesu na kufanya mazoezi kuhusu Neno hili.
Uzoefu huu unatusaidia kutambua uso wa Yesu katika nyuso za ndugu wengi
kandokando yetu na kuona hisia na tabia za yake kwa ajili yao. “Kusikiliza neno
lake kunatupatia nguvu ya kumfuata mpaka mwisho.” Hii ni njia kamili ili tuweze
pia kuishi kama “wana wapendwa” wa Mungu.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário